Asalaam Aleiykum,
Tunaingia katika kiwanja cha kundi la pili, Kundi hili lilojaa kheri tupu, Tunawauliza ili watupe habari wao wanafanya nini hata wakawemo kwenye kundi hili la kheri, Kundi liloridhiwa na Mwenye enzi Mungu.
Nini Wanafanya?
Wanafanya kitu Rahisi sana, Na wakati huo huo ni kigumu sana, Vipi kitakua rahisi na ugumu kwa wakati mmoja, wafanyacho wao ni kinyume cha kusahau, kama kundi la mwanzo wanasahau wao wanakumbuka, hiyo ndio tafauti yao, Na wewe ukifanya hilo la kukumbuka moja kwa moja unaingia katika kundi hili la kheri.
Sasa Ukumbuke Nini?
Kitu cha mwanzo kukumbuka ambacho ndio Sala yenyewe, Ndio Ibada yenyewe, Hata hao wanosali nyakati zote wanakifanya hicho hicho ni (Kulitaja Jina la Mwenye enzi Mungu) Kama alivotuamrisha katika (Sura ya Muzzamil aya ya 8)
وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلاً۬
"Litaje jina la Mollah wako, Na Ujitupe (Kwake)Kikweli(Kwa)(Devotion).
Kwanini ikawa Jina? Kwa sababu wewe mwanaadamu huna njia nyengine ya kumjua Mollah wako ila lazima upitie mlango huu wa jina, na Mlango huu wewe ndio ulopitia mwanzo kwa ajili ya mafundisho yako ya Majina, kutokana na Majina wewe ndio ukaona. (وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلۡأَسۡمَآءَ كُلَّهَا)"Akamfundisha Adam majina ya vitu vyote"(Mpaka inapomalizikia aya) Nimesema unapitia kujua ndio ukaona, nina maana hii, Ingekua kuona ni kujua basi Malaika walipowekewa hivyo vitu wangevijua, Sasa kwanini hawakuvijua, ukijibu kwa urahisi utasema hawakufundishwa, na ukisema hawakufundishwa itabidi unipe nafasi nifafanue zaidi.
Kutokana na Kadhia hiyo lazima kuwepo Mfundishaji, na hilo litakufanya uzame kwenye elimu ya (Tawhid)ili uweze kufahamu nasema nini kuhusiana na (Fumbo)hili la kufundishwa.
Katika kufundishwa au kujua lazima vipatikane vitu vitatu hivi: Anojua(Knower) Kinachojulikana(Known)Na Kisichojulikana(Unknowable) Hichi kisichojulikana ndio kinachokupa wewe uwezo wa kujua(Mollah wako), vipi leo utaweza kukiona hicho kisichoweza kuonekana, Ndio maana Nabii Musa a.s akaambiwa hutoweza kuniona, kwa hiyo na wewe ondoa itikadi yuko hivi au yuko vile usije ukapotosha Imani yako, Na kwa kuwa huwezi kumuona basi kwa Rehma zake kakupa Mbegu uipande ya kuweza kumjua, (Kwani hata ukipewa uwezo wa kumuona hutoweza kumjua) kwa hiyo chukua Mbegu hii ya kumjua ipande na hakuna anojua nini kitaota, unaweza kuota huo Mti wa majina 99 ambayo Insha Allah wiki zijazo nitakua nayapitia mawili matatu ili tupate maana yake na faida zake.
Sasa Turejee nyuma katika lile kundi la kheri kundi la Mwenye enzi Mungu. Kundi hili la pili wameambiwa ili na nyinyi msisahau mkashughulika na mambo mengine basi nyie litajeni Jina la Mwenye enzi Mungu, Lishikeni kwa mtajo Jina langu, Nini kitatokea ikiwa mtadumu katika kunikumbuka kupitia moja katika majina hayo 99. Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment