Asalaam Aleiykum,
Wacha sasa tuchungulie katika Rehma hii ya kusamehe ili tupate kujua tunakutana na nini, Kwanza wacha tujikumbushe au kumbuka wewe ulivokua mdogo umetenda kosa na mzee wako kakasirika, hamaki zimemshika, mkanda ushavuliwa au fimbo iko mkononi kwa ajili yako, kumbuka hali ile ulokua nayo, kama wewe (baba)au(Mtoto)sasa rejea ghafla hamaki zimepotea ukaamua kuzungumza na mwanao badala ya kumpiga ukamsamehe,(wewe mtoto)vipi hali mbili hizi zinakua kwako wewe, ile ya kwanza hofu na maradhi matupu(unakua mgonjwa leo ataniua huyu)na ya pili inakua nini ukisamehewa, Afya na Furaha(Rehma)tupu.
Sasa ikiwa hiyo hali anayokua nayo mwenye kusamehewa, Nini habari yetu sisi kwa yule mwenye kusamehe, Tizama wewe ukikosewa kosa kubwa, ikisha akaja mkosaji akakuomba kwa mayoe na vilio umsamehe, na wewe ukamridhia moyoni na kweli ukamsamehe, nini kinatokezea, jambo la mwanzo kutokezea inakuhudhuria Sahau(Kusahau)na sahau ikikuvaa Rehma inawasili, na Rehma ndio hiyo Afya, ndio furaha, ndio maana ukizama kwenye mchezo wa (senema)hukumbuki chochote, lakini hebu jitizame ukenda msibani kutoa pole unakuaje, maneno ya kumbukumbu matupu yanakutoka, jana tumeongea, mbona aliniaga, alinipigia simu, alikua hata haumwi,ilikua nini kafa ghafla, sababu hutaki kukubali kuwa kesha kufa kwa wakati ule ndio maana umeshikilia jana hivi, jana vile, Unaishi ndani ya (Memory)na hali kama hiyo ndio unayoishi nayo kama utakua si mja mwenye kusamehe.
Ama mwenye kusamehe yeye anapata ishara zote za kuelekea kwenye Ucha Mungu, kwani kusamehe ni Upole, kusamehe ni Imani, na huko kusamehe ni Huruma, basi sifa hizo zote hazikutoshi wewe kukoga kwenye mvua ya Rehma ya Mollah wako, Jitahidi kujizoesha kusamehe, kama (Mke au Mume)kakusoea mara kumi, wewe mshamehe mara kumi na moja, Muunguze kwa moyo wa samahani mpaka awe kama wewe anaishi kwenye (Kasri lako la Msamaha)tena mwambie humu ndani natanguliza samahani kabla hujanikosea, Ikiwa umegombana na Ndugu zako basi anza leo zoezi hili la kusamehe kwanza kwenye moyo wako, na wao kwa Rehma za Mollah wako wataanza kukusamehe kwenye Nyoyo zao, Kama umekoseana au Wazee wako mekorofishana na mpaka leo hamzungumzi, fanya hima wasamehe na watumie Rehma za msamaha ziwafikie kwa walilolifanya, ikisha toka kawaombe wewe Msamaha uone vipi Rehma ifanyavo kazi yake, mpige (Shetani)kwa fimbo ya Rehma, uone miujiza yake.
Ikiwa Marafiki zako wamekukosea kumbuka ufunguo wa furaha unao mwenyewe, kama utachagua kuwasamehe hiyo ni Furaha yako(Rehma)au kama utaamua kubaki na dhiki ya Moyo hutaki kusamehe hilo pia ni chaguo lako, hakuna awezaye kukufanya ufurahi isipokua wewe mwenyewe. Ipate ajabu ya kusamehe kwanza kwa kusamehe wewe, na pia napenda uelewe makosa mengi ya Wanaadamu yanatendwa na Ulimi, kwa hiyo usikubali wewe kutiwa katika (Gereza)la Ulimi, ikawa huzungumzi na mwenzio sababu kasema,(Kumbuka:Ulimi umeumbwa na mate:kuteleza kazi yake)usikubali kukaa mahabusu mwaka mzima kisa sauti iloambatana na upepo imevuma kinyume na matakwa yako, maneno yasikutie maradhi ya kinyongo, kumbuka hayana uzito na yanaishi kwenye Akili kwa muda mchache tu, anobaki kusumbuka ni wewe, lisikunyime Raha kosa ukawa unaishi na maradhi, jitoe jela kwa kufanya jambo moja tu, nalo hili la kusamehe, Samehe upate kusamehewa, Samehe upate kurehemewa, Samehe upate kuingia kwenye Furaha, na hiyo ndio Ajabu ya kusamehe:Mollah wetu tujaalie zawadi hii ya uwezo wa kusamehe, tupe faraja za kusamehe wenzetu kama wewe unavo tusamehe sisi yote tunayo kukosea.Amin
No comments:
Post a Comment