Sunday, April 21, 2013

MWANAFUNZI WA KASUKU PART 2

Asalaam Aleiykum,

Sasa uwe vipi, kuwa kama ndege (Hud Hud)yeye alikuwaje, itabidi tumuulize Nabii Suleiman a.s katika kisa cha Quraan alikuwaje (hud hud)Sura ya Naml aya ya 20,21,22,23,24

" وَتَفَقَّدَ ٱلطَّيۡرَ فَقَالَ مَا لِىَ لَآ أَرَى ٱلۡهُدۡهُدَ أَمۡ ڪَانَ مِنَ ٱلۡغَآٮِٕبِينَ"
Akawakagua Ndege(ikawa hudhud hayupo)Akasema imekuaje mbona simuoni Hud Hud, au amekuwa miongoni mwa wasiokuwepo hapa.
" لَأُعَذِّبَنَّهُ ۥ عَذَابً۬ا شَدِيدًا أَوۡ لَأَاْذۡبَحَنَّهُ ۥۤ أَوۡ لَيَأۡتِيَنِّى بِسُلۡطَـٰنٍ۬ مُّبِينٍ۬"
Kwa yakini nitamuadhibu adhabu kali, au nitamchinja au ataniletea hoja iliyo wazi.

" فَمَكَثَ غَيۡرَ بَعِيدٍ۬ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمۡ تُحِطۡ بِهِۦ وَجِئۡتُكَ مِن سَبَإِۭ بِنَبَإٍ۬ يَقِينٍ"
Basi hakukaa sana mara (Hud Hud akatokea)akasema, Nimegundua usilogundua, na ninakujia kutoka (Mji unaoitwa)Sabaa na (Nakupa)habari yenye yakini.
Naam:usiwe kama Kasuku,  hivi ndivo inavotakiwa uwe kama Hud Hud hakuogopa kuadhibiwa au hata kuchinjwa kenda huku na huko(Na hii ndio ile maana ya katafuteni elimu mpaka Uchina)pita hapa na pale usiogope, soma kwa huyu na yule, usisubiri mpaka Sheikh au Mwalimu akupe ruhusa, Hud Hud hakutaka hata ruhusa kenda kugundua ambayo Nabii Suleiman a.s bado hajagundua na elimu yote aliyopewa, na wewe katafute ugundue mji wa elimu ili uje kutupa habari za yakini, sio mambo ya (copy)Sheikh fulani kasema, iwe ndio sawa tu, haiwezekani, usije ukaganda pahala pamoja utafungika kama Kasuku kwenye tundu lake na watu wakufunike, chuma hapa na pale ili maisha yako yapate kubadilika kwani elimu ndio njia pekee itakayo kutoa kwenye Giza kukupeleka kwenye Nuru, Soma ugundue jambo jipya kama Hud Hud, na kama hujagundua au kuendelea basi jijue wewe Kasuku wala usione haya kasuku pia ndege.
Naam nini kagundua Hud Hud, na habari gani hiyo yenye yakini,
" إِنِّى وَجَدتُّ ٱمۡرَأَةً۬ تَمۡلِڪُهُمۡ وَأُوتِيَتۡ مِن ڪُلِّ شَىۡءٍ۬ وَلَهَا عَرۡشٌ عَظِيمٌ۬"
Hakika nimekuta mwanamke anatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa.
Kapewa Mali na uzuri, na nchi yake ya Sabaa ilikua nzuri, na kiti alichokua akikalia kilikua cha aina ya pekee, na kikubwa cha kutawala Malkia.
"وَجَدتُّهَا وَقَوۡمَهَا يَسۡجُدُونَ لِلشَّمۡسِ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ أَعۡمَـٰلَهُمۡ فَصَدَّهُمۡ عَنِ ٱلسَّبِيلِ فَهُمۡ لَا يَهۡتَدُونَ "
Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenye-enzi-Mungu, na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia(Za Kheri)kwa hivyo hawakuongoka.
Hebu na wewe jaribu kuwa Hud Hud utuletee habari  leo kama utakua Hud Hud utagundua miji ilivochafuka, si kwamba watu wanasujudia Jua tu, bali sasa wamezidisha zaidi wanaabudu mashetani, wanawaamini Waganga na Mizimu na mambo yote ya Shirk ndio yalokumbatiwa, Shetani kayapamba mambo yetu mpaka sasa hakuna hata anayeogopa Akhera mpaka asikie fulani kafariki ndio kidogo anashituka, Shetani ndio anapamba (Ma-Stage)yetu ya mambo machafu, hayo ndio tunayapa umuhimu, jitizame wewe unavotoka mbio ukisikia mduara au pana chakacha, jiangalie nafsi yako inakua vipi ukiambiwa kuna harusi nini inakua hali yako, au usikie kuna Mpira tena (Live)na ikisha rejea nafsi yako mtu akikupa taarifa kuna (Mawaidha)unamtizama usoni unamwambia nifunike kama yule (Kasuku). Nani katawala maisha yako Shetani au Mollah wako, siri hiyo utaijua mwenyewe kama unapoteza siku nzima kwenye TV au katika Darsa, kama kwenye Sala au Nyumba ya Muziki, utatambua mwenyewe dakika ngapi unamkumbuka Mollah wako na masaa mangapi unamkumbuka Mwalimu wako (Kasuku)kama vile nyimbo za Tarab, hayo ndio aloyaona Hud Hud, kwamba Shetani kakupambia mambo ya kidunia anakuzuilia kuujua Ulimwengu na Walimwengu, kakufunga pahala pamoja katika Tundu lako na wala hutaki kufunguliwa ukawa huru, ukaweza kuruka huku na kule, ukaona jipya na la zamani, Kurupuka usingizini ili upate kujifunza katika Ulimwengu huu mambo yapo mengi ya kujifunza na kusoma, na wala usidhani utayamaliza kwani kila siku utakua unasoma mambo mepya, labda ubakie kuwa mwanafunzi wa Kasuku ili ubakie kufunikwa Milele.
Namuomba Mollah atulinde na Ukasuku, tusije kudanganywa na Shetani, atupe uweza wa kugundua kama alivogundua Ndege Hud Hud. Amin

No comments:

Post a Comment