Asalaam Aleiykum,
Unamjua anayepata hasara bila ya kujijua? yule Mwenye kujiita Muumin halafu unapokaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan anaukaribisha kwa (Party na Picnic). Huyo anafanya Sherehe za kumuaga Rafiki yake (Shetani)na kumpa ahadi nisubiri Yaumu shaka tutakutana tena bila ya wasiwasi, Huku Mwenye enzi Mungu anawaita waja wake kwa Mapenzi akisema "Ewe kiumbe wangu wee" njoo ukiwa msafi, anza kujisafisha, njoo ukiwa (Tohara) ili uzifanye hizi siku chache ziwe za utiifu kwa ajili yangu, uje ufanye mambo ya (Taqwa), Wewe Unamjibu ngoja nijichafue zaidi, nipe muda nitie Najis katika Kiwiliwili changu, Niwache nije kwako huku nina kumbukumbu za Rafiki yangu Shetani, mimi katika huo mwezi wako Nakuja Shingo upande, ndio imenibidi tu sababu watu wote wananijua mimi Muislam, lakini kwa uhakika mapenzi yangu yote yapo kwa Shetani na hiyo miezi kumi na mmoja ilobaki, Najua Mollah wangu wewe umenipa Uhai, ikisha Wewe ndio Unanipa Riziki na kila kitu ninacho hitaji lakini mie niache sijiwezi kwa shughuli za (Vunja Jungu).
Enyi "Wanaadamu" hususan nyinyi Waumin hamjikumbushi wakati mtakapo ulizwa kwani hamkusoma Quraan sura ya Yaasin aya ya 60,
"أَلَمۡ أَعۡهَدۡ إِلَيۡكُمۡ يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعۡبُدُواْ ٱلشَّيۡطَـٰنَۖ إِنَّهُ ۥ لَكُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬"
Jee sikukuagizeni Enyi Wanaadamu kuwa msimuabudu Shetani, Hakika yeye ni adui aliye dhahiri(Wazi)kwenu.
Na mmekua hamtaki kusikia ila lazima mvunje Jungu, lazima msondo upigwe, tena kuna watu ikikolea wanasema bila ya kulewa ntaichezaje, (Maskini)hawa hawajalewa wako hali hiyo, nini taarifa zetu tunazopokea yanofanyika katika hilo Vunja Jungu. Hakuna hadith za huko isipokua Maasi, halafu huku unasema unajiandaa kufanya (Taqwa) lakini kwa kupitia njia ya Maasi, Iwapi Ramadhan yako wewe mvunja Jungu, Hana Ramadhan yoyote yule mwenye kufanya maasi katika hili kumi la mwisho la Shaaban(sababu zake utakutana nazo huko mbele). Mfano wa kwanza kabisa kitizame chakula kinavofanya kazi kwenye (System)ya (Tumbo)lako kwanza kinakaa siku nzima kwenye (Utumbo) halafu kinachujwa na (Parcent)kubwa inakwenda kwenye Akili, na bado hujui kwenye Akili kinakaa muda gani, Sasa jiulize Pombe nayo inakaa muda gani, pia kumbuka kuna muda wa vitu kukaa katika hiyo (Body System)yako, kuna vya siku saba na vyengine kumi na nne, na vyengine mpaka siku arobaini havitoki katika kiwiliwili chako, vipi leo Mvunja Jungu useme unaipata Ramadhan.
Huna Ramadhan kwa kunywa Pombe kesho Ramadhan, Huna Ramadhan kwa kunuwiya kula haramu kwa kuwapandishia Waumin bei za Chakula, huna Ramadhan kwa kucheza viuno kwenye Taraab au kutembea Uchi nk, vipi wewe utaipata Ramadhan. Endelea Part 2
Sunday, June 30, 2013
HASARA YA VUNJA JUNGU PART 2
Asalaam Aleiykum,
Vipi leo wewe uingie kwenye funga ya Ramadhan na kapu la mijidhanmbi, kama nani anokwenda kwa Mpenzi wake ananuka, vipi leo wewe unakwenda kwenye Mwezi Mtukufu umebeba bango Mimi Nishazini, Mimi Nishalewa, Mimi nishadhulumu na sasa nakuja kwako Mollah wangu unisamehe.
Nini Ramadhan? Ramadhan ni Rehma, Ramadhan ni Maghfira(Kusamehewa)Ramadhan ni kuchukuliwa dhamana ya kuepushwa na (Moto) na kuingizwa Peponi, Leo zitizame hasara Mja unazokuja nazo kwenye hiyo (Rehma) ya Mollah wako, kwa ajili ya hilo vunja jungu lako, Kusudio la Rehma hapo mwanzo ni kusafishwa hicho (Kiwiliwili)chako na hiyo (Roho)yako ili viwili hivyo viwe safi, tazama sasa vipi unaanza funga yako ya Ramadhan, jungu ndio ushalivunja kwanza kwa kufanya zinaa, zitizame nini hasara za vunja jungu kwa tendo hilo la zinaa, na inakuaje unaikosa hiyo Ramadhan.
Jambo la mwanzo ukihudhuria kwenye kadhia ya (Uzinifu)inapatikana kutamani, Na ukitamani kuna (Energy)ndani ya Mwili wako inaanza kupanda juu (wewe jichunguze) tena kwa kasi inakwenda kugusa sehemu ya matamanio, na sehemu hiyo ikiguswa kila kitu kinachafuka inachukua (Muda Energy) hii kutulia tena, wataalamu wengine wanasema inachukua mpaka siku(40) ndio ipoe. Sababu kubwa umetamani kitu si chako, na kuna tafauti kabisa pale unapotamani cha halali yako, na mfano wa hayo usijitizame wewe mwenyewe hebu mtizame mwizi anakua na hali gani anapotaka kuiba uone (Energy) yake inavopanda kwa kasi, hujamkuta hata siku moja mwizi asoweza kukimbia, lazima huyo awe ka (Retired) na hivi ndio hali anokua nayo anotaka kutenda tendo la zinaa, Na sehemu hii ya kitivo cha matamanio ikiguswa basi (Roho na Akili) vyote vinaingia tafrani na sababu kubwa viwili hivyo vyote ni majirani, na mambo yakichafuka mwili nao unafatia, na hilo lilikua ni mataarisho tu ya (Vunja Jungu).
Ikisha hizoo Roho mbili kwa maridhiano zimeamua kumuasi Mollah wao, Wameamua kutenda dhanmbi kubwa, wanapomaliza wawili hawa tendo hili la Uzinifu (Energy) hiyoo inashuka chini na kuleta uharibifu wa Kimwili, hapo tena mtu anaanza kuchukia lile tendo, mara anaumwa hichi na kile, huyu anajuta, anaona haya mwezi ushaandama, Hapo tena inakatika Rehma ya Mja huyo anaingia katika misukosuko mwezi mzima wa Ramadhan, anapita kununua madafu mchana anakula usiku(Kutongoza), huna funga, sababu (Energy) yote inotakiwa kwenye (Saum) inapanda na kushuka kama kipimo cha (Homa), vipi wewe utafunga huku mawazo yote yapo katika mawazo machafu, unakumbuka vituko vya vunja jungu, mwenye unajijua huna funga lakini unaendelea kujitesa na Njaa.
Endelea.Part 3

HASARA YA VUNJA JUNGU PART 3
Asalaam Aleiykum,
Ikiwa hiyo ndio hali anayobakia nayo mzinifu, nini hali za wenye kunywa ulevi, wale wenye kuvuta bangi na mirungi siku ya vunja jungu, na wao hali kadhalika wanabakiwa na mabaki ya pombe na mirungi kwenye (Body) Miili yao, na hakuna anayepata Rehma ya (Saum-Funga) kabisa. Na hata kama wakifunga basi ni bure ni sawa kujitesa na njaa, na kama ukibisha hayo hebu Muulizeni mgonjwa wa sukari eti kweli (Doctor) wanajua kiwango cha sukari ulokula miezi mitatu ilopita, akipimwa damu taarifa zote zimo anaambiwa ulikua ukiipiga vijiko vingapi kwa siku, ikiwa bado unapinga kaulize vipi anayekufa kwa ulevi akipimwa baada ya mwezi mzima wanakwambia aliuchapa chupa ngapi, na wanasayansi hawakuishia hapo sasa wamevumbua (Chemical)fulani wakikutia kwenye ngozi wanakwambia (Gomba au Bangi) umevuta wiki ya jana au umekula wiki mbili zilizopita, (Puri)ulovuta bado inaonesha kwenye damu na hivyo ndio Mwenye enzi Mungu anavodhihirisha mambo yake mpate kujua kila mnalotenda linabakia (Rekodi) zake kwenye (Mwili) wako, sasa jiulize kwa hali hii ya Kuvunja Jungu kila ufisadi unabakia jee Funga ninayo?
Na wale wenye kuvunja jungu kwa (Party au Taarab) wao ndio wanapigwa picha kabisa na ushahidi upo na kama watabisha basi wataambiwa subirini, "Yaasin 65"
"ٱلۡيَوۡمَ نَخۡتِمُ عَلَىٰٓ أَفۡوَٲهِهِمۡ وَتُكَلِّمُنَآ أَيۡدِيہِمۡ وَتَشۡہَدُ أَرۡجُلُهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ "
siku hiyo tutaifunga midomo yao, na itazungumza (na sisi)mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokua wakiyachuma.
Mimi wakati navunja jungu nilikua nainua mikono juu natamba kukuasi Mollah wangu, Na miguu nayo itashuhudia kweli mimi nilikua nanyanyua visigino halafu nakatika viuno ili nipate kuwachafua waja wako Akili zao, ili wapate kukuasi wewe Mollah wangu, Huingia viumbe hawa katika Mwezi wako Mtukufu hawana (Taqwa) wala si wasafi mwezi mzima mawazo yao yamo kwenye hadith za vunja jungu.
Hizo ndio hasara za vunja jungu, ikisha siku ya Qiyama mkiamrishwa kwenda Motoni mtaanza kushangaa pembezoni mwa Shimo la (Jahannam) mnasema mbona tulikua tukifunga, wataamrishwa Malaika wasukumeni, watakukamateni visogoni kabla ya kukusukumeni watakuulizeni maneno haya"Sura ya Mulk aya ya 8 na 9.
"تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلۡغَيۡظِۖ كُلَّمَآ أُلۡقِىَ فِيہَا فَوۡجٌ۬ سَأَلَهُمۡ خَزَنَتُہَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَذِيرٌ۬"
Unakaribia kupasuka kwa hasira, kila mara litakapotupwa(Shimoni)humo kundi(La wabaya)walinzi wake (Malaika)watawauliza jee hakukufikieni(Nyinyi) muonyaji.
"قَالُواْ بَلَىٰ قَدۡ جَآءَنَا نَذِيرٌ۬ فَكَذَّبۡنَا وَقُلۡنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَىۡءٍ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ۬ كَبِيرٍ۬ "
Watasema kwanini, alitujia Muonyaji, lakini tulikadhibisha na tulisema, Mwenye enzi Mungu hakuteremsha chochote, nyinyi mko katika upotofu mkubwa.
Tulifikia hata kusoma hasara za Vunja jungu, lakini tulikua tunajipa tamaa hakuna chochote, tunatishana tu mambo ya kutiana woga, lakini kwa wale walozinduka basi usilivunje jungu, bali wewe lijenge ulitie saruji liwe madhubuti kwa kusoma Quraan kwa wingi, kwa kuzidisha sala za sunna na kumsabahi na kumkumbuka Mollah wako kuanzia sasa na nakupa muongoz ukifanya hivyo Ramadhan yako safari hii itakua ya namna nyengine kabisa.
Namuomba Mollah wetu atuepushe na Maasi, atupe (Taqwa) na mapenzi yake, atupe afya tuweze kusimamisha nguzo hii na nyengine kwa ajili yake. Amin

Sunday, June 23, 2013
AJABU YA KUSAMEHE PART 1
Asalaam Aleiykum,
Nini Samahani? Kwa Maagizo kutoka kwa Mollah wetu, Msamaha ni Rehma au (Zawadi)maalumu alowapangia waja wake kwa kusema katika Quraan sura ya Zumar aya ya 53.
" قُلۡ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسۡرَفُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ لَا تَقۡنَطُواْ مِن رَّحۡمَةِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًاۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ "
"Sema"Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu, msikate tamaa na Rehma ya Mwenye enzi Mungu, Hakika Mwenye enzi Mungu husamehe dhanbi zote, Hakika yeye ni Mwingi wa Kusamehe (na)Mwingi wa Kurehemu"
Kwa fahamu zetu za Kibinaadamu huwezi kujibu swali la hapo juu mpaka mwanzo ufanye utafiti na upate kujua nini (Kosa)? Kosa ni kitu chochote kinachotendeka baina ya pande mbili,(chengine chochote unachojifanyia mwenyewe kinaitwa Dhuluma)Na nikisema baina ya pande mbili nina maana iwe wewe na Mollah wako au Binaadamu mwenzako. Kwa kuwa leo tunazungumza kusamehe wacha hili neno kosa tuligeuze na kuliita (Dhanbi) dhanbi ni kitendo unachomtendea Mollah wako au Binaadamu mwenzio, kitendo hichi chaweza kuwa kikubwa au kiwe kidogo, kifanyike mchana au usiku, kiwe cha kufurahisha au kukera, kije kwa ubaya au uzuri, madamu ni kosa kitendo hicho hakifutiki au kumalizika mpaka kipate mizani ya Malipo yake, Na hapo ndipo yanapatikana yale maneno ya (Kama ulivokopesha ndivo utakavolipa)Na malipo yapo ya aina mbili, ima Kwa Mwenye enzi Mungu au kwa Binaadamu mwenzako, Kwa Mollah wako utapata msamaha wa aina mbili ama kwa kufidia na jengine utapata hiyo Rehma ya kusamehewa hayo uliyoyatenda.
Lakini kwa Mwanaadamu mwenzako inatakiwa ipatikane hiyo inayoitwa Samahani(Kusamehewa), lazima akusamehe, ndio tunarejea hapo mwanzoni nini Samahani? Samahani ni kitu chenye uzito wa pekee kwa mwenye kuomba na kuombwa. Katika nafsi ya Mwanaadamu iliyomiliki jambo hilo ni mfano wa Mdai na Mdaiwa, ni kama biashara ambayo mwenye kusamehe ndio anafaidika zaidi, ndio Maana ukathibitishiwa katika (Hadith Sharif)unaambiwa"Rehemu upate kurehemiwa(Sababu Kusamehe ni kitendo cha Rehema)""Samehe upate kusamehewa""Wasamehe walio Ardhini, Apate kukusamehe Aliye mbinguni na Ardhini" Na pia Elewa hakuna Waislam wawili wanokutana wakapeana mikono na kusalimiana ila wakiachana basi Mollah huwa ni Mwenye kuwasamehe (Dhanbi)zao. Enyi Ndugu zangu ajabu ya kusamehe na Rehma zake iko hivyo wanokutana tu wakapeana mikono kwa ajili ya kusalimiana ikisha wakakumbatiana basi hupukutika (Dhanbi)zao kama majani makavu yanavopukutika kutoka katika mti ukipigwa na upepo. Nini Habari yako wewe kama utavaa koti la kusamehe, kutaka kuijua Ajabu hii enedelea Part 2

AJABU YA KUSAMEHE PART 2
Asalaam Aleiykum,
Samehe upate kurehemiwa, Nini Kurehemewa?
Unaijua nini Rehema, Rehma ni bahari kubwa ambayo hatuwezi kuikoga kwa uchambuzi, ila nitakupa mifano midogo ya Rehma ile nipate kukuzindua, hiyo Rehma ni huko kuvuta pumzi kwako, kulala kwako, kuzungumza kwako, Afya yako ulonayo, zote hizo ni sehemu katika bahari ya Rehma, hiyo ndio Rahman yenye sifa ya kuonekana na kufichikana, Na kwanini isiwe hivyo wakati mkisalimiana kwa furaha (Dhanbi)zenu zinapukutika kwa (Msamaha). Nini habari yako wewe Ukiamua kusamehe, Ukisamehe unakua ushavaa vazi la (Huruma) na ukivaa vazi la huruma unakua ushajiweka tayari na wewe (Kurehemewa)na Mollah wako, Na Mwenye enzi Mungu akikuona kama kweli umesamehe kwenye Nafsi yako basi hukuteremshia Rehma kwenye Maisha yako, kama una Maradhi bado yamo ndani hayajatokeza basi anakuponesha pasi mwenyewe kujua, kama una donge kifuani ukisamehe linaondoka, kama una dhiki unaipata Faraja, kuna wengine wanapewa Utajiri kwa ajili ya kusamehe tu, hizo ndizo Rehma za Mollah wako kwa Mja mwenye kusamehe.
Pia napenda Ufahamu Kusamehe ni Afya, na Kisasi ni Maradhi, kisasi ni jambo la kudumu, na kama hujakilipa kinakusugua sana katika Maisha yako, ndio maana ikaambiwa katika sura ya Maidah aya ya 45 inapoanzia na kumalizikia kwa maelezo yake kuna kitu Adhimu nacho ni maneno haya" فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ ڪَفَّارَةٌ۬ لَّهُ"
"Lakini Mwenye kusamehe basi itakua kafara kwake".
Kwanini iwe kafara, sababu ujifungue na kisasi, sababu kutokusamehe ni hali ya kukumbuka, na wewe kumbukumbu yako (Memory)yako ni ndogo sana, na ili uishi kwa furaha(Rehma) imejengeka kwa hali ya ushaulivu, ndio maana ukapewa uwezo finyu wa kukumbuka, jiangalie wewe mambo mangapi unaweza kuyakumbuka kwa siku, mengi yanatokezea lakini hukumbuki hata moja, na ikipita siku ulotenda jana yote ushasahau hiyo ndio kawaida yako, sasa ukikaa na jambo au kisasi au kutosamehe inabidi uitumie sehemu ya kumbukumbu yako kwa ajili ya kuifuga hali hiyo, na kama jambo la kukuumiza ndio linaendelea kukudhuru, na kama umedhulumiwa sasa unaendelea kujidhulumu, basi kwanini uteseke na uwezo wa kutoa kafara unao, tena sio bure na wewe utalipwa kwa kafara hiyo, nayo ni hiyo Rehma.
Vipi Utasamehe?
Kusamehe ni ushujaa, ni jambo lisilotendwa na wanaadamu wengi na wewe ukipata nguvu za kuweza kusamehe basi umepata kitu kikubwa sana, usije ukakiachia utakua hasarani, na kusamehe kunatakiwa ukumbuke kitu kimoja tu nacho ni hiyo (Rehma).
Kumbuka alo kukera au kukudhulumu hata yule alo kujeruhi, huyo amekuletea Biashara ya Rehma, Lakini wapi, wewe umezoea Biashara ya (Nipe nikupe)umetoa gari upewe pesa, umetowa nyumba upewe pesa, vipi leo upigwe kibao ukubaliane na habari ya useme ahsante, wewe ukipigwa kibao basi kama kuna Jabali utamtandika yule alokupiga kibao, unataka aumie kushinda kile kibao alichokupiga, Unajua kwanini ikawa hivyo, Sababu Shetani wakati ule ghafla anakusahaulisha Rehma na kukumbusha Heshima, ndio kanikumuta kibao mbele za watu, watu watasemaje, hiyo ya kwanza kwenye akili, halafu yanafatia machungu kwenye shavu, sasa yatizame malipo yako yanakuaje, hapo ndipo unaweza kumuua mbu kwa kutumia Rungu sio kofi tena. Sasa endelea kuitizama Ajabu ya kusamehe na Rehma zake. Part 3

AJABU YA KUSAMEHE PART 3
Asalaam Aleiykum,
Wacha sasa tuchungulie katika Rehma hii ya kusamehe ili tupate kujua tunakutana na nini, Kwanza wacha tujikumbushe au kumbuka wewe ulivokua mdogo umetenda kosa na mzee wako kakasirika, hamaki zimemshika, mkanda ushavuliwa au fimbo iko mkononi kwa ajili yako, kumbuka hali ile ulokua nayo, kama wewe (baba)au(Mtoto)sasa rejea ghafla hamaki zimepotea ukaamua kuzungumza na mwanao badala ya kumpiga ukamsamehe,(wewe mtoto)vipi hali mbili hizi zinakua kwako wewe, ile ya kwanza hofu na maradhi matupu(unakua mgonjwa leo ataniua huyu)na ya pili inakua nini ukisamehewa, Afya na Furaha(Rehma)tupu.
Sasa ikiwa hiyo hali anayokua nayo mwenye kusamehewa, Nini habari yetu sisi kwa yule mwenye kusamehe, Tizama wewe ukikosewa kosa kubwa, ikisha akaja mkosaji akakuomba kwa mayoe na vilio umsamehe, na wewe ukamridhia moyoni na kweli ukamsamehe, nini kinatokezea, jambo la mwanzo kutokezea inakuhudhuria Sahau(Kusahau)na sahau ikikuvaa Rehma inawasili, na Rehma ndio hiyo Afya, ndio furaha, ndio maana ukizama kwenye mchezo wa (senema)hukumbuki chochote, lakini hebu jitizame ukenda msibani kutoa pole unakuaje, maneno ya kumbukumbu matupu yanakutoka, jana tumeongea, mbona aliniaga, alinipigia simu, alikua hata haumwi,ilikua nini kafa ghafla, sababu hutaki kukubali kuwa kesha kufa kwa wakati ule ndio maana umeshikilia jana hivi, jana vile, Unaishi ndani ya (Memory)na hali kama hiyo ndio unayoishi nayo kama utakua si mja mwenye kusamehe.
Ama mwenye kusamehe yeye anapata ishara zote za kuelekea kwenye Ucha Mungu, kwani kusamehe ni Upole, kusamehe ni Imani, na huko kusamehe ni Huruma, basi sifa hizo zote hazikutoshi wewe kukoga kwenye mvua ya Rehma ya Mollah wako, Jitahidi kujizoesha kusamehe, kama (Mke au Mume)kakusoea mara kumi, wewe mshamehe mara kumi na moja, Muunguze kwa moyo wa samahani mpaka awe kama wewe anaishi kwenye (Kasri lako la Msamaha)tena mwambie humu ndani natanguliza samahani kabla hujanikosea, Ikiwa umegombana na Ndugu zako basi anza leo zoezi hili la kusamehe kwanza kwenye moyo wako, na wao kwa Rehma za Mollah wako wataanza kukusamehe kwenye Nyoyo zao, Kama umekoseana au Wazee wako mekorofishana na mpaka leo hamzungumzi, fanya hima wasamehe na watumie Rehma za msamaha ziwafikie kwa walilolifanya, ikisha toka kawaombe wewe Msamaha uone vipi Rehma ifanyavo kazi yake, mpige (Shetani)kwa fimbo ya Rehma, uone miujiza yake.
Ikiwa Marafiki zako wamekukosea kumbuka ufunguo wa furaha unao mwenyewe, kama utachagua kuwasamehe hiyo ni Furaha yako(Rehma)au kama utaamua kubaki na dhiki ya Moyo hutaki kusamehe hilo pia ni chaguo lako, hakuna awezaye kukufanya ufurahi isipokua wewe mwenyewe. Ipate ajabu ya kusamehe kwanza kwa kusamehe wewe, na pia napenda uelewe makosa mengi ya Wanaadamu yanatendwa na Ulimi, kwa hiyo usikubali wewe kutiwa katika (Gereza)la Ulimi, ikawa huzungumzi na mwenzio sababu kasema,(Kumbuka:Ulimi umeumbwa na mate:kuteleza kazi yake)usikubali kukaa mahabusu mwaka mzima kisa sauti iloambatana na upepo imevuma kinyume na matakwa yako, maneno yasikutie maradhi ya kinyongo, kumbuka hayana uzito na yanaishi kwenye Akili kwa muda mchache tu, anobaki kusumbuka ni wewe, lisikunyime Raha kosa ukawa unaishi na maradhi, jitoe jela kwa kufanya jambo moja tu, nalo hili la kusamehe, Samehe upate kusamehewa, Samehe upate kurehemewa, Samehe upate kuingia kwenye Furaha, na hiyo ndio Ajabu ya kusamehe:Mollah wetu tujaalie zawadi hii ya uwezo wa kusamehe, tupe faraja za kusamehe wenzetu kama wewe unavo tusamehe sisi yote tunayo kukosea.Amin

Sunday, June 16, 2013
MAISHA YA INSHAA ALLAH PART 1
Asalaam Aleiykum,
Imeshakufikia ndani ya Moyo wako habari unayoikataa na kuipinga siku zote ya Maisha ya Inshaa Allah, Jee unajua Maisha haya yakoje? Wewe Mwenyewe umeshawahi kuyaishi maisha haya? Na vilevile unataka kuwajua kina Nani wanoishi maisha hayo hivi sasa?, Hayo ndio maswali tutayojiuliza katika Darsa yetu ya leo ili tuupate ufunguo wa kuingia katika hii Nyumba ya (Maisha ya Inshaa Allah).
Kwanza kabisa tujiulize nini maana ya Inshaa Allah, kwa Tafsiri nyepesi(Mwenye enzi Mungu akitaka), Kwa Lugha ya Tawhid itakua vigumu kwa sisi kufahamu kusudio lake mpaka uwe umeshiba Tawhid ya Mollah wako, umeshafunguliwa katika Ubongo maarifa ya (Mystic)na kuona mambo kwa upeo mwengine ambao umefichika kwa watu wakawaida, Na kwanini twende kwenye ugumu wakati wepesi upo, basi tuanzie hapa katika kiwanja cha wepesi na kujiuliza nini Inshaa Allah?
Inshaa Allah ni (Trust)kwa ufupi, au kwa mzunguko mwengine wa kilugha ni Imani, lakini Imani yenyewe ni tafauti na ile ya kutamka Ulimini, Imani hii ni ya kujikabidhi kikamilifu kwa Mollah wako, ikawa huna pingamizi kwa chochote kile kinachotokea katika Ulimwengu huu.
Leo nakupa kioo ujitizame uzuri hiyo sifa unayojipa ya Ucha Mungu, uingalie vizuri kama kweli ipo japo chembe katika moyo wako, Sababu nimesema hivyo sio kukuvunja Moyo ila nia yangu nataka nikufungulie muono zaidi ili upate kuwasili katika huo Ucha Mungu, Na hakuna njia nyepesi ya kuwasili kwenye Ucha Mungu kama hii ya kuishi Maisha ya Inshaa Allah, Lakini maisha yenyewe ni vigumu sana kuyapata, na wanoishi maisha haya ni wachache sana na ni watu pekee wenye furaha katika Ulimwengu huu.
Kwanini wakawa hivyo? Sababu kubwa Wameamini na kukabidhi kwa Ujumla Maisha yao kwa Mollah wao Muumba, Na ukipokelewa na aliyekuumba, unakua umerudi Nyumbani na anaye rudi Nyumbani huwa hana matatizo katika Ulimwengu huu. Sasa na wewe unahamu ujulishwe njia za kuweza kuishi hayo maisha, nini unatakiwa ufanye, na wapi uanzie.
Kuishi Maisha hayo ya Inshaa Allah ni kuitegemea ile nguzo ya sita yenye kuzishika zote, na ukiijenga nguzo hii ikawa madhubuti basi una uhakika Nyumba yako haitoanguka hata kama utatokea mtetemeko wa Imani, Hakuna pakupata maisha hayo isipokua kujitupa na kujifunga katika nguzo hii ya (Qadir)kadar, Kuamini ya kwamba mimi nimo katika hili(Spaceship)Dunia, Mimi nazunguka nayo (Ardhi)hii hata nikifanikiwa kuchupa nikimbie, basi nitaangukia katika Mbingu zako ya Subhanna, Basi kwa kuyajua hayo sasa najijua na mimi vilevile umeniumba kutokana na Ardhi hii, na kuna siku utanirejesha tena ndani ya Ardhi hii, na pale utaporidhia wewe Mollah wangu mimi ninayo tamaa na uhakika utanirejesha tena katika Ulimwengu huu kwa ajili ya kunihukumu.
Sasa ikiwa nina yakini na hayo, nini habari yangu mimi, na kwanini siwezi au sitaki kuishi maisha haya ya Inshaa Allah, Mbona nimekua Jeuri nanyanyasa wenzangu, Mbona kiburi kimenizidi, nini hasa kinacho nifanya niteseke, nikiwa Maskini nateseka, nikiwa Tajiri nateseka nini tatizo langu. Kutaka kujua Tatizo lako ENDELEA PART 2

MAISHA YA INSHAA ALLAH PART 2
Asalaam Aleiykum,
Unateseka kwa sababu huna (Trust) Imani ima dhaifu au haipo kabisa, mambo yako yote yanaanzia kwenye (Ulimi) na kuishia hapo hapo Ulimini, Hutaki kuamini kwamba Maisha ni (Inshaa Allah) Unaona siku zote mambo yanavobadilika leo unakua Tajiri kesho unafilisika, leo mzima kesho una maradhi, Jana ulikua hai kesho unaitwa Marehemu(Maisha hayana Gurantee)Na hiyo ndio Inshaa Allah yenyewe. Anoishi Maisha haya hategemei uhakika wa Akiba wala kupata cha zaidi, kila saa na dakika yeye ni mwenye kumtegemea Mollah wake, Anaishi kama maisha ya Ndege, kama maisha ya Mnyama porini, au kama samaki Baharini, hebu watizame vipi wanyama maisha yao yakoje, ukiyagundua maisha ya wanyama vipi wanaishi kwa Inshaa Allah pengine yatakufungua (akili)huenda ukapata hekima ukatambua kumbe mimi kama samaki au ndege, Na sote tumeumbwa katika Ulimwengu huu tunapita njia, sasa kwanini mimi nahangaika na samaki haangaiki na sote tunakula, sote tunalala, nini kimenifika mimi, ikikujia fikra kama hiyo basi utaona unaanza kupiga hodi katika Mlango wa Maisha ya Inshaa Allah.Endelea kujiuliza nani anawaruzuku, na wakiumwa nani anawaponesha na ukiendelea sana moja kwa moja utajikuta umetokezea kwenye Ukumbusho wa Nabii Ibrahim a.s anaitaja Inshaa Allah kama hivi, sura ya Ash- Shuara aya ya 78 mpaka 81
"ٱلَّذِى خَلَقَنِى فَهُوَ يَہۡدِينِ"
"Ambaye ameniumba na Yeye ananiongoza"
Hivyo ndio inavotakiwa Inshaa Allah, Uikubali (Qadar)yake, kwamba la mwanzo yeye ndio kakuumba, ikisha kama wewe msomi kumbuka yeye ndiye aliyekupa kufahamu, kama utajiri yeye ndie aliyekufungulia njia kiajabu ajabu, kama cheo yeye ndie alosababisha mpaka wewe ukawepo hapo, yeye ndie amuekaye amtakaye, na kumuondosha anayemtaka, yeye ndie anaekuongoza katika kila jambo, ila bado wewe hujashuka katika mji wa Imani moyoni mwako ukagundua hayo.
"وَٱلَّذِى هُوَ يُطۡعِمُنِى وَيَسۡقِينِ"
"Na Ambaye ananilisha na kuninywesha"
Papara zako ndio zenye kukutesa, kutaka cha ziada ndio kunakupa madhara, lakini ukitulia ukaamini kikweli basi utagundua kweli mimi Mollah wangu ndie ananilisha na kuninywesha, tena sio tu kukupa riziki, bali hata ukisha kukipika, jiulize nani anayeona ladha, nani anayejua chakula kitamu, yote hayo ni Uwezo wa Mwenye-enzi-Mungu, Yule ambaye unamuasi, Yule ambaye unamsahau, nini habari yako wewe Ukiumwa kidogo, huwezi kula wala kunywa, watu hawashughuliki na chakula wala maji ila wanahangaika na (Drip)mpige shindano, mnyweshe kwanguvu, nani leo atakupa uwezo wewe wa kula na kunywa, yote hayo yanatokea kwa Mollah wako, wewe huwezi kunyanyua hata kidole bila amri yake, imekuaje leo unayapa mgongo maisha alokujaalia ya Inshaa Allah.
"وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ "
"Na ninaposhikwa na maradhi yeye ndiye Ananiponesha"
Hivi ndio kuikubali (Qadar)Ninaposhikwa na Maradhi yeye kashanitengenezea (System)Maalumu, mimi nina jeshi yakiingia maradhi katika hili jumba langu basi kuna walinzi wananyanyuka bila ya mimi kuwapa amri na huanza kunilinda, mimi nina (Mabodyguard)kama ndege anavopona hendi hospital na mimi vilevile ninao uwezo huo ikiwa nitakamatana nayo Maisha ya Inshaa Allah, lakini weye, Malaria mtu anapiga bao, kichwa mtu anakwenda kwa mzee Mdumilo(Jina la kubuni), sasa hata (Doctor)hataki tena, kachoka na (Ampicilin)anataka lazima apate dawa ya Babu, hivi ndivo dunia inavotutesa kwa kuyapuuza Maisha ya Inshaa Allah.
"وَٱلَّذِى يُمِيتُنِى ثُمَّ يُحۡيِينِ"
"Na Ambaye atanifisha ikisha Atanihuisha"
Na nakubali mie baada ya Uhai wa duniani Mollah wangu ataniondosha na(Kufa)ikisha (Atanifufua kwa mara nyengine)
Huko ndio kuishi Maisha ya Inshaa Allah, na kuishi Maisha haya unatakiwa kukaribisha kila kitu, ukija utajiri sawa, nikiwa maskini sawa, nikiwa mzima kheri, na nikumwa pia niko radhi, ukiridhia mwenendo huo daima utakua furahani na huko ndiko kuishi kwa ajili ya kumtegemea Mollah wako wakati wote, Unakua unamkumbuka Mollah wako leo nini kakupangia, nani umtumikie, wapi atakutuma, nini atakupa upate kukitoa, wakati wote unajiweka katika kuongozwa Mwenye enzi Mungu.
Endelea Part 3

MAISHA YA INSHAA ALLAH PART 3
Asalaam Aleiykum,
Sasa inakuaje mimi na wewe Tunateseka? Tunateseka Sababu hatumtegemei Mwenye-enzi-Mungu, na yanokutesa ni haya ya kujipa Ushujaa, unakua mwenye kutaka zaidi, unajinasibu kwa kipato chako, Unashughulika na Maisha uloyachagua wewe ya kutafuta Mali, na zaidi kujitegemea kwa maarifa yako. Unatafuta utajiri kwa njia yoyote, Akili yako hata ukenda Nyumbani bado inabakia katika mbinu za kujitajirisha zaidi, Na kama utakua Maskini ndio mama yangu, balaa tupu, Baina ya wawili nyie hapana tafauti yoyote, nyote hamumkumbuki Mwenye enzi Mungu, mkikutana msikitini, maskini anangoja kuomba na Tajiri anasubiri kuombwa, Kila mmoja ana fikra zake vipi atamkaba mwenzie, vipi atakumbukwa Mollah katika mazingira kama hayo, na Mwenye enzi Mungu anaendelea kukumbusheni katika Quraan Adh-Dhaariyat 55:"وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ"
Na Endelea kuwakumbusha, maana ukumbusho huwafaa wanoamini.
Umo katika kukumbushwa nguzo hii muhimu ya (Qadir)unatakiwa kama Muumin wa kweli uanze kutafakari, yasome maisha yako, jirudie wewe mwenyewe ujikumbushe kuna mambo mangapi yamekutokezea kwa ajili ya Inshaa Allah, wacha kioo sasa kamata kalamu hebu yaandike, inaweza kuwa cheo, au mkeo au mumeo jinsi mlivokutana, inaweza kuwa mali ulivoipata, wewe una dalili nyingi za Inshaa Allah zimefanya kazi katika maisha yako lakini huzikumbuki, hebu zirejee ili zipate kukurudisha katika Imani.
56"وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ"
Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu.
Unachotakiwa ni Ibadah, ikisha mengine mwachie yeye Mollah wako atakuongoza kwa njia usozifahamu, tena bila ya dhiki wala misukosuko, kwa sababu mwenye kukuongoza ndio anajua kakupangia nini.
58"إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلۡقُوَّةِ ٱلۡمَتِينُ"
Hakika Mwenye enzi Mungu ndiye mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, (Na aliye)Madhubuti,
Naam hivyo ndivo ilivyo Imani, huku ndiko kuishi kwa kutegemea Inshaa Allah, hayo ndio maisha ya Kiroho ya kuamini mimi nimeumbwa na yupo Mwenye kunipa Riziki yangu, Lakini ukiishi kwa Kutegemea Akili yako, unayakaribisha mateso, baada ya kichwani mwako kumjaza Mwenye enzi Mungu, zinajaa Biashara, kinajaa Cheo, na Baada ya hapo Akili limefurika, vipi Utapunguza ili upumzike, unatafuta (Kosha Roho)lazima upate kitu cha (Siri)pembeni, na hakuna jengine ila upate(Kimada).
Maisha ya Inshaa Allah ndio Mollah wetu anayotaka sisi tuishi ikiwa tunamuamini kweli, katupa(Challenge)anatutaka tuabudu tu, ikisha mengine tumuachie Yeye, lakini wapi, hilo ndio lenye kutushinda, tunaacha kuabudu ikisha hao tunakwenda kutumia Masaa 15 kazini, na huku zinakushinda hata dakika 5 za kuabudu, Na kila ukitumia muda wako katika kutafuta haya unayoyaona mafanikio, na huku unazidi kwenda mbali na Mollah wako, Unazidi kuikimbia (Laa Ilah illah Allah)usije ukadhani mbona sitoki Msikitini, mbona nasimamisha Sala zote 5, sikatai kweli unayafanya hayo, lakini hebu katika hizo Sala zako jichunguze Unamsabahi Mollah wako, au unaendelea na mambo ya ofisini, au unapanga faida za biashara, au unaamua kesi ya watoto,pengine unatatua jawabu la mtihani, tizama nini kimo katika hiyo Sala, halafu ndio utajua mimi niko karibu na Mollah wangu, au karibu na mambo yangu.
Usije ukasema huyu anosema haya yeye yukoje, mimi niko kawaida hata (Kanzu)sivai, wala ndevu sina, usinifate ukaniuliza mbona hututishi, sina haja ya kukutisha, ninachofanya kukupa (Ukweli)ukiona unafaa chukua utie moyoni mwako, huna haja ya mwengine kujua anza leo Kuishi Mwenyewe kwa kutegemea Inshaa Allah, huna haja ya kumhadithia mtu isije Inshaa Allah ikakutoka, Na maisha haya yana Mtihani sio Rahisi ukaona si nikubali tu, ukiamua kuingia katika Maisha haya jijue sasa wewe umeamua kujiunga na Waumini, unajiunga kuwa Mcha Mungu, na ukitaka kujiunga lazima kwanza utizamwe jee huyu mkweli, jee kweli unaitegemea nguzo hii madhubuti ya (Qadar)ya Mwenye enzi Mungu, Basi kama kweli umejizatiti sawasawa wacha nikupeleke chumba cha Mtihani. Endelea Part 4

MAISHA YA INSHAA ALLAH PART 4
Asalaam Aleiykum,
Sasa ingia Chumba cha Mtihani uone kama kweli utapasi, fungua sura ya Baqarah aya ya 155 ili upate kuyajua maswali ya mtihani huo.
"وَلَنَبۡلُوَنَّكُم بِشَىۡءٍ۬ مِّنَ ٱلۡخَوۡفِ وَٱلۡجُوعِ وَنَقۡصٍ۬ مِّنَ ٱلۡأَمۡوَٲلِ وَٱلۡأَنفُسِ وَٱلثَّمَرَٲتِۗ وَبَشِّرِ ٱلصَّـٰبِرِينَ"
"Na tutakutieni katika Msukosuko wa hofu na njaa na upungufu wa Mali, wa watu na matunda, Na wabashirie(Wafahamishe)habari njema (wale)wanosubiri"
Naam limetumika neno moja la tutakutieni, ili upate kuzinduka, ikiwa kweli unataka kufaulu mtihani huu basi mwanzo kabisa ingia ndani ya hofu ishi ndani ya hofu, ichambue hiyo hofu kumbuka usije kupigana nayo, hofu daima inashinda na hofu ikishinda hapo balaa ndipo inapoanzia, kwanini ikaanzia hapo, sababu mwanaadamu ni Kiumbe pekee mwenye kutaka zaidi. Mollah wetu katupangia jambo moja ana hakikisha hili la Mahitajio ya lazima analikamisha pasi na wasiwasi, Lakini mwanaadamu ni mwenye kutaka lake la zaidi na hapo ndio hofu inakaa kiti cha mbele na kukutoa kwenye Inshaa Allah na kukuongoza kwenye Uharibifu.
Lau ungejua hofu ni kama Kivuli, basi usinge idekeza, na ukawa unaipalilia, hofu ndio inakupeleka utake cha kuweka Akiba, hapo ndipo safari ya Maradhi yote ya vita vya Maisha inapoanza, hapo ndio (Round About)ya kumsahau Mollah wako, kama utakua Maskini unataka utajiri, na kama Tajiri unataka Mali izidi(na aya imekwambia inapunguzwa)Na ukichunguza utagundua vita vyote vya Upuuzi, wewe na tajiri nyote mnakula chakula cha aina moja, pengine tajiri atakuzidi kwa (Ladha)yeye kautia nazi, au wake wapilau, lakini chakula ni kilekile, Shibe ni ileile,usingizi ni uleule, pumzi ni zilezile, sauti ni zenu ni hizo hizo, mwendo wenu nyote wa miguu miwili, kuona kwenu kote ni kumoja, akiumwa na wewe unaumwa, akikasirika na wewe unakasirika, katika Shani hii ya Mahitaji Mollah kaweka usawa, ila tafauti yenu mmoja kaamua kuishi Maisha ya Inshaa Allah na huyu wa pili kaamua kutumia mbinu zake, Na wewe ukiwa na mbinu zako, na wengine wanazao.
Vinaanza vita hapo kila mmoja kashatoka katika Njia ya Inshaa Allah hakamatiki, sasa unakua umeitafuta njia yako mwenyewe, tizama sasa ukiingia katika vichochoro hivi vya njia yako mwenyewe unakuaje, unakua una hofu, giza nene sijui itakuaje, unaendelea kupata dhiki mja wewe, kama una duka ukenda kusali unalibeba kichwani, sijui wanaiba, sijui nitapata faida, kama uko ofisini sasa unaogopa huyu mtoto mdogo aloletwa atachukua nafasi yangu au vipi, jee huyu ana haja na hichi cheo, unasahau hata kama Mungu alikuweka hapo mwanzo, na huyo unakimbilia kwa (mzee mlilo-jina la kubuni)eti akulindie cheo, na yeye anakutia mtihani anataka kitambaa cheusi ulookota barabarani, sijui mnaambiwa mlete na kucha za simba, eti ulindiwe mali au cheo hasara gani zimetufika hii leo, kawa mganga ndio mwenye kuilinda riziki, Shetani katutoa katika Maisha ya Inshaa Allah(Majaaliwa), katupeleka kwenye (Manyago)matupu, kichupa kiweke kwenye (Mafile)chukua Pete hili usilivue, wewe wakati unasoma ukapata hicho cheo mganga alikua wapi, basi hutumii hiyo akili hata kidogo.
Na ukiingia katika maasi hayo jua matatizo makubwa yanafatia, unaanza kuteseka, utaona mtu ana mali lakini hafurahi na mali yake sababu ya maradhi matupu, au kutwa anatafuta mali akirudi nyumbani usiku kucha anafunga hesabu hapati hata neema ya usingizi, na ukikosa usingizi unakuja wasiwasi ndipo unatafuta watu sasa ufatane nao, huna raha kabisa.
Na Maskini na yeye baada ya kumtegemea Mollah wake kwa Inshaa Allah, Laa na yeye anatoka mbio kwenda kupigana na maisha, na yeye anataka utajiri, anapotea kichochoroni na kumsahau Mollah wake, unamuona Msikitini lakini mawazo yote yapo kwenye doti za kanga alokopa atazilipa vipi, deni la fulani atamkwepaje, na vipi ataimaliza nyumba yake, hivo ndio sote maisha tunayoyachagua.
Sasa wenye kuishi Maisha ya Inshaa Allah wanakuaje?
Wnaishi kwa makubaliano na Mwenye enzi Mungu, wao wanakua ukinipa kula yangu, Alhamdulillah, ukininyima Laa Illah Illah Allah, Ukinipa cha zaidi Shukurani, ukininyima najua ndio kheri yangu, Mimi kwa upande wangu iajaribu, Najua na wewe Mollah wangu utanisaidia, mimi niwe muangalifu na mwenye subira, najua utanionesha ishara zako, zikiwa za kheri nizifate, na ikiwa za shari niziepuke, ukinipa kingi najua ni mtihani utokao kwako na ukininyima ni mtihani ambao mimi nimeukubali, Na kwanini nisiukubali hali ya kua wewe ndie uliyeniumba, ukanilea na kuninusuru nilivokua mdogo, nilipofikia wakati wa kufahamu Mollah wangu ukaniteremshia hekima ima niwe mfanya biashara au msomi, Na sasa naishi kama unavonitaka niishi kwa kukutegemea wewe Mollah wangu, na Maisha yangu yote nimekukabidhi wewe Mollah wangu muumba, nikiwa sina shaka utanitimizia kila mahitaji yangu yote. Na nitakapo taka cha ziada najua nimeamua kujitesa kwa jambo hilo.
Nakuomba Mollah wangu tujaalie Maisha haya ya Inshaa Allah tuwe wenye kukubali na kuiamini (Qadar)yako. tupe sisi Mioyo ya kufahamu kwamba wewe ndie mwenye kumpa huyu awe Raisi huyu awe Mfalme, yule awe Tajiri na huyu aishi maisha ya kawaida, tupe sisi zawadi Adhimu ya kukumbuka kuwa wewe ndie ulotuumba na wewe ndie mwenye maamuzi yote ya Mustakbal wa maisha yetu. Na jengine la zaidi tupunguzie harakati za maisha zinazotupelekea mpaka tukakusahu wewe, halafu tupe utulivu wa Kiroho na Moyo ili tuweke nafasi ndani ya nyoyo zetu nafasi ya kukumbuka wewe wakati wote tukiwa macho na fahamu zetu, Kwani hiyo ndio Ibadah, huo ndio Ucha Mungu, na hayo ndio Maisha ya Inshaa Allah.

Sunday, June 9, 2013
KISIWA CHA WACHA MUNGU PART 1
Asalaam Aleiykum,
Kinapotajwa kisiwa lazima mtu awe makini kuangalia ni kisiwa gani kilokusudiwa, chaweza kuwa kisiwa cha Unguja au Lamu, chaweza kuwa Pemba au Mafia, chochote au vyote katika hivyo kulikuwepo na bado wapo Wacha Mungu na mpaka hii leo wanaendelea na maisha yao Salama Usalimini, huku wakiendelea kufanya Ibada zao , hapa leo nawazungumza wale wa zama zile zilopita walotajwa katika vitabu vya karne za nyuma, na mfano ni mfano, waweza kuwa mfano ukakugusa ili upate kuzinduka, alaa kumbe kilicho kusudiwa ni kisiwa changu, na la pili kumbuka yaweza kisiwa hiki kipo ndani Moyoni au nje Ardhini wewe ndio utakua Hakimu wa uamuzi wa jambo hilo.
Pahala popote pakifanywa Ibada Mollah huteremsha baraka zake na Rehma zake ikawa hata wale watu wanoishi pale ni maskini lakini huteremshiwa Baraka za kila aina na mapenzi ya furaha yasiyo mfano, na yoyote mwenye kuishi katika Kisiwa cha Wacha Mungu huwa anahisi labda (yupo kwenye pepo ya Ulimwengu|)hujiwa na kila kitu, kuanzia chakula na mahitajio yote Mwenye enzi Mungu ana hakikisha waja wake wanatimiziwa, kutokana na (Special Energy)ya Ibada katika kisiwa hicho, basi huvutiwa watu wa Ulimwengu wote kukizuru kisiwa hicho, hapo huendelea kuzaliwa Wacha Mungu na wenye Hekima na Wasomi kadhalika, yanatokezea mapenzi katika Kisiwa cha Wacha Mungu watu wote wakawa wanaonana kila mmoja ndugu wa mwenzie.
Kama ilivyo desturi ya popote pale penye kizuri lazima kando kando pawepo Kibaya, hiyo ndio sheria ya Ulimwengu huu.
Wakapata habari wenyeji wa kando kando kuhusu mazuri na (Ibadah)zinofanyika Kisiwani huko, Kumbuka nimesema(Kando Kando)sio pembezoni (Hapo fanya tafsiri mwenyewe)mwa Bahari, waliposikia habari hii, wakafanya safari ya kukitembela kisiwa hiki wale wenyeji wa kando kando, na kwa bahati walipofika Kisiwani hapo watu wa mwanzo walokutana nao ni Wacha Mungu watatu wakifanya (Ibadah zao),waliwakuta wanaitegemea (Laaillah-illah-Allah)katika kila jambo lao wanalosema na kufanya basi hutanguliza neno hili, wakacheka sana wale wenyeji wa kando kando, vipi nyinyi kila (Ibadah)zenu mnataja neno hili yaonesha hamjui (Ibadah)au hata kama mnajua lakini hivi mfanyavo sivo, Wale Wacha Mungu wakauliza tuelekezeni vipi tufanye, kwani nyie mnaabudu vipi, kuna njia nyengine mnafanya kumridhisha Mollah wenu, pengine mmetuzidi daraja wenzetu, tunaomba tuelimisheni, wale wenyeji wa kando kando wakafahamisha vipi kufanya (Ibadah) ikisha hao wakachukua (Mashua au Ngarawa)wakaanza kuondoka kurejea katika mji wa Kando, walipofika masafa ya maili kadhaa wanageuka nyuma wanaona wale Wacha Mungu wanakuja mbio juu ya maji wanawakimbilia, walipofika karibu wakawaambia tumeghafilika yale maneno yametupotea, hebu tuelekezeni tena yanatamkwa vipi,Ikawafika hofu wenyeji wa kando kando huku wanatetemeka wakawaambia nendeni kasomeni kama mwanzo mlivokua mnasoma, dua zetu, masomo yetu hata siku moja hatujawahi kusimama kwenye Bahari namna hii, vipi leo tutakufundisheni nyinyi, Rudini na tusameheni.
Walipo rudi kwenye mji wao wale wenyeji wa kando kando wakapanga mpango wa kukihujumu kile kisiwa, kuwachafulia mwenendo na desturi zao, sababu kubwa kinatishia Usalama wa dini zao na mila zao huenda wakawafanya watu wao pia wakawa Wacha Mungu, mpaka hii leo kimechafuka kisiwa hichi na ile (Special Energy)yote ya Ibadah imetoweka, pahala palipokuwa na Wacha Mungu wakubwa wakubwa, wakizaliwa watu na Hekima zao na Elimu zao, leo kisiwa hiki kimerejeshwa kuwa hali ya chini kabisa, mpaka imefikia wakati sasa wao ndio wanasomeshwa Ucha Mungu.
Endelea Part 2

KISIWA CHA WACHA MUNGU PART 2
Asalaam Aleiykum,
Kisiwa hichi ninacho kizungumza kilifikia mpaka kutoa wanazuoni kwenda kusomesha katika Mji wa Makka, Kisiwa hiki kina historia kutoka kwa (Majini)yakua Nabii Suleiman a.s alikua akipumzika katika safari zake na Majeshi ya Kijini, hiyo ndio sifa ya Kisiwa cha Wacha Mungu, Nini leo kimetokea katika kisiwa hichi kwa muda mchache wa miaka ipatayo hamsini, yametokea haya, sura ya Al-Rumi aya ya 41"
"ظَهَرَ ٱلۡفَسَادُ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ بِمَا كَسَبَتۡ أَيۡدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعۡضَ ٱلَّذِى عَمِلُواْ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ"
"umedhihiri uharibifu katika Bara na baharini kwa sababu ya yale iliyoifanya mikono ya watu, ili awaonjeshe (Adhabu kwa)baadhi ya mambo waliyoyafanya, huwenda wakarudi( Na Kutubia kwa Mollah wao)"
Naam hayo ndio mambo yalotokea katika kisiwa cha wacha Mungu, imekithiri machafu ya Rushwa na maonevu, imezidi dhuluma na ufisadi, Uzinifu na machafu na mambo makubwa makubwa, Na huko Baharini ndio inapitishwa (Mihadarati)madawa ya kulevya na Ma(Picnic)za kwenye Maboti. Sasa nini anafanya Mollah wako? anawafinya wale Raia wakawaida anawapa adhabu ya umasikini na viongozi wao wanaletewa Maradhi makubwa makubwa, si kwa ajili ya kuwaonea ila anawataka warudi na kuwacha hayo wanayotenda watubu kwa ajili yake, lakini wapi kila maradhi yakizidi, na wao wanazidi, kila umasikini ukizidi na wao ndio wanazidi, tena sasa wanaondoshewa mpaka fahamu wanakua hawatambui chochote hata akija Mtu akawaambia moja na moja Tatu, wanakubali na kusherehekea hali wanajua tatu haigawiki kama ilivo moja, wakati wanajua moja na moja lazima zikutane ndio zifanye mbili, wakati wanajua tatu haupatikani usawa, lakini shetani kama alivowasahaulisha kurudi kwa Mollah wao na mengine vile vile anawasahaulisha ili kisiwa hiki kisirudi katika hali yake ya mwanzo kama kilivokua.
Nini kifanyike?
Sura ya Raad aya ya 11 " لَهُ ۥ مُعَقِّبَـٰتٌ۬ مِّنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ يَحۡفَظُونَهُ ۥ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِہِمۡۗ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوۡمٍ۬ سُوٓءً۬ا فَلَا مَرَدَّ لَهُ ۥۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ "
"(Kila Mtu)ana kundi la (Malaika)mbele yake na nyuma yake, wanamlinda(Na kuyadhibiti unayofanya)kwa amri ya Mwenye enzi Mungu, hakika Mwenye enzi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao"
Kwanza lazima kila mtu atizame kwenye bega lake na ajue kuna (Kiumbe)kinamuangalia, na kiumbe hichi kitakua shahidi kwa yote yanotendekeka(Ukipokea Rushwa usiangalie Askari unayemuona bali pia mtizame na yule usomuona, huyo ana hatari kubwa), halafu (Collective)Jamii nzima lazima ianze kubadilika na kujifunga katika mambo ya Ibada, na kuhimizana katika mambo ya kheri, kusaidiana katika dhiki, kuoneana huruma, kuyapinga kwa nguvu zote mambo ya maasi, basi na Kwa Upande wa Mwenye enzi Mungu nini kitafanyika, atakinyanyua na kukirejesha Kisiwa hiki katika hali yake kilivokua mwanzo, nyie mfanye jambo moja tu, nalo kuyarejea maneno ya Nabii Nuhu a.s aliyowaambia Kaumu yake(Nuhu aya ya 9 mpaka 12)
"ثُمَّ إِنِّىٓ أَعۡلَنتُ لَهُمۡ وَأَسۡرَرۡتُ لَهُمۡ إِسۡرَارً۬ا "
"Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri"
Mnatangaziwa kwenye mabomba na pia miskitini, jamani kisiwa kinaangamia, Ucha Mungu unapotea, vijana wanapotea na kuharibika hebu zindukeni, utamaduni wenu unabadilika nyinyi mlikua sio hivyo, lazima mtizame kuna nini kimesababisha haya, pengine tamaa ya maisha, pengine udhaifu wenu katika umaskini au fisadi za (Roho) ziliopo kwenye kisiwa hiki cha Wacha Mungu ndio mkaruhusu kudhibitiwa.
Akaendelea Nabii Nuhu a.s " فَقُلۡتُ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُ ۥ كَانَ غَفَّارً۬ا "
"Nikawaambia, ombeni msamaha kwa Mollah wenu, hakika yeye ni Mwingi wa Msamaha"
Kinachotakiwa ni kutubu tu, watu warejee kwenye Ucha Mungu kila kitu mtapata baada ya kufanya hivyo.
" يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارً۬ا "
"Atakuleteeni mawingu yanyeshao mvua nyingi".
Maana yake hapo itakuondokeeni shida ya vyakula, mazao yatakua mengi, mtapata matunda ya kila aina kama ilivokua mwanzo.
"وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٲلٍ۬ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّـٰتٍ۬ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡہَـٰرً۬ا "
"Na atakupeni mali na watoto, na atakupeni mabustani, na atakufanyieni mito"
Naam kama mtarejea katika Ucha Mungu, basi Mali itamiminwa(Mtajua wenyewe kama Mafuta au Almasi, au pengine mtachimbuliwa gesi au madini ya kila aina)lakini kinachotakiwa ni kitu kimoja kuweni watu wema, Rejeeni kama zamani, yaepukeni maasi, chukieni vitendo viovu, mkifanya hivyo mtapewa watoto asilia wa kisiwa hiki, yatafanywa mabustani ya kila aina, na mpaka mito mnaweza kutengeneza wenyewe. Hiyo ndio hali ya kisiwa hiki na vengine vilivyokua na Ucha Mungu, shime ni kufanya jitihada na kuvirejesha katika hali yake ya zamani yenye mvuto mpya wa Ucha Mungu na maendeleo. Na kama umekigundua kisiwa hiki basi kiombee dua kiwe chenye kuwa Nuru ya Bara na Baharini, Omba kwa Mollah akiondoshee Maasi na Uchafu ulokithiri hivi sasa, na la Mwisho awatie udugu na upendo wakaazi wake wote wapendane kwa ajili yake Mollah Mlezi mwenye kuwarithisha Visiwa hivi Kaumu anayoichagua yeye.Mollah wangu kilinde kisiwa hiki na Uharibifu na njama za aina yoyote ile ikisha warithishe waja wema wakae kwa utulivu na masikizano. Amin.

Sunday, June 2, 2013
MARAFIKI WA PEPONI PART 1
Asalaam Aleiykum,
Unataka kumjua Nani atakua Rafiki yako wa Peponi kama utaingia?basi ipitie darsa hii kwa uangalifu mkubwa ujue nani atakua mwenzio huko Akhera, akitangulia au ukitangulia yategemea vipi uliishi katika Ulimwengu huu na Ulifanya nini kuhusiana na Sheria na Kanuni ulizofahamishwa uzifate, Unapata habari hii ili kupewa nafasi ya kujibadilisha wakati bado muda unao.
Mwanaadamu mwanzo anapozaliwa anaishi na kukua kwa uangalifu wa Robo ya Maisha inayomshughulisha kupita katika wakati wa Ujana, Ndani ya Robo hii unapatikana msukosuko mkubwa wa kuyaweka maisha ya Mja huyu yawe sawa, Katika pita pita za Umri huo wa ujana unapita katika kipindi cha mwanzo kufungiwa mambo kadhaa likiwemo hili la Elimu na Matamanio(sex), mpaka muda maalumu ulopangwa ukiwasili yanaanza kufunga mawili haya (au kwa lugha nyengine unaonja Tunda)na ukilimega hilo tunda tu mambo yanaanzia hapo, hapo tena yupo mwenye kuonja sigara au ulevi, mwenye kupata (rafiki wa kike au wakiume) iwe kwenye mawazo au kikweli kweli lakini hiyo ndio hali inayotokezea kwetu sote katika mpito huo, na kuna wengine walo bahatika wao wanaonja tunda la fahamu(Elimu)moja kwa moja na wanakita nguvu zao katika upande wa taaluma, kotekote lakini lazima (Tunda) tulitafune, na ukishalitafuna tu inaanza Safari ya kumtafuta yule mlopoteana kutoka huko (Mbinguni) na sasa mnatafutana katika msitu wa (Ardhini).
Kutokana na mtafutano huo ndio huyu anahangaika huku na yule anahangaika kule, Na huku Umri unasogea mpaka pale Mollah anapokuongoza na kukuteremshia Penzi lilofichika Moyoni ikawa wewe Mwenyewe hujui na huyo Mwenzio hajui ikawa wawili nyie mna hamu na shauku kubwa ya kutaka kuishi pamoja, nini kimetokea kati yenu? Kabla hujenda mbali kiulize (Kitabu kitukufu) kuhusiana na Habari hii:
"وَمِن ڪُلِّ شَىۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ"
"Na katika kila kitu tumeumba(Pairs or Patners)Jike na Dume ili Mpate kuzingatia"
Sasa hebu leo zingatia huyu ninaye Ishi naye au ninayetaka kumuoa kweli ni (Soul Mate)wangu, Na kama kweli huyu ni mwenzangu tulokutana katika Ulimwengu huu kwanini namfanyia mengi ya karaha na maudhi hali najua huyu ni nusu ya Mimi, nini hichi kilofichika Moyoni mwangu ikawa nimegandana na kiumbe huyu hata nikimchukia ndio nazidi kumpenda, kila tukigombana baadae tunasamehe nyoyoni, kumbuka wakati wote hicho kilofichika kwa siri katika moyo wako kina (Mionzi)mikali ya (Mahaba) na kila ukitoa sumu basi mionzi hiyo inamurika na kuyayusha sumu yote iloingia kati yenu, Sababu kubwa itizame vipi hali unayokuwa endapo utajifinya mwenyewe machungu unayo hisi, ndio maana nyumba ikiwa na magonvi, au wapenzi wawili wakigombana au kukerana wanakuwa kama wagonjwa.(Sisemi haya mkadhani ni porojo)bali na nyinyi yachunguzeni.
Kwanini Mkakutana? Quraan sura ya Hadid aya ya 22:
" مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِىٓ أَنفُسِكُمۡ إِلَّا فِى ڪِتَـٰبٍ۬ مِّن قَبۡلِ أَن نَّبۡرَأَهَآۚ إِنَّ ذَٲلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ۬"
"Hautokei msiba katika Ardhi wala katika nafsi zenu ila umeshaandikwa katika kitabu, kabla hatujauumba, kwa hakika hilo ni (Jambo)rahisi kwa Mwenye enzi Mungu"
Usije ukasema mbona pametajwa Msiba, nini kinyume cha msiba, ni furaha, na hiyo furaha ni (Nature) yako kama ilivyo afya yako, ndio maana ukatajwa msiba sababu ndio unao kuhuzunisha na kukunyima hiyo furaha, Naam kwa hiyo kila kitu kimeumbwa(Pairs) na kila kitu kishaandikwa kabla ya hapo, hapa itataka uchambuzi kidogo kabla ya kuendelea, najua mshatoa mapanga ya Ulimi kutaka kunijeruhi, kwa hiyo wacha niweke sawa ili tupate kuendelea na darsa hii ya nani atakua Rafiki yako Peponi.
kutaka kuyajua hayo Endelea part 2

MARAFIKI WA PEPONI PART 2
Asalaam Aleiykum,
Katika kupata uchambuzi wa jambo hilo inakuaje mambo yote yashaandikwa, basi mimi sina haja ya kuogopa au kuchukua tahadhari, sasa mwanzo kabisa tazama (Mifano) hii michache halafu utajijibu wewe mwenyewe ili upate kuzingatia, (Kuzaliwa kwako, kufa kwako, kuvuta kwako pumzi, kulala na kuamka kwako,vipi unavokula nani anasaga chakula chako,fikira zako mbona zinakuja bila ya wewe kutarajia na mengi mengineyo ambayo utayachunguza mwenyewe)yanatokea mambo haya bila ya ridhaa yako, kwa hiyo utaona kuna mambo una mamlaka nayo na kuna mambo huna mamlaka nayo, yale ulokua na mamlaka nayo hayo ndio utahukumiwa kutokana na matendo yake ima yawe mazuri au mabaya utalipwa kutokana na kadir ya uzito wake, Na hiyo ndio maana ya kuandikwa kabla ya hapo, Ama hili la kukutana na mwenzio hili liko katika njia ya Mwenye Enzi Mungu ikiwa wewe mwenyewe utaliridhia litokee, halazimishwi mtu katika hilo.
Sasa Jee Ushakutana na Rafiki wa Peponi?
Jee huyo unayeishi naye unataraji uwe naye pamoja peponi, usifurahi ukaona kama nakupa ufunguo sasa ingieni, laa panataka kazi,(Isiwe kama Hadith ya wale mke na mume walopendana wakataka kuishi pamoja peponi, siku walogombana mwanamme kalala akaota kaingia peponi kakaa kwenye kiti wanapita Mahrul-ein, mara akahisi mtu anampiga kwenye bega ikisha akamnongoneza nipo, yule bwana kugeuka anamuona Mkewe kikamtoka kibao usingizini)msiwe kama hivyo hamtoipata pepo abadan, mtamalizikia na maradhi na majonzi maisha yote, sasa vipi mnatakiwa kukaa wewe na mwenzio, Hapa itabidi tujikumbushe maneno ya Kipenzi wetu Mtume s.a.w aliposema "Atakapo (funga)Ndoa Mja, itakua kakamilisha Nusu ya Dini, na huko Kumcha Mungu (Taqwa)ni nusu ilobakia" umepita katika Robo ya kwanza ya mtafutano, sasa umeingia katika nusu na jambo la kuoa au kukutana na mwenzio Bwana Mtume s.a.w kalihusisha na Nusu nzima ya Dini,(Nini Dini?)Dini ni mwenendo mzima wa Maisha, na hili la ndoa inakua ushafika nusu njia, ndio maana ukizini inakua umetenda Dhanbi kubwa, umerejea kwenye Robo, umefanya ufisadi, umetoka kwenye njia, wewe umedhulumu, ushapewa nusu nzima bado unatafuta na nusu za watu, ndio ikaamrishwa mpige makwaju mia huyu hafai kabisa, tena na zaidi mtangazie kwa jamii huyu mzinifu, huyu anayachafua maisha, huyu hatosheki, Mua anao ndani anakwenda kuokota Maganda yake, wakati Mua huo huo anaweza kufanya (Juice)au kutengeneza Sukari, mwenzenu huyu mgonjwa.
Jee ushakutana na Rafiki yako wa Peponi? Pata habari hii ili upate kujirekebisha, upate kurejesha mapenzi, upate kuridhika na ulichonacho. Imekua Nusu, sababu kutokana na hayo mapenzi nyinyi mekutana, kutokana na hayo mapenzi Mollah kakupeni watoto, akakutieni huruma kuvilea vitoto hivyo kwa uangalifu na unyenyekevu mkubwa, akakuleteeni furaha katika maisha yenu mkawa na afya mnacheka na kulia pamoja, vitoto vinakua vikubwa huku mkiviona, akawa Mollah wenu anakuruzukuni pasi hesabu, kwa njia za kila aina mnapata mstakbali wenu, vipi leo wewe unakua katili kwa (Your Other half)vipi leo unamuendea kinyume mwenzio, vipi leo unafika kumpiga na kumtolea ukali mwenzio, kwanini humpi heshima anayokupa wewe, kwanini huiweki nyumba yako ya Ardhini salama na Amani ili na ya huko Akhera iwe yenye mfano huo huo kama utaingia.Jitahidi sana uwe mbora na mzuri wa Roho kuliko mzuri wa sura na Mwili.
Vipi utajua umekutana na mwenzio, kuna mifano mingi ya kukujulisha huyu kweli ni mwenzangu, kwanza kabisa tizama tabia, vipi mnavyopendana, Mahusiano ya Kiroho daima yanakua si yenye masharti lazima uwe tajiri au uwe na cheo, au uwe mzuri, vipi maisha yenu yanavokwenda, jee Baraka zinatushukia baina yetu, isiwe ukatizama Baraka za riziki tu bali hata afya, furaha vinapatikana kwa mwenzangu huyu, Na kama kuna machafuko itumie nafasi hii kuanza kutafakari sasa vipi utabadilisha na kuituliza hali hiyo, la Mwanzo kabisa fanya uwe karibu sana na mwenzio huyu, achana na Marafiki wa Kidunia, itafute siri hii yakua huyu nilonaye hivi sasa pia tutakua pamoja tukiondoka kwenye Ulimwengu huu, Jaribu kuwa mstahamilivu, fanya upole kama mwenzio mkali, kuwa mtiifu kwa mwenzio na kumfurahisha kila ukipata nafasi, Muhimize bila ya kuchoka mkamatane katika njia ya Ibada kwa ajili ya Mwenye enzi Mungu, Jaribu kupata ukaribu wa kushikana mikono, kaeni pamoja katika mazungumzo, peleka ishara za mapenzi usisubiri mpaka uwe na matamanio ndio uanze kumkurubia mwenzio, ukifanya hivyo utajua kama kweli umekutana na mwenzio au unaishi na mtu anayekudanganya. Na ukiligundua hilo kunakitu kitatokea ambacho kitakujulisha ama kweli huyu mwenzangu, nini kitu hicho?. Endelea Part 3

MARAFIKI WA PEPONI PART 3
Asalaam Aleiykum,
Kinatokea kitu kipya baada ya Umri wenu kusogea, na kama kweli mumeishi kwa wema na uaminifu, kusameheana na kupendana kikweli, hapo mapenzi yanapotea hadharani na kubakia moyoni kama vile mwanzo nilivo hadithia, hadharani inabaki Rehema ya Urafiki wa Kiroho unaodumu milele kwa kusaidiana na kuwa pamoja kwa hali na mali, unabaki umoja ulofunganisha (familia nzima kuwa kitu kimoja).Yanapotea matamanio na kubaki Maradhiano ya Kiroho katika mambo ya Ibada na Taqwa, kila mmoja anakua mbioni kujitaarisha na safari ndefu ya kwenda kukutana na Mollah wake na kutaraji kufufuliwa na kupewa Zawadi ya Mapenzi ya kukutanishwa na mwenzie tena na kuingizwa Peponi kuishi humo Milele kwa mapenzi na Furaha.
Na Mwenye enzi Mungu anatupa ahadi kwa wale alowapa zawadi hii ya kuwakutanisha katika Ulimwengu ikisha wakafanya nini?
Quraan sura ya Muumin aya ya 8,
"وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٲعُونَ"
"Na ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia"
Mwenye enzi Mungu anakupa amana kadhaa ikiwemo hii ya kufunga (Ndoa)yakua umekutana na mwenzio na sasa unaamua kuishi maisha ya sheria za Kiroho, na unachukua ahadi yakua utaingalia amana hii na nyengine atakazo kukabidhi Mollah wako kama watoto na kadhalika, sasa ole wao wale wenye kuwanyanyasa wanawake au wanaume, hao wamevunja kile kiapo cha ahadi, na yatakayo wafika basi wajue wameyataka wenyewe hakuna wa kumlaumu.
Na ikiwa umeishi kwa uangalifu katika Ulimwengu huu, ukatenda wema na kujiepusha na mabaya basi Mollah wako anakuahidi katika sura ya Zukhruf aya ya 68 mpaka 71
"يَـٰعِبَادِ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡكُمُ ٱلۡيَوۡمَ وَلَآ أَنتُمۡ تَحۡزَنُونَ"
"Enyi waja (wangu wema)hamtakua na hofu siku hiyo wala hamtohuzunika"
Nyinyi mlikua mkitenda mazuri katika dunia, mkiishi uzuri na wenzenu, mkiwafanyia ihsani, mkistahamiliana,mkipendana,mkitizamana kwa macho ya huruma ikisha kubwa zaidi ni hili:
"ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِـَٔايَـٰتِنَا وَڪَانُواْ مُسۡلِمِينَ "
"Ambao waliziamini aya zetu na walikuwa waislamu kamili"
Kumbuka maneno ya Bwana Mtume s.a.w "Nusu ilobaki ni" "Kumcha Mollah" Na huo ndio Uislamu kamili ulokusudiwa hapo, kwanza umeziamini aya, halafu ukakamilisha hayo maisha(Dini) na kuwa Mkamilifu, nini sasa malipo yako kutoka kwa Mollah wako.
"ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ أَنتُمۡ وَأَزۡوَٲجُكُمۡ تُحۡبَرُونَ"
Ingieni Bustanini(Peponi)nyinyi na wake zenu(na humo)Mtafurahishwa.
Sasa kutana na Mkeo, kutana na Rafiki yako uloishi naye kwa wema, mkawa mnapendana na kumtii Mollah wenu, ingieni pamoja mkaone Raha za huko peponi.
"يُطَافُ عَلَيۡہِم بِصِحَافٍ۬ مِّن ذَهَبٍ۬ وَأَكۡوَابٍ۬ۖ وَفِيهَا مَا تَشۡتَهِيهِ ٱلۡأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلۡأَعۡيُنُۖ وَأَنتُمۡ فِيهَا خَـٰلِدُونَ"
(Humo)Watakua wanapitishiwa sahani za Dhahabu na Vikombe, Na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.
Naam yote hayo mtayapata, wanakuhudumieni wafanyakazi wa Mbinguni, mtapata humo huo utajiri mnaoumezea mate hapa Duniani, na jua kila unachokipenda nafsi ikakosa katika Ulimwengu huu basi utakikuta huko kesho uendako, kama unapenda ugali wa muhogo utaukuta kwa magunia, na yale yote macho ambayo yalikua yanafurahia na hurusiwi pengine kuona huko utawekewa wazi ili upate kuviona, kwa hiyo usisikitike sana kama unavikosa hapa Ulimwenguni jua utavipata vyote kwa idhini ya Mollah wako.
Ila hapa duniani zidisha subira, jifunze kukinai, wacha tamaa na kaa vizuri na mwenzio ili upate kufanikiwa kwa hayo mazuri ya Peponi ambayo tunamuomba Mollah wetu aturuzuku kwa Uwezo wake.Amin.

Subscribe to:
Posts (Atom)