Sunday, April 28, 2013

SINA CHA KUFUNDISHA PART 3

Asalaam Aleiykum,

Ikiwa mtu kakudanganya yeye anafundisha, yeye anajua yasojulikana basi irejee Quraan sura ya Baqarah aya ya 31uone inasemaje."
"وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَہُمۡ عَلَى ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِى بِأَسۡمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمۡ صَـٰدِقِينَ "
"Na akamfundisha (Nabii Adam a.s)majina ya vitu vyote, ikisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema (Kuwaambia)Niambieni majina ya vitu hivi ikiwa mnasema kweli" hivo ndio kufundishwa, ukishajua sasa unaambiwa waambie (wasomeshe majina ya vitu hivi)Vipi kufundishwa, inayofundishwa ni Roho na inayosomeshwa ni akili, vipi inakua, mchukue mtoto mdogo halafu muoneshe embe atajua hiki ni kitu, atakua yeye na kitu anakiona lakini hajui ni kitu gani(Nambieni ikiwa mnasema kweli)mtoto hawezi kusema atakaa ana shangaa halafu atakuuliza hichi nini? Ukimjibu hii inaitwa Embe hapo inakua ushamsomesha, ushambadilisha akili yake, ushatia jina na sasa kila akiona Embe atakua anaikumbuka kwenye (Memory)yake, akiiona tu anaijua (Embe dodo hiyo)Vipi leo mimi nitakua na kitu cha kufundisha.
Sasa ikiwa na wewe unataka kugundua vipi unafundishwa na Mollah wako, kuwa mtulivu, kaa kimya,kaa itikafu, sikiliza ujumbe gani unakuja katika nafsi yako, fanya Ibada za usiku kwa wingi, ghafla utaanza kufungukiwa na elimu ya kujua, najua unajiuliza nitajuaje, hapo itakua Akili ishaingilia kati, na Akili ikiingia ndio unaambiwa sasa soma kwa Jina la Mollah wako alo Mkarim, kwani unajuaje sasa nyanyua mguu, vipi unatambua sasa toa sauti, nenda kalale, kule kuna hatari, kisu kinakata, hii chai ya moto, lile jua hayo ndio machache katika kufundishwa ama kusoma ni (Faculty) ya Akili, kusoma ni kilele cha kufundishwa, kufundishwa ni (Knowing) na kusoma ni (Knowledge) ndio utaona viwili hivi vikikutana utasikia mwanafunzi huyu hodari, na vipi asiwe hodari na yeye kapewa vitu viwili kwa wakati mmoja, na vikikutana viwili hivi ndio anapatikana Sheikh, au Mwalimu, anapatika Mwenye (Degree) au (Professor) na kama hujapata vyote utakua na kimoja chake, ima msomi bila ya hekima, au utakua na hekima bila ya kusoma, namie nawependa wote na nawahimiza sana watu wasome kwani hekima unakua nayo lakini usomi unatafutwa, na mie nawapenda wasomi wanopata vyeti vyao wakapata Riziki zao za halali na kuleta maendeleo katika jamii zao, hiyo ndio maana ya Elimu, kutolewa kwenye giza lolote kupelekwa kwenye Nuru, na hiyo ndio maana ya aya hii." وَوَجَدَكَ ضَآلاًّ۬ فَهَدَىٰ" "akakukuta umepotea akakuongoa"
Yaa Aalim tupe elimu ya kukufahamu weye na Ufalme wako ulotuzunguka, Tuongoze katika Nuru, ututoe kwenye giza.Amin.

No comments:

Post a Comment