Asalaam Aleiykum,
Kubali kuna kitu kinakusumbua, Kuna jambo hutaki kulisema, mbona umenyamaza kimya, unadhani nani atakusemea, Na hofu sasa imekuzidi Umri unasonga mbele, Na ndani ya moyo wako una yakini Imani haipo, hujui ufanye nini, Moyo unakutu, kipande hicho cha nyama umekijeruhi kwa mambo chungu nzima ya maasi nk, ndio maana Imani haina nafasi ya kukaa kabisa, Na una wasiwasi pengine hiyo ndio sababu dua hazipokelewi, unakhisi katika mambo ya Dini umekua muflis, hali hiyo inakufanya uwe dua zako mfano wa(Mtu aliye kwenda kwa Tajiri akaomba akopeshwe pesa ya kiwanja, na huyo tajiri akashangaa hii huyu utajenga vipi hiyo nyumba) Na hivi ndivo sote tunavo shangaa katika jambo hili la Imani, Mbona kwangu haitokezi Imani hii, Hali yangu mimi najijua sina chochote moyoni, Nasoma Quraan, Nasali sana lakini ndani Kifuani(Empty).
Na baya zaidi nikishikwa na dhiki ima namtegemea Mganga au binaadamu mwenzangu kunitatulia matatizo yangu, sasa hapo iwapi Imani yangu, Na kibaya zaidi nakwenda kwa mganga eti kutafuta Utajiri hali najua huyo Mganga mwenyewe anataraji mie ndio nimpe pesa ili apate chakula chake, Inakua vipi namuamini Mganga kuliko Mollah wangu. Haya yote yanatukuta na tumo tunajiuliza lini na mimi nitaipata hiyo Imani niachane na mambo haya, lini nitaipata Imani iwe napeleka sala yangu kikamilifu, Nini tufanye tupate kutoka madhila, Tupate kusafisha Nyoyo zetu ili ije kukaa hiyo Imani.
Midamu umeuliza swali hili unajibiwa kuwa zipo mbinu na njia ukifanya unaweza kuipata hiyo Imani na zaidi ya Imani, ukifanya utafunguliwa mambo ambayo hujayategemea katika maisha yako, basi kama uko tayari chukua Zawadi ya aya iliyopo kwenye sura ya Rad aya ya 28. Inasemaje kuhusiana na kuipata hiyo Imani
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment