Asalaam Aleiykum,
Ilivokua ushapinga amri za Mollah wako muumba, na meachana kama wanyama, sasa nenda kakutane na kifo cha (Mapenzi)Nenda ukapate mongonyoko wa ardhi uliyoibeba. Yanatokea vipi Machungu haya? Wanatwambia Madaktari(Doctors)na wakufunzi wengine wa mambo ya taaluma ya akili kwamba asilimia 95% ya maradhi ya mwanaadamu yana sababishwa na akili(Mind)Naam kama utaamini umerogwa hata uambiwe uongo wewe hukubali, ikiwa utaamini kwenye nyumba kuna shetani basi utaanza kuona mpaka mabuibui yanapita kizani, Sasa nini shughuli ya hii Akili(Mind) iwe jambo limetokea kweli, jambo lenyewe liwe lile la kutengana na mwenzio, pengine mepata kizazi mna vitoto pamoja au kuna kumbukumbu za mambo mazuri mlokua mnafanya pamoja, pengine iwe furaha au visa vya kufurahisha au labda matunzo alokua anakupa na wewe ukimpa vyote hivyo vimesaki Akilini na leo wawili nyie mnaamua kutengana(Mnaibandua ile Magnet)kwa nguvu, toka na mwanamke au mwanamme huyo anatoka nini hapo kinafatia.
Kinachofatia hapo ni fimbo ya mwanzo ya Mwenye-enzi-Mungu kwa kuwa mevuka mipaka yake, hamkufata amri zake jambo la mwanzo anafunga Mlango wa mapenzi, na ukifungwa mlango wa mapenzi (Automatic)unafunguka mlango wa chuki na hii chuki ni bakora ya pili, Nini chuki? chuki ni mbolea ya maradhi yenye kurutubisha Akili(Mind). Na akili haipendi kifo cha haraka, inapenda kuteseka na kufa kidogo kidogo, Na hapo ndipo Machungu yanapoanza, na machungu yakianza yanafatiwa na visa, Utaliona Dume linamfata fata mwanamke nyuma nyuma bure ili ajue aendako, sasa wewe ushaamua kumuacha hizi shughuli zinakufikia nini, na hutokea vita vikubwa ikiwa atamkuta anazungumza na mwanamme mwengine, wanaweza kuchapana ngumi sokoni kutokana na hamaki zinazo patikana hapo.
Na mwanamke hali kadhalika analia kwa mashoga zake, anaungulika kwa tabu na mashaka makubwa yanayompata, halafu hatua nyengine inayofatia(Anakaa kati Ibilis)kuamrisha sasa zamu ya matusi, akiona hamtaki matusi mnaogopa kunywa sumu hii basi hapo anakupelekeni kwenye uwanja wa visa, utaona mume ghafla kaanza kulewa au kuvuta (Mihadarati)au hata sigara pia lete au anakula miraa na kucheza kamari au kuzini, eti kujaribu kumsahau yule alo muacha bila ya utaratibu wa sheria, na huku unakuta mke kapayuka, kashetupa hijab, yuko uwanjani anarusha roho, pengine maskini alikua hana tabia hiyo, Mume kwa tafrani za talaka alotoa mwenyewe anaanza kuzungumza saana, mambo yakizidi anazusha balaa jengine la kulipiza kisasi, eti anatafuta mke mwengine au mume mwengine.
Anachukua zile chuki na bakora zake alizochapwa huko atokeapo na kwenda kumpachika nazo mtu mwengine aso husika kabisa, Zinaendelea chuki hizi na sumu za talaka na kama hazina pakutokea inabidi sasa zishuke kwenye (Body)sababu (Akili-Mind)ni sehemu ya kiwiliwili, na ikishuka chini sumu hii inaanza kuangamiza viuongo, ndio utasikia mara sukari, mara kichwa, tumbo halishi, na (Ulcer)za kila leo, mara mapigo ya moyo yanakwenda haraka haraka, mara shingo imevimba, miguu haishiki, na ugonjwa wa wasiwasi unafatia juu yake, kumbe chanzo cha hayo yote ni Talaka, nyie yafanyieni uchunguzi mtayagundua hayo.
Ndio maana mkaambiwa Talaka ni ruhusa anayo ichukia Mollah wetu, na ajue yoyote yule afanyae kwa makusudi kuivunja ndoa kwa kutoa talaka au kudai talaka basi ajue fimbo ya Mollah wake inamsubiri na ni lazima adhibiwe. Na mnapofikia hali yakua sasa hamuwezi hata mkijaribu kuishi pamoja, basi fanyeni hima kuikumbuka aya hii ya mwanzo ya sura ya Talaq, mwanamke asitoke ndani ya nyumba abadan. Amwambie mumewe mimi naogopa kukutesa wewe na kujitesa na mimi kwa ajili ya kupinga amri ya Mwenye-enzi-Mungu, au kama huwezi basi muandikie barua yeye si anaandika talaka, wewe andika barua mwambie"Ewe mwenzangu katika Imani, kumbuka wema na ihsani tokea tulipo funga ndoa, kumbuka heshima tulopewa katika harusi yetu, na zawadi zilotoka kwa watu na Mollah wetu, za furaha na mazuri"kwa ajili hiyo mimi naogopa kumuasi Mollah wangu kwa amri zake alizozitaja katika sura ya Talaq aya ya kwanza na ya pili, na kama wewe mwenye kusisitiza ya kuwa nitoke, basi namueka Mollah wangu kuwa shahidi wa hayo, na mimi namuomba Mollah wangu adhabu zote za hii Talaq akushushie wewe kwa uweza wake. Ikiwa umeridhika na hilo mimi nitaondoka, ikiwa mwanamme au mwanamke hayo ndio yawe maneno yako.
Ndugu zangu Msifanye talaka kuwa jambo la mchezo, Talaka zina athari kubwa katika maisha ya Binaadamu, zinaleta uharibifu wa afya, ukosefu wa furaha, upotoshaji wa kizazi, pamoja na kuiharibu akili yako, kwa kujidhulumu na kujinyima raha na ladha ya Mapenzi inakatika kabisa, mpaka upate mtu mwenye taaluma kubwa ya mapenzi na utiifu kwa Mollah wake ndio aweze kuufungua tena huo mlango, na hilo ni vigumu kutokea kila wakati.
Basi kwa yoyote yule mwenye kudhamiria kudai au kutoa hiyo Talaka basi kwanza azingatie hayo niliyoeleza kabla hajafikia uamuzi wa kutenda jambo hilo.
Namuomba Mollah wangu utudumishe katika ndoa zetu mpaka tuhitimishane, Wenye magonvi wapatane, waloachana warejeane, wanochukiana Rabb wapendane, Akija Ibilis Mollah wajaalie kwa dalili wamuone, Na akitokea Jasusi la kuharibu ndoa Rabbana tujaalie tushikane. Amin
MashaaAllah ni ukumbusho mzuri kwa wenye mazingatio.
ReplyDeleteHeee mihani. Maneno mazito kwa mwenye kuyazingatia. Ndo itakua ule msemo. 2Ningejua nsingedai talaka ina mambo" Mungu atuhifadhi in shaa Allah
ReplyDelete