Sunday, June 2, 2013

MARAFIKI WA PEPONI PART 1

Asalaam Aleiykum,

Unataka kumjua Nani atakua Rafiki yako wa Peponi kama utaingia?basi ipitie darsa hii kwa uangalifu mkubwa ujue nani atakua mwenzio huko Akhera, akitangulia au ukitangulia yategemea vipi uliishi katika Ulimwengu huu na Ulifanya nini kuhusiana na Sheria na Kanuni ulizofahamishwa uzifate, Unapata habari hii ili kupewa nafasi ya kujibadilisha wakati bado muda unao.
Mwanaadamu mwanzo anapozaliwa anaishi na kukua kwa uangalifu wa Robo ya Maisha inayomshughulisha kupita katika wakati wa Ujana, Ndani ya Robo hii unapatikana msukosuko mkubwa wa kuyaweka maisha ya Mja huyu yawe sawa, Katika pita pita za Umri huo wa ujana unapita katika kipindi cha mwanzo kufungiwa mambo kadhaa likiwemo hili la Elimu na Matamanio(sex), mpaka muda maalumu ulopangwa ukiwasili yanaanza kufunga mawili haya (au kwa lugha nyengine unaonja Tunda)na ukilimega hilo tunda tu mambo yanaanzia hapo, hapo tena yupo mwenye kuonja sigara au ulevi, mwenye kupata (rafiki wa kike au wakiume) iwe kwenye mawazo au kikweli kweli lakini hiyo ndio hali inayotokezea kwetu sote katika mpito huo, na kuna wengine walo bahatika wao wanaonja tunda la fahamu(Elimu)moja kwa moja na wanakita nguvu zao katika upande wa taaluma, kotekote lakini lazima (Tunda) tulitafune, na ukishalitafuna tu inaanza Safari ya kumtafuta yule mlopoteana kutoka huko (Mbinguni) na sasa mnatafutana katika msitu wa (Ardhini).
Kutokana na mtafutano huo ndio huyu anahangaika huku na yule anahangaika kule, Na huku Umri unasogea mpaka pale Mollah anapokuongoza na kukuteremshia Penzi lilofichika Moyoni ikawa wewe Mwenyewe hujui na huyo Mwenzio hajui ikawa wawili nyie mna hamu na shauku kubwa ya kutaka kuishi pamoja, nini kimetokea kati yenu? Kabla hujenda mbali kiulize (Kitabu kitukufu) kuhusiana na Habari hii:
"وَمِن ڪُلِّ شَىۡءٍ خَلَقۡنَا زَوۡجَيۡنِ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ"
"Na katika kila kitu tumeumba(Pairs or Patners)Jike na Dume ili Mpate kuzingatia"
Sasa hebu leo zingatia huyu ninaye Ishi naye au ninayetaka kumuoa kweli ni (Soul Mate)wangu, Na kama kweli huyu ni mwenzangu tulokutana katika Ulimwengu huu kwanini namfanyia mengi ya karaha na maudhi hali najua huyu ni nusu ya Mimi, nini hichi kilofichika Moyoni mwangu ikawa nimegandana na kiumbe huyu hata nikimchukia ndio nazidi kumpenda, kila tukigombana baadae tunasamehe nyoyoni, kumbuka wakati wote hicho kilofichika kwa siri katika moyo wako kina (Mionzi)mikali ya (Mahaba) na kila ukitoa sumu basi mionzi hiyo inamurika na kuyayusha sumu yote iloingia kati yenu, Sababu kubwa itizame vipi hali unayokuwa endapo utajifinya mwenyewe machungu unayo hisi, ndio maana nyumba ikiwa na magonvi, au wapenzi wawili wakigombana au kukerana wanakuwa kama wagonjwa.(Sisemi haya mkadhani ni porojo)bali na nyinyi yachunguzeni.
Kwanini Mkakutana? Quraan sura ya Hadid aya ya 22:
" مَآ أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِىٓ أَنفُسِكُمۡ إِلَّا فِى ڪِتَـٰبٍ۬ مِّن قَبۡلِ أَن نَّبۡرَأَهَآ‌ۚ إِنَّ ذَٲلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ۬"
"Hautokei msiba katika Ardhi wala katika nafsi zenu ila umeshaandikwa katika kitabu, kabla hatujauumba, kwa hakika hilo ni (Jambo)rahisi kwa Mwenye enzi Mungu"
Usije ukasema mbona pametajwa Msiba, nini kinyume cha msiba, ni furaha, na hiyo furaha ni (Nature) yako kama ilivyo afya yako, ndio maana ukatajwa msiba sababu ndio unao kuhuzunisha na kukunyima hiyo furaha, Naam kwa hiyo kila kitu kimeumbwa(Pairs) na kila kitu kishaandikwa kabla ya hapo, hapa itataka uchambuzi kidogo kabla ya kuendelea, najua mshatoa mapanga ya Ulimi kutaka kunijeruhi, kwa hiyo wacha niweke sawa ili tupate kuendelea na darsa hii ya nani atakua Rafiki yako Peponi.
kutaka kuyajua hayo Endelea part 2

No comments:

Post a Comment