Monday, April 1, 2013

MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA-PART-2

Asalaam Aleiykum,

Sasa ikiwa ushapata uhakika yakuwa Mwenyewe Alokuumba kasha kwambia atakutia katika Mtihani vipi leo unashindwa kuwa makini katika kujibu mtihani huo kwa ridhaa na maridhio ya kukubali, Mwanzo kabisa kwenye aya imetajwa nitakupa matatizo ya (Hofu) Nini hofu? Hofu ni lugha nyengine inayo tafsirika sambamba na Mauti, Ukiwa na hofu ikisha ukaidekeza hiyo hofu, ukaitilia mbolea na maji unakua unaishi kama vile Mfu(Zombie) Unakua huipati Sala, wala Mapenzi, hupati furaha vyote hivyo vinatoweka kwako sababu ya hiyo hofu, inatawaliwa Akili na hofu na kujazwa Maradhi mpaka ina haribika, nini maharibiko ya Akili, maharibiko ya Akili ni  kutoka kabisa katika njia ya maamrisho ya Mollah wako , ndipo hofu inakuchukua na inakupeleka sasa katika mambo haya,
Unahitaji Mali na umri  ndio unakatika, unaanza mapigano ya kuitafuta mali, unataka Nyumba hofu inakufanya utaipata lini, unahitaji mwanamke au mwanamme, ukiwashwa na Tumbo kidogo mbona limewasha, ukitizamwa kidogo tu kwanini kanitizama kakusudia nini kunitizama vile, itakuaje akijua, mbona kifua hakiponi, Shetani kasema nitadhurika, daktari kanipa mwezi mmoja tu wakuishi, watoto sijui wataishi vipi bila ya mimi, mbona hajatusalimia, kapandishwa cheo yeye nimeachwa mie, leo tutakula nini, fulani mbona jeuri na mengi mengineo kwa sasa utakua ushaanza kujijua kumbe loo na mimi ninayo Hofu. Ndio maana aya Mwanzo ikaanza na Hofu, na ukiichunguza kwa makini hiyo hofu yenyewe si kitu chenye Uhai kabisa, ni wewe mwenyewe ndie mwenye kukiunda ukakipa Uhai, ndio maana nikasema hofu ni ndugu wa Mauti. Na ukianza kuifufua nayo inafufuka na kuanza kuishi, na hapo unaanza kuonja upungufu wa kweli kweli katika nafsi yako.
Na Nafsi ikianza kuwa na upungufu ndipo maradhi yote yanazaliwa kwa sababu usharuhusu hofu iishi ndani ya mwili wako,Pia napenda ukumbuke Hofu ni chanzo cha yote yanofatia, Na maradhi yakiingia unaanza kupigana nayo na hapo ndipo zinaanza (Ngumi) za Njaa,(Neno la pili aya limeitaja njaa)Hapa linatajwa hilo litakalo tupeleka wengi Motoni, hichi chakula ndio fitna kubwa ya mwanaadamu, kwanini ikawa hivyo, Chakula ni Jumba la Roho, chakula ndicho kinacho kufanya uwepo Duniani kwa njia ya kuonekana, na kama utakikosa kwa muda wa miezi mitatu tu huna uhai(Utakufa)huwezi kuishi, hichi chakula ndicho chenye kusababisha Maafa yote, Mtu atadanganya, atakopa, ataiba, atadhulumu, atapokea Rushwa lazima tonge iende kinywani, na kila ukitenda matendo hayo yote elewa umefeli Mtihani na marejeo yako ni sehemu (Mbaya huko Akhera) Imekua jambo la hatari kubwa katika kuitatua dhiki ya njaa, sababu kila mmoja wetu anataka aokoke na balaa hili ili mauti yasimkute, na kama nani anopenda mauti yamkute, na hilo jambo la njaa ndilo linatupelekea kumsahau Mollah wetu kabisa, njaa ndio inayotufanya mtu hataki mambo ya dini, njaa inaturudisha katika kundi la wanyama kikamilifu japokua sisi tumepewa fahamu ya kuondoka katika hali hiyo. Tafauti yako na mnyama ni hivi, Mnyama anaruzukiwa hana fahamu, wakati wewe unaruzukiwa ukiwa na fahamu kamili, na umepewa ulimi wenye kuhisi au (Test) ya ladha zipatazo laki tatu, lakini mtizame Farasi au Ngombe ana ladha moja au mbili tu ya majani, hasikitiki , halalamiki karidhika wala hapati shida yoyote, hana haja ya kuweka akiba, lakini jitizame wewe ulopewa fahamu unakuaje, kwanza unataka chakula cha leo, ikisha cha kesho, halafu tena cha Akiba na kile cha ziada cha kuwatesea Binaadamu wenzio wasiokua nacho hicho cha kula. Lakini Mnyama akisha kula huyo anakwenda zake hashughuliki mpaka njaa imshike tena, kama ndege ndio anasowera angani anaimba akimsabahi Mollah wake na furaha tele ya Shukurani.
Jambo la tatu nalo ni hilo la upungufu wa Mali, hakuna yoyote mwenye kukubali kupungukiwa na Mali seuze ukawa huna kabisa, vita vinaanza hapo sasa, mbona natumia tu hazirudi, mbona siku hizi sipati faida, au umejenga jumba la Ghorofa unaona ukuta mmoja hautoshi zungusha na wapili, weka na walinzi tunaweza kudhurika, Mwenye-enzi-Mungu anakutia mtihani mali inapungua taratibu huku wewe moyoni unatetemeka na hapo tena ndio unaingia makosani kwa kumwita Mganga aje kusafisha nyota au aulizwe Jini mbona mambo simazuri kuna nini.
Enedelea Part 3

No comments:

Post a Comment