Asalaam Aleiykum,
Katika Ulimwengu wa Elimu zipo za aina mbili, ya kwanza ni hii ya Dhahiri, na ya pili ni ile ya siri ilofichika ambayo leo tunaingia japo kidogo tupate kuchungulia tujue faida mbili tatu ambazo zitaweza kutujulisha mambo ya upande wa pili katika hiyo elimu isiyo onekana, Twende tukapajue pahala panapotokea hiyo siri.
Nitaanza darsa yetu ya leo kwa msemo wa hekima ulo maarufu unaosema hivi"(KAVUNJA UKUTA WA WATU KWA HARUFU YA CHAKULA KITAMU)"
Msemo huu kwa nje unaonekana ni wa kawaida lakini ukizama ndani ya maana ya maneno haya utakutana na Siri kubwa ilofichika ndani ya Ukuta huo.(Kavunja Ukuta wa Watu) tujiulize kwanini akavunja?. Inaonesha labda hajui Mlango ulipo, Na hivi ndivo sote tulivo, hatujui mlango uwapi na kila mtu anapita akivunja ukuta wa mwenzie bila ya faida yoyote.
Sasa Ukuta kwani una siri gani? Ukitaka kujua siri ya Ukuta kihudhurie kisa cha Msemezwa na Mwenye enzi Mungu Nabii Musa a.s na yule Mja alopewa elimu na Mollah wake kwa jina anaitwa Al Khidhir, Kisa chenyewe kilianzia pale walipofika katika mji wakaomba wapewe chakula na wale watu wa ule mji wakakataa, Ndipo Al Khidhir alipoukuta Ukuta unataka kuanguka akaujenga, Na Nabii Musa a.s akamwambia kwanini umeujenga, Al Khidhir akamjibu.
وَأَمَّا ٱلۡجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَـٰمَيۡنِ يَتِيمَيۡنِ فِى ٱلۡمَدِينَةِ وَكَانَ تَحۡتَهُ ۥ كَنزٌ۬ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَـٰلِحً۬ا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبۡلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسۡتَخۡرِجَا كَنزَهُمَا رَحۡمَةً۬ مِّن رَّبِّكَۚ
"Na ama(ule)Ukuta, Ulikuwa wa watoto wawili mayatima katika huo mji, Na chini yake(Ya Ukuta)kulikuwa na Hazina yao, Na Baba yao alikuwa (Mtu)mwema, kwa hivyo Mollah wako alitaka wafikie baleghe yao (Ili)wajitolee hazina yao, Hiyo ni Rehma inayotoka kwa Mollah wako" Mpaka inapomalizikia aya.
Naam hizo ndizo habari ya siri za Ukuta, Ukuta ni wenye kuficha Siri na Hazina za kila aina, Sasa huo wa kwenye Quraan ulikua ndio unaanguka ukajengwa, lakini kinyume na Ukuta wetu kenda mtu kuuvunja makusudi, Na sababu yake kubwa kuvunjwa ukuta huu ni hiyo harufu.
Nini Harufu? Nipeni nafasi nifanye ufafanuzi mdogo wa harufu ili tujue Harufu ina mahusiano gani na (Siri ndani ya Siri)pata faida hii uitie kibindoni iwe manufaa kwako. Harufu kwa upande wa sayansi inapatikana kwenye pua na lazima ipatikane(molecules)kutoka katika hicho kitu ili upate kunusa hiyo harufu, lakini upande wetu wa (Mystic)katika fani ya Dini tunatambua harufu inatokea kulekule inapopatikana hizo (Senses)tano kubwa ikiwemo na kunusa, zipo za ziada lakini leo tutazitaja hizi tano ili kufupisha uchambuzi, nazo ni (Kuona, Kusikia, Kunusa, Kugusa na Kuhisi) yote hayo yanamilikiwa na hiyo Siri, Na hiyo Siri inakaa kwenye huo Mwili lakini cha ajabu haigusani na huo Mwili(Siri ndani ya Siri) Na kwenye hiyo siri ndipo inapopatikana Harufu, Na hiyo harufu yenyewe inaendelea kuwa siri, Mwana sayansi anaweza kulikamata Ua akatwambia kuna kitu kinatoka katika hilo ua kinaitwa (esters)kinatokea kwenye Ua ukimuuliza afafanue hajui ni kitu gani, au akujibu nini,ila atakwambia livamie upate (DNA)zake, lakini utapata (DNA)huwezi kupata harufu na hiyo ndio haja yako, kwa hiyo Utavunja ukuta wake lakini hupati harufu yake, Sasa ufanye nini kuijua hiyo harufu? Endelea part 2
No comments:
Post a Comment