Asalaam Aleiykum,
Kwanini utulivu haupatikani kwa sababu huna Imani, Na kama Imani haipo ndio utaona kila ukianza Ibada huyoo unatoka arijojo hurejei mpaka pale Ibada inapotaka kwisha, Sasa hii aina ya Pili ni ya Kutamka iwe taratibu au kwa sauti, hii kidogo ni Rahisi nikisema rahisi nina maana kama utaifanyia mazoezi labda unaweza kuipata hiyo Imani kwa kutumia njia hii ya kukumbuka Majina ya Mwenye enzi Mungu, Na majina hivyo hivyo yako mengine ni magumu kujihusisha nayo kwa njia ya kukumbuka, mie nimekuchagulieni jina hili la Rahisi pengine mtu anaweza kulizoea nalo ni kalima ya Tawhid(Laa Illa Illah Allah) Lifanyie mazoezi ya kulitaja na kulikumbuka Jina hili japo kwa siku nzima uone faida zake, na ukiweza kufanya kwa miezi mitatu utaona faida zake kubwa kubwa zinazopatikana katika jina hili la Mollah wako.
Nini Kinatokea?
Ukiweza kufanya moja katika mawili hayo nilokueleza utaanza kuona Utulivu unakushukia katika Moyo wako, Na huo Utulivu ukija unafatana na hiyo Imani,Na kwa ajili gani ukaja huo utulivu, kwa sababu Fikra zako haziwezi kumudu mambo mawili, Fikra zako zina (Focus)katika jambo moja tu, kwa hiyo Unapo mkumbuka Mollah wako una (Block) vyengine vyote, na ukivizuia hivyo vyengine ndipo unapata huo Utulivu, Na utulivu ukija unageuka na kuwa Imani, Na Ukiipata Imani unakua ushafanikiwa, watu wanaweza kuchukua utu wako, wanaweza kuchukua heshima yako, wanaweza kuchukua cheo chako na mali yako, Lakini kitu kimoja hawawezi kukichukua ni hiyo Imani yako Adhimu uliyonayo. Na huo utulivu unatokea vipi, kihudhurie kisa hiki cha Mke na Mume(Walipokua wamepanda Jahazi wanasafiri mara kukazuka Kimbunga kikubwa, Yule Mke akaanza kupiga mayowe na kelele huku akimwambia Mumewe fanya maarifa tuokoke au tutakufa, Yule mume alipoona makelele yamezidi alichomoa jambia lake akamuekea mkewe shingoni, yule mke akanyamaza kimya, baada ya muda kupita yule bwana akaondosha kile kisu shingoni, Ikisha akamuuliza Mkewe nini kimetokea mbona umenyamza kimya, Yule bibi akajibu umenijia Utulivu sijapata kuuona, hofu yote ya kimbunga iliniondoka, ikawa naona kwa kimbunga nitakufa na kwa jambia nitakufa sasa kelele za nini. Yule Mume akasema na mimi nimetulia moyo wangu nikawa najua aloleta Kimbunga hichi yeye ana uwezo akitaka tutakufa na akitaka tuokoke basi atakiondosha kimbunga kama alivofanya sasa hivi).
Na hiyo ndio Imani na utulivu ulokusudiwa, sio ya matatizo kidogo kukimbilia kwa waganga kuomba ufanikiwe, Unamtegemea Mtu mpaka unamuasi Mollah wako, Na sasa turejee nyuma katika yale mambo mawili ya (Dhikiri) au kukumbuka, Nini Kinatokezea?
Ukiweza kudumu kukumbuka, unakua unatumia (Energy)nguvu ambayo inatumika ukiwa kimya au ukitoa sauti, yote hayo ni sawa.
Unapotumia hizo nguvu unakutana na Sheria mbili moja hii inojulikana ya Ulimwengu ambayo inaitwa (Gravitation) na ile ya Pili ya Dunia ya pili ambayo ni ya (Sipiritual)inayoitwa(Levitation) pengine mtu ishawahi kukutokezea lakini huijui, na inatokezea mara nyingi kama umedumu kwenye Ibada au unasoma Quraan utahisi kama unapaa au unanyanyuka kutoka katika ardhi wakati umekaa, Na kama haijakutokezea fanya ujaribu upate faida ya kuijua hiyo (Levitation).
Aya Imesema wale wenye kuamini wanapata utulivu kwa kumkumbuka Mollah wao, Wanapoanza kukumbuka wanakua wanapeleka nguvu hizo za kukumbuka Moyoni, na kama kweli Mja anafanya kwa Ikhlas na kumuhitaji Mollah wake na kumkumbuka kila mara, Basi Mollah wao huwapa nguvu hii ya (Levitation)ikatokea Moyoni na kuwa utulivu wa Imani, Na ukipatikana huo utulivu nguvu hiyo haibakii hapo moyoni bali inapanda juu, Na hapo ndio unapatikana Ucha Mungu, Kwenye moyo umetulia haikubabaishi mali ya mtu, anotaka kukuroga, anotaka kukudhulumu,vyote hivyo havikushitu kabisa, Na juu kwenye kichwa utaona furaha na mapenzi yanotokea kwenye huo moyo, na hapo tena ndio unaanza kutoa nuru moyoni mwako, wale wanofahamu wanajua sasa ushapanda daraja, unageuka wewe kuwa (Light)Laa illa illlah Allah inakungarisha mbali ya kukupa utulivu, na yoyote atokua karibu na wewe anapata hiyo nuru, macho yako yatakua yanangara kwa nuru ya Mwenye enzi Mungu.
Huo ndio Utulivu ambao unaambatana na Imani, Na hakuna kitu kizuri katika Ulimwengu huu kama Imani, Imani haibadiliki, Imani haisemi uongo, siku zote inatoa uhakika, siku zote iko vilevile haibadiliki, Na ikiingia Imani unakua ushashinda, usha (Surrender) na huo ndio Uislam, kwa hiyo fanya hima ujitahidi kualika hiyo Imani ije kwenye Moyo wako ili upate utulivu, fanya sana bidii ya kukumbuka, kwani ushasikiliza Mawaidha chungu nzima mambo yako vile vile, ushasomewa hadith mabuku kwa mabuku bado hujabadilika, basi hebu jaribu dawa hii yaweza kuwa ndio ponyo lako ukapata hiyo Imani, kinachotakiwa ni kukumbuka tu, sikwambii ni rahisi lakini inawezekana, na Imani ikiingia Moyoni kwako hapo ndio unaipata Sala sawasawa, Dua zako zinapokelewa kwa uhakika. Naomba Baraka za Mollah zitushukie sote tuwe na Imani.
No comments:
Post a Comment