Asalaam Aleiykum,
Vipi leo wewe uingie kwenye funga ya Ramadhan na kapu la mijidhanmbi, kama nani anokwenda kwa Mpenzi wake ananuka, vipi leo wewe unakwenda kwenye Mwezi Mtukufu umebeba bango Mimi Nishazini, Mimi Nishalewa, Mimi nishadhulumu na sasa nakuja kwako Mollah wangu unisamehe.
Nini Ramadhan? Ramadhan ni Rehma, Ramadhan ni Maghfira(Kusamehewa)Ramadhan ni kuchukuliwa dhamana ya kuepushwa na (Moto) na kuingizwa Peponi, Leo zitizame hasara Mja unazokuja nazo kwenye hiyo (Rehma) ya Mollah wako, kwa ajili ya hilo vunja jungu lako, Kusudio la Rehma hapo mwanzo ni kusafishwa hicho (Kiwiliwili)chako na hiyo (Roho)yako ili viwili hivyo viwe safi, tazama sasa vipi unaanza funga yako ya Ramadhan, jungu ndio ushalivunja kwanza kwa kufanya zinaa, zitizame nini hasara za vunja jungu kwa tendo hilo la zinaa, na inakuaje unaikosa hiyo Ramadhan.
Jambo la mwanzo ukihudhuria kwenye kadhia ya (Uzinifu)inapatikana kutamani, Na ukitamani kuna (Energy)ndani ya Mwili wako inaanza kupanda juu (wewe jichunguze) tena kwa kasi inakwenda kugusa sehemu ya matamanio, na sehemu hiyo ikiguswa kila kitu kinachafuka inachukua (Muda Energy) hii kutulia tena, wataalamu wengine wanasema inachukua mpaka siku(40) ndio ipoe. Sababu kubwa umetamani kitu si chako, na kuna tafauti kabisa pale unapotamani cha halali yako, na mfano wa hayo usijitizame wewe mwenyewe hebu mtizame mwizi anakua na hali gani anapotaka kuiba uone (Energy) yake inavopanda kwa kasi, hujamkuta hata siku moja mwizi asoweza kukimbia, lazima huyo awe ka (Retired) na hivi ndio hali anokua nayo anotaka kutenda tendo la zinaa, Na sehemu hii ya kitivo cha matamanio ikiguswa basi (Roho na Akili) vyote vinaingia tafrani na sababu kubwa viwili hivyo vyote ni majirani, na mambo yakichafuka mwili nao unafatia, na hilo lilikua ni mataarisho tu ya (Vunja Jungu).
Ikisha hizoo Roho mbili kwa maridhiano zimeamua kumuasi Mollah wao, Wameamua kutenda dhanmbi kubwa, wanapomaliza wawili hawa tendo hili la Uzinifu (Energy) hiyoo inashuka chini na kuleta uharibifu wa Kimwili, hapo tena mtu anaanza kuchukia lile tendo, mara anaumwa hichi na kile, huyu anajuta, anaona haya mwezi ushaandama, Hapo tena inakatika Rehma ya Mja huyo anaingia katika misukosuko mwezi mzima wa Ramadhan, anapita kununua madafu mchana anakula usiku(Kutongoza), huna funga, sababu (Energy) yote inotakiwa kwenye (Saum) inapanda na kushuka kama kipimo cha (Homa), vipi wewe utafunga huku mawazo yote yapo katika mawazo machafu, unakumbuka vituko vya vunja jungu, mwenye unajijua huna funga lakini unaendelea kujitesa na Njaa.
Endelea.Part 3
No comments:
Post a Comment