Sunday, June 9, 2013

KISIWA CHA WACHA MUNGU PART 1

Asalaam Aleiykum,

Kinapotajwa kisiwa lazima mtu awe makini kuangalia ni kisiwa gani kilokusudiwa, chaweza kuwa kisiwa cha Unguja au Lamu, chaweza kuwa Pemba au Mafia, chochote au vyote katika hivyo kulikuwepo na bado wapo Wacha Mungu na mpaka hii leo wanaendelea na maisha yao Salama Usalimini, huku wakiendelea kufanya Ibada zao , hapa leo nawazungumza wale wa zama zile zilopita walotajwa katika vitabu vya karne za nyuma, na mfano ni mfano, waweza kuwa mfano ukakugusa ili upate kuzinduka, alaa kumbe kilicho kusudiwa ni kisiwa changu, na la pili kumbuka yaweza kisiwa hiki kipo ndani Moyoni au nje Ardhini wewe ndio utakua Hakimu wa uamuzi wa jambo hilo.
Pahala popote pakifanywa Ibada Mollah huteremsha baraka zake na Rehma zake ikawa hata wale watu wanoishi pale ni maskini lakini huteremshiwa Baraka za kila aina na mapenzi ya furaha yasiyo mfano, na yoyote mwenye kuishi katika Kisiwa cha Wacha Mungu huwa anahisi labda (yupo kwenye pepo ya Ulimwengu|)hujiwa na kila kitu, kuanzia chakula na mahitajio yote Mwenye enzi Mungu ana hakikisha waja wake wanatimiziwa, kutokana na (Special Energy)ya Ibada katika kisiwa hicho, basi huvutiwa watu wa Ulimwengu wote kukizuru kisiwa hicho, hapo huendelea kuzaliwa Wacha Mungu na wenye Hekima na Wasomi kadhalika, yanatokezea mapenzi katika Kisiwa cha Wacha Mungu watu wote wakawa wanaonana kila mmoja ndugu wa mwenzie.
Kama ilivyo desturi ya popote pale penye kizuri lazima kando kando pawepo Kibaya, hiyo ndio sheria ya Ulimwengu huu.
Wakapata habari wenyeji wa kando kando kuhusu mazuri na (Ibadah)zinofanyika Kisiwani huko, Kumbuka nimesema(Kando Kando)sio pembezoni (Hapo fanya tafsiri mwenyewe)mwa Bahari, waliposikia habari hii, wakafanya safari ya kukitembela kisiwa hiki wale wenyeji wa kando kando, na kwa bahati walipofika Kisiwani hapo watu wa mwanzo walokutana nao ni Wacha Mungu watatu wakifanya (Ibadah zao),waliwakuta wanaitegemea (Laaillah-illah-Allah)katika kila jambo lao wanalosema na kufanya basi hutanguliza neno hili, wakacheka sana wale wenyeji wa kando kando, vipi nyinyi kila (Ibadah)zenu mnataja neno hili yaonesha hamjui (Ibadah)au hata kama mnajua lakini hivi mfanyavo sivo, Wale Wacha Mungu wakauliza tuelekezeni vipi tufanye, kwani nyie mnaabudu vipi, kuna njia nyengine mnafanya kumridhisha Mollah wenu, pengine mmetuzidi daraja wenzetu, tunaomba tuelimisheni, wale wenyeji wa kando kando wakafahamisha vipi kufanya (Ibadah) ikisha hao wakachukua (Mashua au Ngarawa)wakaanza kuondoka kurejea katika mji wa Kando, walipofika masafa ya maili kadhaa wanageuka nyuma wanaona wale Wacha Mungu wanakuja mbio juu ya maji wanawakimbilia, walipofika karibu wakawaambia tumeghafilika yale maneno yametupotea, hebu tuelekezeni tena yanatamkwa vipi,Ikawafika hofu wenyeji wa kando kando huku wanatetemeka  wakawaambia nendeni kasomeni kama mwanzo mlivokua mnasoma, dua zetu, masomo yetu hata siku moja hatujawahi kusimama kwenye Bahari namna hii, vipi leo tutakufundisheni nyinyi, Rudini na tusameheni.
Walipo rudi kwenye mji wao wale wenyeji wa kando kando wakapanga mpango wa kukihujumu kile kisiwa, kuwachafulia mwenendo na desturi zao, sababu kubwa kinatishia Usalama wa dini zao na mila zao huenda wakawafanya watu wao pia wakawa Wacha Mungu, mpaka hii leo kimechafuka kisiwa hichi na ile (Special Energy)yote ya Ibadah imetoweka, pahala palipokuwa na Wacha Mungu wakubwa wakubwa, wakizaliwa watu na Hekima zao na Elimu zao, leo kisiwa hiki kimerejeshwa kuwa hali ya chini kabisa, mpaka imefikia wakati sasa wao ndio  wanasomeshwa Ucha Mungu. 

Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment