Asalaam Aleiykum,
Kisiwa hichi ninacho kizungumza kilifikia mpaka kutoa wanazuoni kwenda kusomesha katika Mji wa Makka, Kisiwa hiki kina historia kutoka kwa (Majini)yakua Nabii Suleiman a.s alikua akipumzika katika safari zake na Majeshi ya Kijini, hiyo ndio sifa ya Kisiwa cha Wacha Mungu, Nini leo kimetokea katika kisiwa hichi kwa muda mchache wa miaka ipatayo hamsini, yametokea haya, sura ya Al-Rumi aya ya 41"
"ظَهَرَ ٱلۡفَسَادُ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ بِمَا كَسَبَتۡ أَيۡدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعۡضَ ٱلَّذِى عَمِلُواْ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ"
"umedhihiri uharibifu katika Bara na baharini kwa sababu ya yale iliyoifanya mikono ya watu, ili awaonjeshe (Adhabu kwa)baadhi ya mambo waliyoyafanya, huwenda wakarudi( Na Kutubia kwa Mollah wao)"
Naam hayo ndio mambo yalotokea katika kisiwa cha wacha Mungu, imekithiri machafu ya Rushwa na maonevu, imezidi dhuluma na ufisadi, Uzinifu na machafu na mambo makubwa makubwa, Na huko Baharini ndio inapitishwa (Mihadarati)madawa ya kulevya na Ma(Picnic)za kwenye Maboti. Sasa nini anafanya Mollah wako? anawafinya wale Raia wakawaida anawapa adhabu ya umasikini na viongozi wao wanaletewa Maradhi makubwa makubwa, si kwa ajili ya kuwaonea ila anawataka warudi na kuwacha hayo wanayotenda watubu kwa ajili yake, lakini wapi kila maradhi yakizidi, na wao wanazidi, kila umasikini ukizidi na wao ndio wanazidi, tena sasa wanaondoshewa mpaka fahamu wanakua hawatambui chochote hata akija Mtu akawaambia moja na moja Tatu, wanakubali na kusherehekea hali wanajua tatu haigawiki kama ilivo moja, wakati wanajua moja na moja lazima zikutane ndio zifanye mbili, wakati wanajua tatu haupatikani usawa, lakini shetani kama alivowasahaulisha kurudi kwa Mollah wao na mengine vile vile anawasahaulisha ili kisiwa hiki kisirudi katika hali yake ya mwanzo kama kilivokua.
Nini kifanyike?
Sura ya Raad aya ya 11 " لَهُ ۥ مُعَقِّبَـٰتٌ۬ مِّنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ يَحۡفَظُونَهُ ۥ مِنۡ أَمۡرِ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوۡمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنفُسِہِمۡۗ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوۡمٍ۬ سُوٓءً۬ا فَلَا مَرَدَّ لَهُ ۥۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ "
"(Kila Mtu)ana kundi la (Malaika)mbele yake na nyuma yake, wanamlinda(Na kuyadhibiti unayofanya)kwa amri ya Mwenye enzi Mungu, hakika Mwenye enzi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao"
Kwanza lazima kila mtu atizame kwenye bega lake na ajue kuna (Kiumbe)kinamuangalia, na kiumbe hichi kitakua shahidi kwa yote yanotendekeka(Ukipokea Rushwa usiangalie Askari unayemuona bali pia mtizame na yule usomuona, huyo ana hatari kubwa), halafu (Collective)Jamii nzima lazima ianze kubadilika na kujifunga katika mambo ya Ibada, na kuhimizana katika mambo ya kheri, kusaidiana katika dhiki, kuoneana huruma, kuyapinga kwa nguvu zote mambo ya maasi, basi na Kwa Upande wa Mwenye enzi Mungu nini kitafanyika, atakinyanyua na kukirejesha Kisiwa hiki katika hali yake kilivokua mwanzo, nyie mfanye jambo moja tu, nalo kuyarejea maneno ya Nabii Nuhu a.s aliyowaambia Kaumu yake(Nuhu aya ya 9 mpaka 12)
"ثُمَّ إِنِّىٓ أَعۡلَنتُ لَهُمۡ وَأَسۡرَرۡتُ لَهُمۡ إِسۡرَارً۬ا "
"Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri"
Mnatangaziwa kwenye mabomba na pia miskitini, jamani kisiwa kinaangamia, Ucha Mungu unapotea, vijana wanapotea na kuharibika hebu zindukeni, utamaduni wenu unabadilika nyinyi mlikua sio hivyo, lazima mtizame kuna nini kimesababisha haya, pengine tamaa ya maisha, pengine udhaifu wenu katika umaskini au fisadi za (Roho) ziliopo kwenye kisiwa hiki cha Wacha Mungu ndio mkaruhusu kudhibitiwa.
Akaendelea Nabii Nuhu a.s " فَقُلۡتُ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُ ۥ كَانَ غَفَّارً۬ا "
"Nikawaambia, ombeni msamaha kwa Mollah wenu, hakika yeye ni Mwingi wa Msamaha"
Kinachotakiwa ni kutubu tu, watu warejee kwenye Ucha Mungu kila kitu mtapata baada ya kufanya hivyo.
" يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارً۬ا "
"Atakuleteeni mawingu yanyeshao mvua nyingi".
Maana yake hapo itakuondokeeni shida ya vyakula, mazao yatakua mengi, mtapata matunda ya kila aina kama ilivokua mwanzo.
"وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٲلٍ۬ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّـٰتٍ۬ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡہَـٰرً۬ا "
"Na atakupeni mali na watoto, na atakupeni mabustani, na atakufanyieni mito"
Naam kama mtarejea katika Ucha Mungu, basi Mali itamiminwa(Mtajua wenyewe kama Mafuta au Almasi, au pengine mtachimbuliwa gesi au madini ya kila aina)lakini kinachotakiwa ni kitu kimoja kuweni watu wema, Rejeeni kama zamani, yaepukeni maasi, chukieni vitendo viovu, mkifanya hivyo mtapewa watoto asilia wa kisiwa hiki, yatafanywa mabustani ya kila aina, na mpaka mito mnaweza kutengeneza wenyewe. Hiyo ndio hali ya kisiwa hiki na vengine vilivyokua na Ucha Mungu, shime ni kufanya jitihada na kuvirejesha katika hali yake ya zamani yenye mvuto mpya wa Ucha Mungu na maendeleo. Na kama umekigundua kisiwa hiki basi kiombee dua kiwe chenye kuwa Nuru ya Bara na Baharini, Omba kwa Mollah akiondoshee Maasi na Uchafu ulokithiri hivi sasa, na la Mwisho awatie udugu na upendo wakaazi wake wote wapendane kwa ajili yake Mollah Mlezi mwenye kuwarithisha Visiwa hivi Kaumu anayoichagua yeye.Mollah wangu kilinde kisiwa hiki na Uharibifu na njama za aina yoyote ile ikisha warithishe waja wema wakae kwa utulivu na masikizano. Amin.
No comments:
Post a Comment