Sunday, June 30, 2013

HASARA YA VUNJA JUNGU PART 1

Asalaam Aleiykum,

Unamjua anayepata hasara bila ya kujijua? yule Mwenye kujiita Muumin halafu unapokaribia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan anaukaribisha kwa (Party na Picnic). Huyo anafanya Sherehe za kumuaga Rafiki yake (Shetani)na kumpa ahadi nisubiri Yaumu shaka tutakutana tena bila ya wasiwasi, Huku Mwenye enzi Mungu anawaita waja wake kwa Mapenzi akisema "Ewe kiumbe wangu wee" njoo ukiwa msafi, anza kujisafisha, njoo ukiwa (Tohara) ili uzifanye hizi siku chache ziwe za utiifu kwa ajili yangu, uje ufanye mambo ya (Taqwa), Wewe Unamjibu ngoja nijichafue zaidi, nipe muda nitie Najis katika Kiwiliwili changu, Niwache nije kwako huku nina kumbukumbu za Rafiki yangu Shetani, mimi katika huo mwezi wako Nakuja Shingo upande, ndio imenibidi tu sababu watu wote wananijua mimi Muislam, lakini kwa uhakika mapenzi yangu yote yapo kwa Shetani na hiyo miezi kumi na mmoja ilobaki, Najua Mollah wangu wewe umenipa Uhai, ikisha Wewe ndio Unanipa Riziki na kila kitu ninacho hitaji lakini mie niache sijiwezi kwa shughuli za (Vunja Jungu).
Enyi "Wanaadamu" hususan nyinyi Waumin hamjikumbushi wakati mtakapo ulizwa kwani hamkusoma Quraan sura ya Yaasin aya ya 60,

"أَلَمۡ أَعۡهَدۡ إِلَيۡكُمۡ يَـٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعۡبُدُواْ ٱلشَّيۡطَـٰنَ‌ۖ إِنَّهُ ۥ لَكُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬"
Jee sikukuagizeni Enyi Wanaadamu kuwa msimuabudu Shetani, Hakika yeye ni adui aliye dhahiri(Wazi)kwenu.
Na mmekua hamtaki kusikia ila lazima mvunje Jungu, lazima msondo upigwe, tena kuna watu ikikolea wanasema bila ya kulewa ntaichezaje, (Maskini)hawa hawajalewa wako hali hiyo, nini taarifa zetu tunazopokea yanofanyika katika hilo Vunja Jungu. Hakuna hadith za huko isipokua Maasi, halafu huku unasema unajiandaa kufanya (Taqwa) lakini kwa kupitia njia ya Maasi, Iwapi Ramadhan yako wewe mvunja Jungu, Hana Ramadhan yoyote yule mwenye kufanya maasi katika hili kumi la mwisho la Shaaban(sababu zake utakutana nazo huko mbele). Mfano wa kwanza kabisa kitizame chakula kinavofanya kazi kwenye (System)ya (Tumbo)lako kwanza kinakaa siku nzima kwenye (Utumbo) halafu kinachujwa na (Parcent)kubwa inakwenda kwenye Akili, na bado hujui kwenye Akili kinakaa muda gani, Sasa jiulize Pombe nayo inakaa muda gani, pia kumbuka kuna muda wa vitu kukaa katika hiyo (Body System)yako, kuna vya siku saba na vyengine kumi na nne, na vyengine mpaka siku arobaini havitoki katika kiwiliwili chako, vipi leo Mvunja Jungu useme unaipata Ramadhan.
Huna Ramadhan kwa kunywa Pombe kesho Ramadhan, Huna Ramadhan kwa kunuwiya kula haramu kwa kuwapandishia Waumin bei za Chakula, huna Ramadhan kwa kucheza viuno kwenye Taraab au kutembea Uchi nk, vipi wewe utaipata Ramadhan. Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment