Asalaam Aleiykum,
Sasa wacha niwaguse dada zangu na hii shughuli ya kioo na udanganyifu wake, hakuna kioo chochote utacho jitizama kikakwambia wewe mzuri, uzuri hautokei kwenye kioo, kioo ni chenye kukutengeneza tu, sifa zote za uzuri unategemea wanaadamu wenzio wakujulishe au wakusifu wengine wakutamani hapo ndipo unapata kufurahi Roho yako yakuwa kumbe mimi mzuri, kutokana na hali hiyo unahitaji visaidizi kwa sababu wale walo kutizama hawakuona uzuri, wao wenyewe hawaujui uzuri, nini wameona, wameona mapambo ya kuvutia kama vile (Lip-stick) kuchongwa kwa nyusi, vipini vya pua na mapambo mengine ndio maana mkaambiwa (Haram)kuonesha vivutio hivyo, sasa kwanini unafanya hivyo, unafanya hivyo kwa sababu hujaridhika, japokua aya ishakwambia hakuna makosa katika uumbaji wa Mollah wako lakini huridhiki, labda unaona hawataki nijipambe, na bila ya kujipamba siwi mzuri, wakati ukipishana na kiumbe huyo Sokoni na (Natural)yake alomuumbia Mollah wake utaona anameremeta kwa uzuri utokao kwa Mollah wake, kapendeza hana chochote katika sura yake lakini wacha itangazwe harusi ukakutane na mtu huyo huyo, unaweza kukimbia, pengine utamkuta baada ya kupendeza anatisha kwa (Foundation) na podari debe zima, anadhani uzuri unatokezea hapo, kumbe anajiharibu anauficha na kuharibu uzuri wake, na kama mtu atabisha haya ajaribu kwenda harusini (Simple)aweke vitu vyake lakini kwa njia ya (Moderation) na ataona tafauti ikoje na wenzie walopaka poda mwiko mzima na kufanya shughuli za kuuziba uzuri wao, kwanini ujibadilishe siku hii ya harusi wakati siku zote wewe mzuri.
Sasa Uzuri unatokea wapi kwa mwanaadamu?
utizame kwa makini uzuri unapotokea, fanya bidii upajue hapo,
Kwa hilo itabidi tuhudhurie Quraan sura ya Yussuf aya ya 22
"وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ ۥۤ ءَاتَيۡنَـٰهُ حُكۡمً۬ا وَعِلۡمً۬اۚ وَكَذَٲلِكَ نَجۡزِى ٱلۡمُحۡسِنِينَ "
"Na(Nabii Yusuf)alipo baleghe tulimpa Hikima na elimu, na kama hivi (ndivo)tunawalipa wanaotenda mema"
Hapa aya inatukumbusha kitu muhimu sana, inatuonesha tafauti ya vitu viwili hivi, (Inteligence)na(Education) Unaweza kumkuta mtu ana Degree au Phd lakini maskini kakosa (Inteligence)hekima, hata mazungumzo yake haya maana, kwanini ikawa hivyo kwa sababu yeye ana kipande cha karatasi cha kumjulisha kenda University lakini katika maisha yake anaishi kama mnyama, hana uzuri wowote wa maisha hajui chochote kizuri katika nafsi yake wala ya binaadamu wenzake hana hekima, lakini (Inteligence)hekima ni kitu chengine kabisa na utaona mfano wake kwa watoto maswali wanayouliza kutaka kujua maana ya kitu, watoto wanauliza kutumia (Inteligence) na sisi tunawajibu kutumia (Education) na kwa sababu hatutumii hekima katika majibu yetu, tuna haribu kabisa hekima ya watoto, sasa kwanini nikasema hayo, sababu kubwa watizame watoto utapata tabu sana kumuona mtoto mbaya(Ugly Baby)watoto wote wanazaliwa wazuri(Beautiful)na hekima zao(Hawana dhambi ni wasafi), sasa ngojea wewe wafike umri wa miaka kumi na nne uone sasa ufisadi gani unaingia kuharibu mwenendo, tabia na hekima zote zilizo nzuri, utamkuta mtoto wa kike keshafundishwa kupakwa chokaa, kesha tobolewa pua, tayari anajua kunyoa nyusi, inakua fujo tupu na yule wakiume naye keshaona mapambo hajiwezi tena wanakwenda waja hawa hata wakifikia miaka 30 uzuri wote ushapotea, nuru imezimika kabisa(ndio unasikia mtu anakuuliza unaweza kukisia mie miaka mingapi).
"Sasa tumrejee Nabii Yusuf a.s" Alipofika Baleghe alipewa vyote viwili Hekima na Elimu, hekima kuulinda uzuri wake, kujua mabaya na kujiepusha nayo, kujiweka katika hali ya Tohara(Pure)Nafsi yake isigubikwe na ufisadi wowote ule na hii ndio siri ya uzuri kaa makini uifahamu vizuri(Kama Nafsi itajiepusha na kila mabaya, itakua haina mambo ya kipuuzi imejitupa kwa Mollah wake)basi inatokea kwa hakika (Glowing:To shine brightly and steadily, especially
without a flame)Unangara nafsi yako ina meremeta(Pure Being)kila kiungo chako kizuri, watu wanakushangaa ndio maana katika Aya ya 31 ya sura hiyo hiyo ikasema,
"فَلَمَّا سَمِعَتۡ بِمَكۡرِهِنَّ أَرۡسَلَتۡ إِلَيۡہِنَّ وَأَعۡتَدَتۡ لَهُنَّ مُتَّكَـًٔ۬ا وَءَاتَتۡ كُلَّ وَٲحِدَةٍ۬ مِّنۡہُنَّ سِكِّينً۬ا وَقَالَتِ ٱخۡرُجۡ عَلَيۡہِنَّۖ فَلَمَّا رَأَيۡنَهُ ۥۤ أَكۡبَرۡنَهُ ۥ وَقَطَّعۡنَ أَيۡدِيَہُنَّ وَقُلۡنَ حَـٰشَ لِلَّهِ مَا هَـٰذَا بَشَرًا إِنۡ هَـٰذَآ إِلَّا مَلَكٌ۬ كَرِيمٌ۬ "
"Basi (yule mke)aliposikia msemo wao aliwaita(Waje kumuona Yusuf a.s kwa uzuri wake)na akawafanyia karamu na akampa kila mmoja katika wao kisu na akamwambia (Yusuf a.s)Tokeza mbele yao, basi walipomuona waliona ni kitu kikubwa kabisa na wakakata mikono yao(Kwa visu)na wakasema "hassha lillahi" huyu si mwanaadamu, hakuwa huyu ila ni Malaika Mtukufu"
Hapo utaona kimetokezea kitu kwa ghafla kinameremeta, nuru inawaka, hao wanawake hawamjui Malaika, lakini kwa kuwa kitu kilotokezea kimewashangaza wakadhani labda Malaika, hakujipamba Nabii Yusuf a.s, hakuvaa chochote chenye mvutio, katokeza na nafsi yake tu yenye kungara na wote walokuwepo wakajikata vidole(hata wewe jua likikupiga ghafla machoni wakati unaendesha gari si unapata ajali)huo ndio uzuri unatokezea katika roho yako, sio kwenye mwili wala kwenye mapambo, safisha roho yako, ifanyie tohara daima utakua mzuri mpaka kufa kwako.
"Na hiyo elimu aliyopewa Nabii Yusuf a.s" ndio hiyo ya kujua mambo ya ndoto nk.
"Sasa nini kuhusu wewe" Nafsi ishazimika kwa mambo yalojaa Rohoni (Switch)haionekani tena na wewe bado unataka kuonekana mzuri, hakuna la kufanya ili uwache kujipamba, zidisha Ibada, Muweke Mwenye-enzi-Mungu katika mawazo yako, mkumbuke kila mara, zoea kusoma Quraan sana, baada ya miezi mitatu utaanza kuona dalili za uzuri zinakurejea, taa inaanza kuwaka tena, sasa unaweza kwenda harusini bila ya kujipamba na watu wote wakaanza kukutizama wewe, kwanini ikawa hivyo, kwa sababu utaanza kutoa nuru fulani katika macho yako, na hapo inapotokea hiyo nuru ndipo unapokaa uzuri, na kama unataka kuyajua hayo mtizame yoyote unayedhani ni mzuri kwako wewe utaona mtazamo wako wote unaishia kwenye macho, na hayo macho ni dirisha la uzuri, namalizia kwa kusema uzuri unakaa ndani sio nje kama mnavodhani ndio maana wazungu wakasema(The Beauty is in the eyes of the Beholder)Nakuomba Mollah wangu utupe fahamu hii ya uzuri, tufahamu uzuri wa vitendo vyetu, uzuri wa Nafsi zetu, na mwisho Uzuri wa huu Uhai wetu ulo Tukirim katika hizi Roho zetu.
Amin.
No comments:
Post a Comment