Sunday, June 30, 2013

HASARA YA VUNJA JUNGU PART 3

Asalaam Aleiykum,

Ikiwa hiyo ndio hali anayobakia nayo mzinifu, nini hali za wenye kunywa ulevi, wale wenye kuvuta bangi na mirungi siku ya vunja jungu, na wao hali kadhalika wanabakiwa na mabaki ya pombe na mirungi kwenye (Body) Miili yao, na hakuna anayepata Rehma ya (Saum-Funga) kabisa. Na hata kama wakifunga basi ni bure ni sawa kujitesa na njaa, na kama ukibisha hayo hebu Muulizeni mgonjwa wa sukari eti kweli (Doctor) wanajua kiwango cha sukari ulokula miezi mitatu ilopita, akipimwa damu taarifa zote zimo anaambiwa ulikua ukiipiga vijiko vingapi kwa siku, ikiwa bado unapinga kaulize vipi anayekufa kwa ulevi akipimwa baada ya mwezi mzima wanakwambia aliuchapa chupa ngapi, na wanasayansi hawakuishia hapo sasa wamevumbua (Chemical)fulani wakikutia kwenye ngozi wanakwambia (Gomba au Bangi) umevuta wiki ya jana au umekula wiki mbili zilizopita, (Puri)ulovuta bado inaonesha kwenye damu na  hivyo ndio Mwenye enzi Mungu anavodhihirisha mambo yake mpate kujua kila mnalotenda linabakia (Rekodi) zake kwenye (Mwili) wako, sasa jiulize kwa hali hii ya Kuvunja Jungu kila ufisadi unabakia jee Funga ninayo?
Na wale wenye kuvunja jungu kwa (Party au Taarab) wao ndio wanapigwa picha kabisa na ushahidi upo na kama watabisha basi wataambiwa subirini, "Yaasin 65"
"ٱلۡيَوۡمَ نَخۡتِمُ عَلَىٰٓ أَفۡوَٲهِهِمۡ وَتُكَلِّمُنَآ أَيۡدِيہِمۡ وَتَشۡہَدُ أَرۡجُلُهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ "
siku hiyo tutaifunga midomo yao, na itazungumza (na sisi)mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa yale waliyokua wakiyachuma.
Mimi wakati navunja jungu nilikua nainua mikono juu natamba kukuasi Mollah wangu, Na miguu nayo itashuhudia kweli mimi nilikua nanyanyua visigino halafu nakatika viuno ili nipate kuwachafua waja wako Akili zao, ili wapate kukuasi wewe Mollah wangu, Huingia viumbe hawa katika Mwezi wako Mtukufu hawana (Taqwa) wala si wasafi mwezi mzima mawazo yao yamo kwenye hadith za vunja jungu.
Hizo ndio hasara za vunja jungu, ikisha siku ya Qiyama mkiamrishwa kwenda Motoni mtaanza kushangaa pembezoni mwa Shimo la (Jahannam) mnasema mbona tulikua tukifunga, wataamrishwa Malaika wasukumeni, watakukamateni visogoni kabla ya kukusukumeni watakuulizeni maneno haya"Sura ya Mulk aya ya 8 na 9.
"تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلۡغَيۡظِ‌ۖ كُلَّمَآ أُلۡقِىَ فِيہَا فَوۡجٌ۬ سَأَلَهُمۡ خَزَنَتُہَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَذِيرٌ۬"
Unakaribia kupasuka kwa hasira, kila mara litakapotupwa(Shimoni)humo kundi(La wabaya)walinzi wake (Malaika)watawauliza jee hakukufikieni(Nyinyi) muonyaji.

"قَالُواْ بَلَىٰ قَدۡ جَآءَنَا نَذِيرٌ۬ فَكَذَّبۡنَا وَقُلۡنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَىۡءٍ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا فِى ضَلَـٰلٍ۬ كَبِيرٍ۬ "
Watasema kwanini, alitujia Muonyaji, lakini tulikadhibisha na tulisema, Mwenye enzi Mungu hakuteremsha chochote, nyinyi mko katika upotofu mkubwa.
Tulifikia hata kusoma hasara za Vunja jungu, lakini tulikua tunajipa tamaa hakuna chochote, tunatishana tu mambo ya kutiana woga, lakini kwa wale walozinduka basi usilivunje jungu, bali wewe lijenge ulitie saruji liwe madhubuti kwa kusoma Quraan kwa wingi, kwa kuzidisha sala za sunna na kumsabahi na kumkumbuka Mollah wako kuanzia sasa na nakupa muongoz ukifanya hivyo Ramadhan yako safari hii itakua ya namna nyengine kabisa.
Namuomba Mollah wetu atuepushe na Maasi, atupe (Taqwa) na mapenzi yake, atupe afya tuweze kusimamisha nguzo hii na nyengine kwa ajili yake. Amin

1 comment:

  1. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na kufanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi ili kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito ili kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    . kutokuwa na uhakika wa ubaba au ubaba usio na sifa

    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete