Sunday, April 28, 2013

SINA CHA KUFUNDISHA PART 1

Asalaam Aleiykum,

Ameniuliza Muulizaji mbona elimu yako chache ulonayo huifundishi kwa wanafunzi maalum, ikisha na wao wakaifundishe, muulizaji lazima alikua na kitu ndani ya maulizo yake, pengine kuna jambo limemgusa, au kuna kitu kinamtesa kuhusu usomeshaji wangu, kwa sababu angekua anataka kuwamo katika hao wanotaka kufundishwa asingeuliza kwa kubeza, inaonesha ana taaluma za vitabu alizokusanya kupitia vitabu mbali mbali, au kwa Mwalim huyu na yule, hajui hata tafauti ya kufundisha na kusomesha.
Nini Tafauti yake?
Kusomesha nikuchukua (Some information)ukampa mtu mwengine, huko ndio kusomesha, unachukua wanafunzi wasioelewa kitu fulani halafu unawahadithia inakua jinsi kadhaa wa kadhaa, unatoa kwenye kichwa chako unapeleka kwenye kichwa cha wengine. Nini kufundisha? Kufundisha ni (Understanding,Wisdom,Inteligence)ndio tena kinapatikana kitu kinachoitwa(Transformation)ya kujua kutokana na hayo mafundisho, Wapi yanatokea mafundisho(Kutoka kwa Mollah wako)(By Knowing itself through experience)hapo tena ndio inapatikana hiyo kujua.Mfano Gari inasomeshwa, lakini Baskeli inafundishwa, kuogelea Baharini unafundishwa, lakini kukoga tohara unasomeshwa. Vipi leo niweze kufundisha wakati mie mwenyewe sijamaliza kujifunza.
Alipojiwa Mtume s.a.w na Malaika Jibril a.s aliambiwa maneno haya mawili kusomeshwa na kufundishwa, ili tupate kuyajua kwa makini maneno hayo hebu na tuihudhurie aya 1-5 sura ya (Alaq)
"ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ"
"Soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba"
Neno la Mwanzo kaambiwa soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba, tizama vipi unaingia katika tafsiri ya maneno haya, namna gani utaishi ndani ya maneno haya matukufu, kwanini kaambiwa soma wakati Mwenye-enzi-Mungu anajua Mtume s.a.w hajui kusoma, vipi leo atasoma, kutokana na tamko hilo kimedumu kitabu hichi kitukufu mpaka hii leo, kimefasiriwa na wanazuoni mbali mbali ulimwenguni, na kinaendelea kusomwa kama kilivo anza kwa tamko la Soma kwa jina la Mollah wako aliyeumba, kwanini ikawa kwa jina la Mollah wako, kwa sababu vyote unavovijua kwenye ulimwengu huu na usivovijua kaviumba yeye, kwa hiyo kama utasoma basi ni kwa jina lake yeye asiyekua na mshirika, kila kitu chanzo chake ni yeye na marejeo yake ni kwake, hakuna kinachotokea (out of nothing). Lakini unapoambiwa soma moja kwa moja unaangukia kwenye(Intellectual)na huo si muradi wa kusudio lake hapo, unaweza kusoma ulichofundishwa, hiyo ndio maana ya hiyo(aya)lakini huwezi kufundishwa ulichosoma vitu viwili tafauti, Kufundishwa ni tukio linalotokea ndani yako(Experience)kama mwanamke hajawahi kuzaa vipi utamfundisha uchungu unakuaje, lakini alokwisha kuzaa anakua kashafundishwa uchungu ukoje anaujua kutokana na uzoefu, na huko kujua ndiko kufundishwa, vipi leo mimi nitaweza kufundisha.
Usije kukimbilia kwa Mwalimu sana analoweza atakupa masomo lakini hawezi kukufundisha, kusoma ni (Theory)ndio maana Bwana Mtume s.a.w akaambiwa "Mollah wako aliyeumba"
"خَلَقَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مِنۡ عَلَقٍ"
"Kamuumba mwanaadamu kwa pande la Damu"
Ukimtizama mwanaadamu huoni pande la Damu, hapo imetumika kusoma, lakini ukenda ndani na kuanza kumchambua utakuta kweli ni pande la damu, na huko ndio kufundishwa, umegundua kama ni damu, umepata kufahamu (through understanding).
"ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ "
"Soma(Kwa ajili ya)Mollah wako ni Mkarim"
Kakufanyia ihsani kubwa ya kuweza kukupa ufahamu wa kufundishwa, sasa ushayajua maisha, kakufanya Khalifa katika hii Ardhi, kakufundisha jema na baya ili uishi kwa salama, kakupa kila kinachohitajika katika maisha yako, anakuruzuku na kukuponesha maradhi unapoumwa, anakulea mpaka unakamilisha umri wako katika ulimwengu huu basi sasa yasome yote yalokuzunguka ili upate kuujua Ukarim wake.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment