Asalaam Aleiykum,
Ikiwa hiyo ndio hali anayobakia nayo mzinifu, nini hali za wenye kunywa ulevi, wale wenye kuvuta bangi na mirungi siku ya vunja jungu, na wao hali kadhalika wanabakiwa na mabaki ya pombe na mirungi kwenye (Body) Miili yao, na hakuna anayepata Rehma ya (Saum-Funga) kabisa. Na hata kama wakifunga basi ni bure ni sawa kujitesa na njaa, na kama ukibisha hayo hebu Muulizeni mgonjwa wa sukari eti kweli (Doctor) wanajua kiwango cha sukari ulokula miezi mitatu ilopita, akipimwa damu taarifa zote zimo anaambiwa ulikua ukiipiga vijiko vingapi kwa siku, ikiwa bado unapinga kaulize vipi anayekufa kwa ulevi akipimwa baada ya mwezi mzima wanakwambia aliuchapa chupa ngapi, na wanasayansi hawakuishia hapo sasa wamevumbua (Chemical)fulani wakikutia kwenye ngozi wanakwambia (Gomba au Bangi) umevuta wiki ya jana au umekula wiki mbili zilizopita, (Puri)ulovuta bado inaonesha kwenye damu na hivyo ndio Mwenye enzi Mungu anavodhihirisha mambo yake mpate kujua kila mnalotenda linabakia (Rekodi) zake kwenye (Mwili) wako, sasa jiulize kwa hali hii ya Kuvunja Jungu kila ufisadi unabakia jee Funga ninayo?
Na wale wenye kuvunja jungu kwa (Party au Taarab) wao ndio wanapigwa picha kabisa na ushahidi upo na kama watabisha basi wataambiwa subirini, "Yaasin 65"
"ٱلۡيَوۡمَ نَخۡتِمُ عَلَىٰٓ أَفۡوَٲهِهِمۡ وَتُكَلِّمُنَآ أَيۡدِيہِمۡ وَتَشۡہَدُ أَرۡجُلُهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ "
siku hiyo tutaifunga midomo yao, na itazungumza (na sisi)mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokua wakiyachuma.
Mimi wakati navunja jungu nilikua nainua mikono juu natamba kukuasi Mollah wangu, Na miguu nayo itashuhudia kweli mimi nilikua nanyanyua visigino halafu nakatika viuno ili nipate kuwachafua waja wako Akili zao, ili wapate kukuasi wewe Mollah wangu, Huingia viumbe hawa katika Mwezi wako Mtukufu hawana (Taqwa) wala si wasafi mwezi mzima mawazo yao yamo kwenye hadith za vunja jungu.
Hizo ndio hasara za vunja jungu, ikisha siku ya Qiyama mkiamrishwa kwenda Motoni mtaanza kushangaa pembezoni mwa Shimo la (Jahannam) mnasema mbona tulikua tukifunga, wataamrishwa Malaika wasukumeni, watakukamateni visogoni kabla ya kukusukumeni watakuulizeni maneno haya"Sura ya Mulk aya ya 8 na 9.
"تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلۡغَيۡظِۖ كُلَّمَآ أُلۡقِىَ فِيہَا فَوۡجٌ۬ سَأَلَهُمۡ خَزَنَتُہَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَذِيرٌ۬"
Unakaribia kupasuka kwa hasira, kila mara litakapotupwa(Shimoni)humo kundi(La wabaya)walinzi wake (Malaika)watawauliza jee hakukufikieni(Nyinyi) muonyaji.
"قَالُواْ بَلَىٰ قَدۡ جَآءَنَا نَذِيرٌ۬ فَكَذَّبۡنَا وَقُلۡنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَىۡءٍ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ۬ كَبِيرٍ۬ "
Watasema kwanini, alitujia Muonyaji, lakini tulikadhibisha na tulisema, Mwenye enzi Mungu hakuteremsha chochote, nyinyi mko katika upotofu mkubwa.
Tulifikia hata kusoma hasara za Vunja jungu, lakini tulikua tunajipa tamaa hakuna chochote, tunatishana tu mambo ya kutiana woga, lakini kwa wale walozinduka basi usilivunje jungu, bali wewe lijenge ulitie saruji liwe madhubuti kwa kusoma Quraan kwa wingi, kwa kuzidisha sala za sunna na kumsabahi na kumkumbuka Mollah wako kuanzia sasa na nakupa muongoz ukifanya hivyo Ramadhan yako safari hii itakua ya namna nyengine kabisa.
Namuomba Mollah wetu atuepushe na Maasi, atupe (Taqwa) na mapenzi yake, atupe afya tuweze kusimamisha nguzo hii na nyengine kwa ajili yake. Amin
No comments:
Post a Comment