Asalaam Aleiykum,
Imeshakufikia ndani ya Moyo wako habari unayoikataa na kuipinga siku zote ya Maisha ya Inshaa Allah, Jee unajua Maisha haya yakoje? Wewe Mwenyewe umeshawahi kuyaishi maisha haya? Na vilevile unataka kuwajua kina Nani wanoishi maisha hayo hivi sasa?, Hayo ndio maswali tutayojiuliza katika Darsa yetu ya leo ili tuupate ufunguo wa kuingia katika hii Nyumba ya (Maisha ya Inshaa Allah).
Kwanza kabisa tujiulize nini maana ya Inshaa Allah, kwa Tafsiri nyepesi(Mwenye enzi Mungu akitaka), Kwa Lugha ya Tawhid itakua vigumu kwa sisi kufahamu kusudio lake mpaka uwe umeshiba Tawhid ya Mollah wako, umeshafunguliwa katika Ubongo maarifa ya (Mystic)na kuona mambo kwa upeo mwengine ambao umefichika kwa watu wakawaida, Na kwanini twende kwenye ugumu wakati wepesi upo, basi tuanzie hapa katika kiwanja cha wepesi na kujiuliza nini Inshaa Allah?
Inshaa Allah ni (Trust)kwa ufupi, au kwa mzunguko mwengine wa kilugha ni Imani, lakini Imani yenyewe ni tafauti na ile ya kutamka Ulimini, Imani hii ni ya kujikabidhi kikamilifu kwa Mollah wako, ikawa huna pingamizi kwa chochote kile kinachotokea katika Ulimwengu huu.
Leo nakupa kioo ujitizame uzuri hiyo sifa unayojipa ya Ucha Mungu, uingalie vizuri kama kweli ipo japo chembe katika moyo wako, Sababu nimesema hivyo sio kukuvunja Moyo ila nia yangu nataka nikufungulie muono zaidi ili upate kuwasili katika huo Ucha Mungu, Na hakuna njia nyepesi ya kuwasili kwenye Ucha Mungu kama hii ya kuishi Maisha ya Inshaa Allah, Lakini maisha yenyewe ni vigumu sana kuyapata, na wanoishi maisha haya ni wachache sana na ni watu pekee wenye furaha katika Ulimwengu huu.
Kwanini wakawa hivyo? Sababu kubwa Wameamini na kukabidhi kwa Ujumla Maisha yao kwa Mollah wao Muumba, Na ukipokelewa na aliyekuumba, unakua umerudi Nyumbani na anaye rudi Nyumbani huwa hana matatizo katika Ulimwengu huu. Sasa na wewe unahamu ujulishwe njia za kuweza kuishi hayo maisha, nini unatakiwa ufanye, na wapi uanzie.
Kuishi Maisha hayo ya Inshaa Allah ni kuitegemea ile nguzo ya sita yenye kuzishika zote, na ukiijenga nguzo hii ikawa madhubuti basi una uhakika Nyumba yako haitoanguka hata kama utatokea mtetemeko wa Imani, Hakuna pakupata maisha hayo isipokua kujitupa na kujifunga katika nguzo hii ya (Qadir)kadar, Kuamini ya kwamba mimi nimo katika hili(Spaceship)Dunia, Mimi nazunguka nayo (Ardhi)hii hata nikifanikiwa kuchupa nikimbie, basi nitaangukia katika Mbingu zako ya Subhanna, Basi kwa kuyajua hayo sasa najijua na mimi vilevile umeniumba kutokana na Ardhi hii, na kuna siku utanirejesha tena ndani ya Ardhi hii, na pale utaporidhia wewe Mollah wangu mimi ninayo tamaa na uhakika utanirejesha tena katika Ulimwengu huu kwa ajili ya kunihukumu.
Sasa ikiwa nina yakini na hayo, nini habari yangu mimi, na kwanini siwezi au sitaki kuishi maisha haya ya Inshaa Allah, Mbona nimekua Jeuri nanyanyasa wenzangu, Mbona kiburi kimenizidi, nini hasa kinacho nifanya niteseke, nikiwa Maskini nateseka, nikiwa Tajiri nateseka nini tatizo langu. Kutaka kujua Tatizo lako ENDELEA PART 2
No comments:
Post a Comment