Sunday, April 7, 2013

SIRI YA UZURI PART 2

Asalaam Aleiykum,

"ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ طِبَاقً۬ا‌ۖ مَّا تَرَىٰ فِى خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ مِن تَفَـٰوُتٍ۬‌ۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ۬ ٣) ثُمَّ ٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ كَرَّتَيۡنِ يَنقَلِبۡ إِلَيۡكَ ٱلۡبَصَرُ خَاسِئً۬ا وَهُوَ حَسِيرٌ۬ (٤) وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَـٰبِيحَ وَجَعَلۡنَـٰهَا رُجُومً۬ا لِّلشَّيَـٰطِينِ‌ۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ "
"Ambaye ameumba mbingu saba zenye Tabaka,(Moja baada ya nyengine)huoni tafauti katika uumbaji wa mwingi wa Rehma, ikisha rejesha macho, je unaona kosa(Lolote)(3).
ikisha rejesha tena macho (yako)mara nyingi zaidi, litarudi jicho lako hali yakua limehizika na kuwa chovu (Kuchoka)(4) Na hakika tumeipamba  mbingu ( hii ya)Dunia kwa mataa, na tumeyafanya(Majinga ya Moto)kuwapigia mashetani, na tumewaekea adhabu ya moto uwakao (kwa nguvu)"
Naam hiyo ndio hali ya huko juu na hapa chini huwezi kuona tafauti, hakuna makosa katika uumbaji wa Mwenye-enzi-Mungu huwezi kukuta chochote chenye kukosewa ndio maana ukatakiwa angalia sana, rejea kuangalia mara nyingi, na kweli ukiangalia sana mbingu jaribu nusu saa tu uitizame mbingu basi utaona macho yamejaa lepe lepe la usingizi(jaribu utaona)jicho linavo choka. Aya ikaendelea kusema tukaipamba mbingu kwa mataa, kumbuka Mwenye-enzi-Mungu anatwambia tazameni mapambo ya mbingu, yaonesha binaadamu tunaishi katika Ulimwengu huu hatuyaoni mambo mazuri yalotuzunguka, na vipi wewe utaona uzuri wa Mbingu ikiwa Mkeo huwezi kumuangalia Uzuri wake, ikiwa huoni cha karibu vipi utakiona cha mbali na kama unabisha hayo kama wewe huoni mazuri wacha tuangalie mfano huu, halafu utajua wewe unayaona mazuri au uzuri wa Ulimwengu huu au kinyume chake huoni kabisa.
Mambo mazuri katika Ulimwengu huu yapo mengi na yametuzunguka lakini masikini tumekua vipofu hatuoni chochote, katika ulimwengu huu mpaka ndege wana rangi nzuri, nyota zina uzuri wake, kipepeo ana uzuri wake, njiwa ana uzuri wake, tausi kapambwa kivyake,maua yana uzuri wake kila jambo lina uzuri wake tumezungukwa na mambo mazuri, tunaishi katika ulimwengu mzuri, kila kilichomo kizuri, mpaka maisha yako mazuri, wewe mwenyewe mzuri, lakini matatizo yetu wanaadamu hatuyaoni kabisa mazuri haya, na siyo hatuyaoni bali hata kuyajua hatuyajui kabisa, na mfano kama kilivyo kichwa, bila ya kichwa kuumwa unajua kama una kichwa si mpaka kiume, hiyo ndio hali ya uzuri ilivyo tunaishi ndani ya Uzuri lakini maskini Roho zetu zina ukungu hatuoni uzuri wowote uliomo katika Ulimwengu huu, Na kama unakaidi hilo jiulize wewe mwenyewe kwa siku unayaona mazuri mangapi, hebu kumbuka japo leo mazuri mangapi umepishana nayo na hujayagundua.
Vipi wewe utayagundua mazuri wakati huwezi hata kumgundua mke kavaa(Dish Dasha)la Rangi gani, Jitizame sasa hali yako ukirejea nyumbani unakuwaje, ukifunguliwa mlango swali lako la mwanzo unauliza hamjalala, alaa anolala anafungua mlango, unakuta nyumba ina harufu nzuri za udi unauliza mbona kunanukia, sasa wacha uwekewe chakula uone vipi umelala, hupo kabisa, hata mkeo humtizami usoni, eti wewe ndio unaona haya, una jambo gani wewe hata huoni uzuri wa mkeo, sasa ngoja uwekewe chakula uone nini kinatokea, pengine kuna Biriani na ndizi mbivu, au zimewekwa katlesi na venginevyo, basi unaweza kuishika Biriani (Wallahi)huku unafikiri kisambu cha hawara, unakamata katlesi unafikiri sijui yule kimada kawatia wale samaki kwenye friji, au utafikiri mpira au mambo ya barazani mpaka mkeo akuonee huruma tena anakuamsha chunvi iko sawa ndio unakuruka usingizini, sawa, unashindwa hata kusema chakula kitamu, vipi leo utaona mazuri, utajuaje nini kizuri, wakati kizuri kiko mbele yako hukioni anakwambia Mollah wako katika sura ya Tin aya ya nne.
" لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ فِىٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٍ۬" Tumemuumba mwanaadamu  kwa umbo lilo bora kabisa" vipi leo huwezi kugundua uzuri uliopo katika mambo yote yalokuzunguka, na kwanini hutaki kujua sababu za kutokuona kwako, lazima kuna pahala unafanya makosa fulani ndio maana umenyimwa neema hii ya kuona mazuri katika Ulimwengu huu. Sasa kama nilivyo ahidi nitarejea kwa dada zetu ikisha nijulishe wapi uzuri unatokea na ufanye nini ili upate kuona vizuri. Endelea part 3

No comments:

Post a Comment