Asalaam Aleiykum,
Leo hapa nataka uonje na mimi japo kidogo chakula cha elimu ya Uzuri, ndani ya chakula hichi upate kujua ladha na maana ya neno hili la uzuri,(Mpaka leo wanahangaika wanasayansi)kujua nini uzuri lakini wameshindwa kuitambua siri hii, na usidhani na sisi ndio tumeigundua laa, tunajaribu kupata chakula hichi cha miujiza ili kwa uchache kitukate njaa yetu yakujua nini uzuri. Sasa utajiuliza kwanini nimeliunganisha neno la uzuri na chakula, sababu kubwa ya kutumia neno hili ni kwa kuwa na wewe unalitumia kila mara katika hicho chakula, unalitumia katika kuwahukumu wanaadamu nani mzuri na nani mbaya, lakini cha ajabu hujui maana yake na wapi huo uzuri unatokea, na kwanini ukatokea, na inakuaje unapotokea, na ikiwa unajua basi wewe ni katika wachache walopewa bahati hiyo ya kuelewa, lakini kwa wale wasojua basi hii ndio Darsa yao ya kupata faida mbili tatu ya siri ya uzuri.
NINI UZURI?
Uzuri una desturi ya kuficha tafsiri yake kama ilivyo Afya na Furaha, ukiulizwa nini Afya unakua huna jawabu, lakini waweza kujibu nini Maradhi ukayaeleza haya ya Sukari, haya ya Figo, haya ya tumbo nk. Na furaha vilevile unaweza kutaja sababu ya Furaha lakini ukashindwa kueleza furaha yenyewe ni nini, na Uzuri hali kadhalika huwezi kuuchambua ila unajua tu hichi kizuri, huyu mzuri , kwa uchache vyote hivyo ni vitendo vya kuhisi(Experience) lazima uishi ndani yake ndio ujue sasa umo katika hali hiyo. Anaweza kusema Mtu kwanini asitaje kuona, Naam kuona unaona kila siku lakini jee unaona mazuri, ndio nikakwambia darsa hii nataka nikufahamishe vipi utizame vizuri au (Uzuri)wa kila kitu ili upate faida.
Tumepewa Fadhila kubwa na Mollah wetu katika neema hii ya (Kuona) nini kinatokea katika kuona(Elewa nazungumza haya kupitia elimu ya dini na sio ya sayansi)Nini kinatokea mpaka tunaona, Unapotizama kitu kwa kutumia macho unakua unatoa (Energy) au nguvu fulani kwenda nje kwenye hicho kitu, na hicho kitu kinatoa (Energy)inayokuja kwako kwenda ndani ya akili na kufanyiwa uchambuzi ili kipatikane kujulikana ni kitu gani, na kikisha julikana inapatikana hiyo yenye kuitwa (Knowledge) au (Known) kwa ufupi. Kwa maana hiyo kila kitu katika Ulimwengu huu ni (Matter) na hiyo (Matter) ni (Energy) na hiyo (Energy)tuwaachie wana (Physics)watatuchambulia zaidi.
Leo katika Darsa hii nitagusa (Lip-stick) Rangi ya mdomo, (Eye-Shadow) nitapita katika utowaji wa nyusi na mengineyo lakini kabla ya kwenda huko wacha nikutembezeni kwenye hii Bustani ya (Known)kujua ili mchume matunda ya fahamu ili mkitoka katika bustani hii na nyie muwe katika kundi la wenye kuelewa. Ndani ya bustani hii tunakutana na kitabu cha wageni, kitabu kikarim Quraan sura ya Mulk aya ya tatu mpaka ya tano. Endelea part 2
No comments:
Post a Comment