Sunday, April 14, 2013

UKOMBOZI WA NAFSI PART 2

Asalaam Aleiykum,

Umefika wakati unahitaji ukombozi wa nafsi yako ili  yasije Mauti yakakukuta katika hali hiyo, ili upate kuokolewa kutoka katika makucha ya Shetani na Wanaadamu wenzio, nini cha kufanya ili uokoke, lakini huwezi kujiokoa kama hujui matatizo yako, wacha tuzidi kupata mfano ili iwe fundisho kwetu na kwa wengine, itizame Nafsi yako ilivofunikwa na wimbi la maonesho, Jitizame kama wewe Imam vipi inakua hali yako katika kusalisha, unaanza na Sala nia yako ipo kwenye sauti sijui nzuri, inapendeza, nimetia shada, pale nimevuta, sijui mguu nimeweka sawa, ukiwa katika kufunikwa na hali kama hiyo jua hiyo si Sala, kwenye Sala, yule anosali anapotea kabisa na anabakia Mwenye-enzi-Mungu, ukijiona unachunguza Sala za wenzio mguu umekaa vipi, na hivi na vile basi jijue unahitaji ukombolewe kwani Nafsi yako haitaki kujitupa kwa ukamilifu kwa Mollah wako.
Itizame Nafsi yako ilivozama kwenye maonesho ukiwa na Elimu basi lazima matabu yajae nyumbani kwako, watu watajuaje,Umezidi maonesho mpaka ukinunua soksi lazima watu wajue, ukinunua saa au nguo mpya na ikawa watu hawajatambua basi unaweza kuumwa kwanini watu hawajajua, sijui mbaya au wamenidharau, ukihifadhi aya tatu kwenye Quraan mji mzima unataka uelewe wewe shekhe, ukihifadhi hadith mbili tatu unataka uonekane umeshika dini, na ukija kutafakari zaidi utaona unajitangaza mpaka kwenye maasi, jana nilifanya jinsi kadhaa wa kadhaa, hata ukija zinduka wapi Ibilis  kakuzunguka kila pembe hutoki tena na huku watu wanazidi kukupigia makofi endelea tutakua pamoja (Motoni). Ukiangalia Mwanaadamu wewe hufanyi chochote kwa ajili ya Mollah wako, kumbuka kipi unachofanya kwa ajili ya yule Alokuumba, kawaida yako imekua hivi mazuri yote unayatangaza, na yale mabaya yote unamkusanyia Mwenye-enzi-Mungu na huku ukisema   nisitiri wasijue, nivue usiniadhibu, nilinde nisiadhirike, naomba nisidhurike. hiyo ndio Nafsi yako ilivyo mpaka wakati huu, hayo ndio machache niliyo yataja, lakini kuna mengi ambayo Nafsi inayajua.
Sasa ufanyeje ili ujifungue katika hicho kifungo cha nje, hakuna jengine ila kurejea katika Nafsi yako uanze kufuta mavumbi ili upate kuwa safi, ungare.
Muulize Mollah wako anasemaje katika kadhia hii ya Ukombozi, ufanye nini ili uwe safi na kujiepusha kabisa na maonesho hayo ambayo umeishi nayo miaka yote mpaka kufikia hivi sasa. Anasema Mollah wako usi ishi Maisha ya kujionesha,kwani ukifanya hivyo utashughulika zaidi na wanaadamu wenzio na kumsahau moja kwa moja yeye Muumba, Ila umepewa Ruhusa ya (Kuhadithia)kumbuka kujionesha na kuhadithia ni vitu viwili tafauti, na Ruhusa yenyewe imo katika sura ya Dhuha aya ya 11
"وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ"
"Na Neema ya Mollah wako Ihadithie"
Vipi Utahadithia Neema za Mollah wako zipo nyingi sana, basi ziseme japo hizo chache, Nilikua nimepotea Mollah wangu kaniongoza, nilikua si Sali sasa na Sali, Nilikua simkumbuki haijambo nimeanza kidogo kidogo kumkumbuka, Nilikua nalewa sasa nimeacha, nilikua nazini lakini sifanyi tena, nilikua nikisema watu nimeacha,mambo yote ya haram najiepusha nayo. Akanikuta Mollah wangu maskini lakini nashukuru sasa kidogo mambo mazuri, riziki yangu sasa napata kwa wepesi, hivi sasa najiweza japokua Mollah wangu hajanipa utajiri lakini pia siombi, na mtu akija kuniomba simfukuzi nafanya bidii kuhakikisha naitatua shida yake,Nilikua mgonjwa sasa sijambo na kwa ajili hiyo naona Nafsi yangu nyepesi kwa hivi sasa, na mimi nimejifunga kuyaelekeza maisha yangu kwa ajili ya Mollah wangu pekee.Endelea part 3

No comments:

Post a Comment