Sunday, June 23, 2013

AJABU YA KUSAMEHE PART 1

Asalaam Aleiykum,

Nini Samahani? Kwa Maagizo kutoka kwa Mollah wetu, Msamaha ni Rehma au (Zawadi)maalumu alowapangia waja wake kwa kusema katika Quraan sura ya Zumar aya ya 53.
" قُلۡ يَـٰعِبَادِىَ ٱلَّذِينَ أَسۡرَفُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ لَا تَقۡنَطُواْ مِن رَّحۡمَةِ ٱللَّهِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ جَمِيعًا‌ۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ "
"Sema"Enyi waja wangu mliojidhulumu nafsi zenu, msikate tamaa na Rehma ya Mwenye enzi Mungu, Hakika Mwenye enzi Mungu husamehe dhanbi zote, Hakika yeye ni Mwingi wa Kusamehe (na)Mwingi wa Kurehemu"
Kwa fahamu zetu za Kibinaadamu huwezi kujibu swali la hapo juu mpaka mwanzo ufanye utafiti na upate kujua nini (Kosa)? Kosa ni kitu chochote kinachotendeka baina ya pande mbili,(chengine chochote unachojifanyia mwenyewe kinaitwa Dhuluma)Na nikisema baina ya pande mbili nina maana iwe wewe na Mollah wako au Binaadamu mwenzako. Kwa kuwa leo tunazungumza kusamehe wacha hili neno kosa tuligeuze na kuliita (Dhanbi) dhanbi ni kitendo unachomtendea Mollah wako au Binaadamu mwenzio, kitendo hichi chaweza kuwa kikubwa au kiwe kidogo, kifanyike mchana au usiku, kiwe cha kufurahisha au kukera, kije kwa ubaya au uzuri, madamu ni kosa kitendo hicho hakifutiki au kumalizika mpaka kipate mizani ya Malipo yake, Na hapo ndipo yanapatikana yale maneno ya (Kama ulivokopesha ndivo utakavolipa)Na malipo yapo ya aina mbili, ima Kwa Mwenye enzi Mungu au kwa Binaadamu mwenzako, Kwa Mollah wako utapata msamaha wa aina mbili ama kwa kufidia  na jengine utapata hiyo Rehma ya kusamehewa hayo uliyoyatenda.
Lakini kwa Mwanaadamu mwenzako inatakiwa ipatikane hiyo inayoitwa Samahani(Kusamehewa), lazima akusamehe, ndio tunarejea hapo mwanzoni nini Samahani? Samahani ni kitu chenye uzito wa pekee kwa mwenye kuomba na kuombwa. Katika nafsi ya Mwanaadamu iliyomiliki jambo hilo ni mfano wa Mdai na Mdaiwa, ni kama biashara ambayo mwenye kusamehe ndio anafaidika zaidi, ndio Maana ukathibitishiwa katika (Hadith Sharif)unaambiwa"Rehemu upate kurehemiwa(Sababu Kusamehe ni kitendo cha Rehema)""Samehe upate kusamehewa""Wasamehe walio Ardhini, Apate kukusamehe Aliye mbinguni na Ardhini" Na pia Elewa hakuna Waislam wawili wanokutana wakapeana mikono na kusalimiana ila wakiachana basi Mollah huwa ni Mwenye kuwasamehe (Dhanbi)zao. Enyi Ndugu zangu ajabu ya kusamehe na Rehma zake iko hivyo wanokutana tu wakapeana mikono kwa ajili ya kusalimiana ikisha wakakumbatiana basi hupukutika (Dhanbi)zao kama majani makavu yanavopukutika kutoka katika mti ukipigwa na upepo. Nini Habari yako wewe kama utavaa koti la kusamehe, kutaka kuijua Ajabu hii enedelea Part 2

No comments:

Post a Comment