Sunday, April 14, 2013

UKOMBOZI WA NAFSI PART 1

Asalaam Aleiykum,

Nini Mapinduzi? Mapinduzi ni kitu chochote kilogeuzwa, kinaweza kuwa kiti au meza, yaweza kuwa sufuria au Nchi, lakini kuwa na hakika chochote kile chenye kupinduliwa hakitokaa sawa mpaka kirejeshwe katika hali yake ya mwanzo au kama kilivokua, kinyume na hilo hakuna mategemeo ya kukaa sawa daima, na mifano iko mingi ya nchi na mengineyo wenyewe mtachunguza.
Nini Ukombozi?
Ukombozi ni tendo la kutolewa katika hali ya ulazimishwaji, iwe kulazimishwa huko kwa udanganyifu au mbinu ya hila za nguvu, au hadaa ya hiyari ilokupelekea mpaka ukakubali kutawaliwa na jambo husika lenye madhara na wewe, kama vile kutekwa nyara na ukawa huna uwezo wa kujikomboa. Mimi nina uhakika yakwamba kila mmoja wetu ni mahabusu(Mfungwa)wa ima Shetani au Mwanaadamu mwenzio, lazima katika wawili hao mmoja kakuteka nyara, Ikiwa sio mahabusu wa Shetani basi itakua Mwanaadamu mwenzio kakumiliki katika sehemu zote au chache zilobakia, kwa ajili hiyo sasa imekujia darsa hii ya Ukombozi ili upate kuokolewa katika hicho kifungo chako cha khiyari, ili utoke katika (Jela)hii inatakikana mbinu imara za kuifungua minyororo ilo kuzunguka kwenye kila kiungo chako.
Sasa kwanini unatakikana Ukombozi huu wa Nafsi? Sababu kubwa kabisa ya kwanza inayo kufanya uhitaji ukombozi huu ni ile ilokufanya Umsahau Mollah wako, Ambaye kwa Mapenzi yake yasopimika kakupa uhai huu unaoufanyia mzaha kwa wakati huu, Na ukiitizama Nafsi yako imetawaliwa na Maonesho matupu, katika maisha yako imekua kila kitu chako ni lazima kiwe cha shirika, sasa virejee vitendo ntakavo vitaja hapa halafu kwa ukweli wa nafsi yako jiulize mimi ninazo tabia hizi au ni porojo tu.
Umeingia wewe katika (Showing off)hii kuanzia kwenye nguo mpaka chakula, mpaka mazungumzo yako ukijisikiliza utajua nimekusudia nini, Imefunikwa Nafsi yako kiasi ambacho huwezi hata kukumbuka kujiridhisha wewe Mwenyewe au Mollah wako.
Ukisali kwa ajili ya watu, ukitoa Sadaka kwa ajili ya watu wajue unatoa, ukimsaidia mtu kama hutaki kulipwa lakini unailazimisha Nafsi ya huyo ulomsaidia akunyenyekee au akukumbuke daima kwamba ulimsaidia, ukijenga Nyumba kwa ajili ya watu, ukinunua gari lazima watu watambue, imezungukwa Nafsi yako na (Khofu) ya watu mpaka inakua kutwa nzima maisha yako ni kuridhisha watu, na watu ndio watu, kama hujawaridhisha wanageuka kuwa mahasimu zako, hapo unakuanza ugonjwa wa wasiwasi,(Unasema Kichwani kwako kutwa) sijui kaniona, ama kafanya kusudi, Mbona anatenda dhambi, yule anakwenda motoni umejitahidi mpaka umechukua cheti cha Uhakimu sasa, umejibebesha mzigo wa mateso ambayo yanaweza kuepukika kirahisi kabisa na tena bila ya ugumu wowote.
Kwa hali hiyo wewe sasa unahitaji Ukombozi ambao utakutana nao Part 2

No comments:

Post a Comment