Asalaam Aleiykum,
Jee unataka kujua wewe kundi gani?, Na pia unataka kuelewa ukiwemo kwenye hilo kundi nini kitakufika? Basi hudhuria darsa hii kwa uangalifu mkubwa ili upate kuchagua kundi lako kwa busara. Huna huja ya kusubiri Kiyama au mpaka ufike kaburini, hapahapa Ulimwenguni utajijua mimi ni mtu wa kundi fulani, Na katika hayo makundi yapo ya aina tatu lakini mimi leo nitayazungumza mawili lile la mwanzo la hasara, na lile la pili kundi la kheri.
Kazi yangu mimi ni kukueleza kwanini upo katika kundi fulani na kwa sababu gani, Kitu cha mwanzo unachotakiwa ukifahamu kwamba huu Uhai wako wote ni mtihani, Na hakuna mtihani mkubwa Mwanaadamu unao mshinda kama kusahau, Madhara makubwa sana yanapatikana katika kipindi hichi cha kusahau,Dhanbi zote zinafanyika katika kipindi hicho, Shida zote zipo hapo kwenye kusahau, lau Wanaadamu tungepata theluthi moja ya kukumbuka, basi ungekua wewe Walii, wewe Mcha Mungu, lakini kinyume na hivyo kundi lako litakua la balaa tupu. Na ikiwa utajikuta umo katika kundi baya basi fanya jitihada ukurupuke utoke mbio, na kama umo kwenye kundi la kheri zidi kujipigilia misumari usije ukachomoka.
Sasa kwanza acha tuingie katika kundi la hasara, Kundi la adhabu, kundi la mateso ambalo limewafunika waja kwa moshi mkubwa wa moto wa shetani, Na ndani ya kundi hili yaweza kuwa umo mwanzoni au katikati au umezama kabisa huonekani hata kichwa. Katika kundi hili la hasara limegubikwa na Matendo ya kusahau ambayo yanapambwa na Vitendo vya Shetani kama alivoahidi mwenyewe( Sad aya ya 82)قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغۡوِيَنَّهُمۡ أَجۡمَعِينَ
"Akasema Naapa kwa haki ya utukufu wako, Nitawapoteza wote"
Sasa vitendo vipi Shetani anakuingia mpaka kukupoteza, ni huko kusahau, anakuondoshea kukumbuka Ufalme wa Mwenye enzi Mungu, na ukisahau Ufalme huo unaingia hasarani, Hapa inabidi kabla sijavitaja vitendo vyenyewe mnipe nafasi nifafanue kidogo, Naomba kukumbusha hujakatazwa kuishi, sio kila kitu haramu, Maisha sio uteseke, ila kinachokutia hasarani ni kitendo cha kusahau, na jambo la mwanzo katika matendo nitayoyataja utashangaa kwamba si chengine ila Taji la Pesa, Pesa ndio Baba la ushaulivu, Penye pesa Mungu hakai kabisa, penye pesa anakaa shetani na kiburi chake, Pesa ni msukosuko, lakini cha ajabu sote tunafukuzia kundi la pesa, Jee wewe kundi gani? Hili la cheo na umaarufu, Hili la (Power and Security)Hili la kunyanyasa na kuwadharau viumbe wenzio, basi ikiwa ndio hivyo fanya haraka iwezekano umlainishe ngamia wako mifupa kwani itakua tabu kubwa kupita kwenye tundu ya shindano lazima utakwama kichwa(1).
La pili(2)Linalo tusahaulisha Ufalme wa Mwenye enzi Mungu ni Matamanio(Sex), hapa tena tukifika mtu ndio hukumbuki chochote, ndio tunalala kabisa, wewe jitizame ukiwa na mpenzi wako unamkumbuka Mollah wako, Hili la (sex) lina visa chungu nzima ndio linakupofua kabisa, na kama utatajiwa mambo ya akhera wakati huo unaweza kumnasa kibao mtu anakuharibia mambo yako ya starehe, inawezekana hapo kuna watu mia mbili wanakuangalia wewe, ukaambiwa watu wanakuona, ukageuka nakujibu wote hawanioni, hao wanadhani tu, na fanya uchunguzi utaona mambo yako yote unafanya kwa ajili ya hayo matamanio, hisani zote nyuma yake imejificha (Sex) chunguza utapata jawabu la jambo hilo.
Na Jambo la(3)Kutusahaulisha ni Macho, haya ndio hatari tupu, Mimi hapa nataja mambo katika maelfu ya majambo ili nitoe mwanga wa kusahau, Basi hata wewe Macho unanisahaulisha mimi, Ndio, kupitia kwangu ndio unaona Ulimwengu, mimi ndiye ninayekuonesha mipira na senema, Ngoma Na manyama nyama yanotingishika, vipi leo wewe utaweza kumkumbuka Mollah wako.
Jambo la (4)Mdomo mimi ndio (Chifu) wa mazungumzo, mimi ndio nasababisha unazungumza mambo yote ya watu ya kweli na ya uongo, vipi uwe katika vikao na ukaweza kumkumbuka Mollah wako.
Na la (5)Ni hilo shikio, kwanini likaitwa shikio, kwa sababu linashika habari za kila mtu, linasikiliza muziki wote, hili ndilo linalo kusahaulisha kwa utamu (wa ngoma kucheza ukizunguka raha zimezidi)za kumsahau Mollah wako, na takriban kuna mambo mengi ila mimi nimeyataja haya machache makubwa ili nikujulishe mimi na wewe tumo kundi gani. Na kazi yangu mimi na yako ni kufanya jitihada za kuweza kutoka katika kundi hili la hasara, kama alivokumbusha Mwenye enzi Mungu katika sura ya Mujaddilah aya ya 19ٱسۡتَحۡوَذَ عَلَيۡهِمُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ فَأَنسَٮٰهُمۡ ذِكۡرَ ٱللَّهِۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ حِزۡبُ ٱلشَّيۡطَـٰنِۚ أَلَآ إِنَّ حِزۡبَ ٱلشَّيۡطَـٰنِ هُمُ ٱلۡخَـٰسِرُونَ
"Amewatalia Shetani , Akawasahaulisha kumkumbuka Mwenye enzi Mungu, Hao ndio kundi la Shetani, Sikilizeni kwa hakika kundi la Shetani ndilo lenye Kuhasirika(Limo Hasarani)"
Ama kuhusu kundi la pili Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment