Sunday, June 23, 2013

AJABU YA KUSAMEHE PART 2

Asalaam Aleiykum,

Samehe upate kurehemiwa, Nini Kurehemewa?
Unaijua nini Rehema, Rehma ni bahari kubwa ambayo hatuwezi kuikoga kwa uchambuzi, ila nitakupa mifano midogo ya Rehma ile nipate kukuzindua, hiyo Rehma ni huko kuvuta pumzi kwako, kulala kwako, kuzungumza kwako, Afya yako ulonayo, zote hizo ni sehemu katika bahari ya Rehma, hiyo ndio Rahman yenye sifa ya kuonekana na kufichikana, Na kwanini isiwe hivyo wakati mkisalimiana kwa furaha (Dhanbi)zenu zinapukutika kwa (Msamaha). Nini habari yako wewe Ukiamua kusamehe, Ukisamehe unakua ushavaa vazi la (Huruma) na ukivaa vazi la huruma unakua ushajiweka tayari na wewe (Kurehemewa)na Mollah wako, Na Mwenye enzi Mungu akikuona kama kweli umesamehe kwenye Nafsi yako basi hukuteremshia Rehma kwenye Maisha yako, kama una Maradhi bado yamo ndani hayajatokeza basi anakuponesha pasi mwenyewe kujua, kama una donge kifuani ukisamehe linaondoka, kama una dhiki unaipata Faraja, kuna wengine wanapewa Utajiri kwa ajili ya kusamehe tu, hizo ndizo Rehma za Mollah wako kwa Mja mwenye kusamehe.
Pia napenda Ufahamu Kusamehe ni Afya, na Kisasi ni Maradhi, kisasi ni jambo la kudumu, na kama hujakilipa kinakusugua sana katika Maisha yako, ndio maana ikaambiwa katika sura ya Maidah aya ya 45 inapoanzia na kumalizikia kwa maelezo yake kuna kitu Adhimu nacho ni maneno haya" فَمَن تَصَدَّقَ بِهِۦ فَهُوَ ڪَفَّارَةٌ۬ لَّهُ"
"Lakini Mwenye kusamehe basi itakua kafara kwake".
Kwanini iwe kafara, sababu ujifungue na kisasi, sababu kutokusamehe ni hali ya kukumbuka, na wewe kumbukumbu yako (Memory)yako ni ndogo sana, na ili uishi kwa furaha(Rehma) imejengeka kwa hali ya ushaulivu, ndio maana ukapewa uwezo finyu wa kukumbuka, jiangalie wewe mambo mangapi unaweza kuyakumbuka kwa siku, mengi yanatokezea lakini hukumbuki hata moja, na ikipita siku ulotenda jana yote ushasahau hiyo ndio kawaida yako, sasa ukikaa na jambo au kisasi au kutosamehe inabidi uitumie sehemu ya kumbukumbu yako kwa ajili ya kuifuga hali hiyo, na kama jambo la kukuumiza ndio linaendelea kukudhuru, na kama umedhulumiwa sasa unaendelea kujidhulumu, basi kwanini uteseke na uwezo wa kutoa kafara unao, tena sio bure na wewe utalipwa kwa kafara hiyo, nayo ni hiyo Rehma.
Vipi Utasamehe?
Kusamehe ni ushujaa, ni jambo lisilotendwa na wanaadamu wengi na wewe ukipata nguvu za kuweza kusamehe basi umepata kitu kikubwa sana, usije ukakiachia utakua hasarani, na kusamehe kunatakiwa ukumbuke kitu kimoja tu nacho ni hiyo (Rehma).
Kumbuka alo kukera au kukudhulumu hata yule alo kujeruhi, huyo amekuletea Biashara ya Rehma, Lakini wapi, wewe umezoea Biashara ya (Nipe nikupe)umetoa gari upewe pesa, umetowa nyumba upewe pesa, vipi leo upigwe kibao ukubaliane na habari ya useme ahsante, wewe ukipigwa kibao basi kama kuna Jabali utamtandika yule alokupiga kibao, unataka aumie kushinda kile kibao alichokupiga, Unajua kwanini ikawa hivyo, Sababu Shetani wakati ule ghafla anakusahaulisha Rehma na kukumbusha Heshima, ndio kanikumuta kibao mbele za watu, watu watasemaje, hiyo ya kwanza kwenye akili, halafu yanafatia machungu kwenye  shavu, sasa yatizame malipo yako yanakuaje, hapo ndipo unaweza kumuua mbu kwa kutumia Rungu sio kofi tena. Sasa endelea kuitizama Ajabu ya kusamehe na Rehma zake. Part 3

No comments:

Post a Comment