Monday, April 1, 2013

MAKOSA YA MJA MWENYE SHIDA-PART-4

Asalaam Aleiykum,

Unakuja kufungua macho kwa uwazi katika aya ya 156 sura ya Baqarah, "ٱلَّذِينَ إِذَآ أَصَـٰبَتۡهُم مُّصِيبَةٌ۬ قَالُوٓاْ إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّآ إِلَيۡهِ رَٲجِعُونَ "
"Ambao uwapatapo msiba husema hakika sisi ni(Waja) wa Mwenye-enzi-Mungu, na kwake yeye tutarejea"
Ikiwa huko mwanzoni umeshaambiwa hiyo yote ni mitihani, sasa hofu inakuondoka unakubali matokeo yote kumbe ni kazi ya Mwenye-Enzi-Mungu na wewe huwezi kushindana na Molla wako, ilobaki ufanye nini?, uridhike, na ukiridhika ndipo kikitokea kifo japo  una huzuni lakini unakua mwepesi wa kuridhika na kukubali kuwa  mwenyewe ndie aliyeleta na sasa kakichukua, ukiwa huna mali unajua Mollah ndie Mjuzi anajua sababu ya mimi kutokunipa mali, Ukifilisika pia unaelewa yeye ndie alonipa na sasa kachukua, Ukiwa na njaa, sasa unajua kwa subira yako kama anaweza kuniponesha na maradhi hashindwi kunipa njia ya kupata riziki ya chakula, ukishapata zawadi hii ya subira ukawa unajua kila kitu anapanga Mollah wangu, na mimi sasa sitaki kushindana na dunia hii, Nimeridhika nataka niishi kama njiwa vile hana wasiwasi basi unapata Ridhaa ya Mollah wako na  unaingia katika aya ya 157 ya sura hiyo hiyo inayosema,
" أُوْلَـٰٓٮِٕكَ عَلَيۡہِمۡ صَلَوَٲتٌ۬ مِّن رَّبِّهِمۡ وَرَحۡمَةٌ۬‌ۖ وَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡمُهۡتَدُونَ "
"Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mollah wao na Rehma, na ndio wenye kuongoka"
Ukishatimiza masharti ya Subira ukajifunga kweli kweli kuikabili mitihani alokupa Mollah wako na kufuzu, basi zinamiminika Baraka kutoka kwa Mollah wako(Blessing) watu wanakua wakisema aa usishindane naye yule kabarikiwa, na Rehma za kila aina zinakushukia unakua mwenye kufanikiwa katika mambo yako pasi hata kuomba, utaona mtu kakuletea zawadi bure, mara hichi mara kile, watu wanakutamania, na baraka za Mollah wako ni nyingi huwezi kuzipokea zote ukawa umezuia utaanza kuwapa na wenzio, utakua ukitoa kwa furaha, na ukipata hali kama hiyo wewe tena unakua umeshaongoka, umefuzu mtihani, umefanikiwa kutizama bila ya kutumia Macho(Ndio Maana ya Subira). Mollah wetu Tujaalie tupate hekima hii ya subira iwe kila mtihani wako ukija tunauona mpaka unaondoka, tujaalie kheri ndani ya mtihani huo tusikusahau daima, tupe moyo wa subira tudumu katika kuhifadhi yale ya kheri uliyotuamrisha ili tupate Baraka na Rehma zako kama ulivo ahidi. Amin.


No comments:

Post a Comment