Sunday, September 29, 2013

UZURI WA MAISHA PART 1

Asalaam Aleiykum,

Tunaishi katika Ulimwengu huu tukiwa tumegubikwa na dhiki, mateso, na tabu za maisha, Na kila siku ijayo kwetu sisi inakua nzito na ilojaa vitimbi vya kero.
Kwanini inakua hivyo jawabu utalikuta unalo mwenyewe lakini hujawahi kujiuliza, unaogopa kujiuliza kwa sababu unaona katika kuishi kwenye hizo kero, maudhi na tafrani za maisha zilojaa Akilini ni bora, kwa sababu kila mmoja anaona bora mie kuliko mwenzangu, yeye dhiki zimemzidi, yeye anahangaika, kwa kuona hivyo mtu anaona bora nitafute dawa za kunipa nafuu na matatizo haya, na hakuna dawa  za kunilaza mimi na kunipa raha ila Mirungi na Bangi, Mihadarati na ulevi mwengine ili nipate kuzungumza sana nijizubaishe na dhiki hizi za maisha, Wacha mimi nikazubaishe wakati kwenye Taraab, au ngoma ya mduara, mimi haijambo ninacho cha kunizubaisha angalau kwa muda mfupi kuyapata mazuri hayo, na yakimalizika narudi tena kama kawaida kwenye matatizo yangu ya (Dipression)na mengineyo.
Sasa huko tayari kama atakuja mtu akakwambia kuna dawa ya kutibu hiyo(Dippression), kuondosha hayo matatizo, kuponesha hayo maradhi yanokufanya usione (Uzuri huu wa Maisha), Basi toa nafasi tuchane (Kizoro ulichojifunika)ili tupate kukujulisha nini Uzuri wa maisha, na vipi utafanya ili uweze kuyaona maisha haya unayoishi ni mazuri.
Kukupeleka katika ufahamu huo itabidi kwanza urejee nyuma na kuangalia ndani ya Akili yako au kwa lugha nyengine utazame (Fikira)zako, lakini nakutahadharisha hizo fikira zitakuzungusha(Merry go round) zitakutesa fikira hizo usijue nini la kufanya kama ulivyo hivi sasa, zitaendelea kukuadhibu usipate kuona uzuri wa maisha, Ndio maana mwanzo nikasisitiza kuangalia au kuona kwa sababu katika kuona ni tafauti na kufikiri, Na ukiwa tafauti na fikira unaanza kuyaona maisha kwa njia nyengine(Pureness of life)njia ya uzuri wake, na ukiyaona kwa njia hiyo na wewe unageuka kuwa(Blissful).
Basi kwanza itabidi uangalie kwanini huoni maisha haya uzuri wake, Sababu kubwa ifanyavo hivyo ni kuwa Akili yako imetawaliwa na mabaya mengi, Kivipi? Jitizame wewe kwanini hukumbuki harusi yako lakini unakumbuka maradhi yako, kwanini hukumbuki mema 99 ila unakumbuka ubaya mmoja, kwanini unakumbuka mateso na hukumbuki furaha, kwanini unakumbuka machungu na hukumbuki raha, na mengi mengineyo mnayoyajua. Sasa nini kinatokea hapa? Endelea Part 2

UZURI WA MAISHA PART 2

Asalaam Aleiykum,

Kutokana na hali hiyo sote tunajijua Wagonjwa na sasa tunahitaji dawa ili tupate nafuu ya maradhi haya, tupate japo kidogo katika umri wetu kuona uzuri wa maisha, Na (Dose) ipo huna haja ya kwenda hospital au pharmacy, huko wanakwenda walozidiwa wewe unaweza kutibiwa nyumbani bila ya matatizo, na dawa ya mwanzo kabisa utaipata ndani ya (Quraan) nitakupa hii sura ambayo kama utaifanyia kazi ina siri ndani yake, inaponesha maradhi ya fikra ulo nayo, inaponesha (Depression) inaondoa wasiwasi akilini, inakutuliza ama kwa kuisoma au kusomewa iwe kwa kuandikiwa au kutiliwa kwenye maji dawa (mjaarab) sana mimi mwenyewe binafsi nawapa watu na inawasaidia, Na hiyo ndio siri ya (Quraan)kama nilivoitaja katika Darsa yangu ya (Rehma na matibabu ya Quraan).
Katika sura hii ni sahihi kabisa kama ilivotajwa na (Masheikh wakubwa wakubwa kuwa imeteremshwa kwa ajili ya kumliwaza Bwana Mtume s.a.w)lakini kumbuka alichoteremshiwa Bwana Mtume s.a.w wameteremshiwa walimwengu wote, na kila Mwanaadamu inamgusa isipokua akiwa hataki mwenyewe, kabla ya kwenda kwenye sura yenyewe na kujua faida yake napenda kukujulisha dhumuni la nje la sura hii, kwa njia ya nje nayo ni (Rehma)inakutaka sura hii uwe Shahidi(Witness) na sio (Historian)kama ulivo sasa unaishi(in the past) inakutaka sura hii uwe na uwezo kama ulionao hivi sasa wa kuweza kusahau Mazuri basi na mabaya usiyakumbuke uwe mtu wa kati na kati( وَڪَانَ بَيۡنَ ذَٲلِكَ قَوَامً۬ا ) ukiiwacha tabia hiyo utapata nafasi ya kwenda  (Beyond Both) Utakua hukumbuki mazuri wala mabaya, fanya ((Balance and then you are)unakua ushawasili kwenye ushahidi, Nikamate mkono vizuri usafiri na mimi kwenye Ulimwengu huu nikutoe kwenye mashaka upate kuona Uzuri wa Maisha haya, fika pahala ambapo kama utazinduka basi kila jambo lako ukiwa maskini au tajiri, ukiwa na maradhi au afya utakua una furaha, na kila kitu chako utakiona kuwa ni kizuri, hapo ukishawasili kwa furaha za kuona uzuri wa maisha haya hata mtu akikupiga kibao shavu la kulia utamgeuzia na la kushoto akumalizie.
Na hiyo sehemu ya pili ya sura hii ambayo ndani yake kuna hizo (coded massage) za kutibu maradhi kama (Depression)na wasiwasi utaisoma pia ukiwa na donge la Roho ni kuandikiwa au kuyasomea maji mara 70 sura hii ya (Dhuhaa) inaondosha madhara ya Tafrani katika Akili yako, Na uteremkaji wa sura hii ulikuja pale Bwana Mtume s.a.w alipokaa muda mrefu ukawa (Wahyi)haukuteremka basi alikua katika hali ya huzuni kubwa ya maisha yake, na huku Watu wakimfanyia stihzai, vipi Mollah wako kakasirika nk, ndio ikateremka sura hii kumliwaza na kumpoza Bwana Mtume s.a.w, Na wewe pia inakupoza  sura hii kama ilivosemwa Quraan imeletwa kwa ajili ya (Mankind)basi na wewe umo, na Mollah wako anakupoza na ukiwa Shahidi utajua kweli na mimi nimepita katika hali hizo zote na hiyo ndio Quraan na maajabu yake, uongozi wake, matibabu yake pamoja na hizo Rehma. Sasa tutaipitia aya moja baada ya moja ili tugundue tufanye nini na sisi tufurahi kama alivofurahi Bwana Mtume s.a.w ilivoteremka sura hii, na hakuna furaha tutayoipata sisi kama kuona uzuri wa maisha haya, kumbe mambo hivi ndivo yalivyo. Endelea part 3

UZURI WA MAISHA PART 3

Asalaam Aleiykum,

Kwanza wacha nifafanue nikisema unatakiwa uwe shahidi namaanisha nini kama utanifahamu, mwanzo kabisa nilitaja kitendo cha kuona, kuona kwenyewe kunakua hivi.
Ulipokua mdogo unayaona maisha lakini huyajui uzuri wake, Ulipofikia Ujana uliyajua lakini huyafahamu, na sasa Uko Uzeeni unayafahamu maisha uzuri wake lakini huyajui tena, maneno yasikuchanganye kwani kujua kunatokana na (Mind) Akili, na kufahamu kunatokana na Roho(Soul) Ulipokua kijana unajua kukoga wala huogopi kokote unachupa, lakini sasa hivi Mzee unafahamu loo nikichupa msuli ukibana nimekufa, huko ndiko kufahamu, au nitoe mfano mwengine kwa wale walocheza mpira au dance watafahamu vipi unapocheza kandanda (Mind) Akili inavo (Stop)hukumbuki mke wala jamaa unabakia wewe na mpira, unakua (Totally)pale umewasili, au mcheza ngoma huwezi huku unacheza ukawa unafikiri nitakula nini (style) zitakupotea, kwa hiyo kuna vitu vinakufanya usahau hiyo (Akili) na ukiisahau wakati ule ndio unakua Shahidi(Then you are)ukiweza kuhisi hivyo ndio utaona uzuri wa maisha.
وَٱلضُّحَىٰ
"Naapa kwa Mchana"
Aya imeanza moja kwa moja kwa Mchana,(Light)Mchana ni wenye kumurika, mchana ni wenye kuleta furaha, Mchana unakupa mwanga.
وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ 
"Na kwa usiku unapotanda(Kutulia)"
Hapo vimetajwa vitu viwili unavo vishuhudia, wewe unapita katika viwili hivi kimoja unakua mcheshi unaruka ruka chengine unakua mkimya tayari kwa kulala, usiku unakuvunja kasi(Dark night) ndio maana huku Ulaya unaona watu na Tafrani sana za maisha wakati wa (Winter)kutokana na (Dark night) hapo vimetajwa viwili vyote ili upate kujua haya maisha na kujaa na kukupwa, kuna furaha na machungu, kuna kuzaliwa na kufa, kuna mabaya na mzuri, kuna utajiri na umasikini, kuna kupata na kukosa kuna maradhi na afya wewe pita katika hayo yote ukiwa Shahidi ndio utaona uzuri wa maisha haya.
 مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
"Hakukuacha Mollah wako wala hakukasirika"
Na maneno haya kila mmoja yanamuhusu wengine wanalaumu dini, wanaacha kuabudu, anapita mtu kusema nasali siku zote mbona sipati, vipi Mollah wako akutupe na yeye ndiye aliyekupa nafasi hii ya uhai, na hiyo riziki unayoitafuta kwa nguvu zako zote, vipi akukasirikie na wewe kiumbe chake dhaifu, anakupa ukimuasi na hata ukimkimbia usimuabudu yeye anakusubiri anajua utarudi kwake, vipi akukasirikie, kutokana na pupa zako wewe ndie mwenye kukasirika, jiangalie uzuri usimtafute mchawi ni wewe mwenyewe.
وَلَلۡأَخِرَةُ خَيۡرٌ۬ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ
"Na wakati ujao (Utakua) Bora kwako kuliko ulotangulia"
Kila mmoja wetu mwenye kufikia dhamana ya Akili yake anafahamu hili, vipi alivopita kwenye misukosuko ya maisha mpaka kufikia hii leo, Tumepita sisi  katika hali ngumu za maisha, matatizo ya kila aina, lakini kila siku zikenda unapata nafuu na utulivu wa maisha haya na kuzingatia (Uzuri wake) Kama umefahamu uzuri basi huna haja ya kuanza kufikiri zamani ilikua raha, tulikua hivi na vile, tukistarehe, maisha yalikua mazuri, hiyo utakua unafikiri (Collective) kwa ujumla, kwanini sasa hivi yasiwe mazuri, sababu kubwa unaishi sasa lakini (Mind) Akili yako ipo kwenye zamani na hayo ni matatizo, Ishi maisha ya sasa Utayaona Uzuri wake, dunia haijabadilika wewe ndio umebadilika, Ndege ndio wale wale, kunguru bado wapo, Bahari iko vilevile, mawingu ni yaleyale, hebu ishi usijitie dhiki, tizama uzuri wa maisha, kumbuka wakati ndio ulopita, sasa hivi sio wakati wako, Vijana ndio wakati wao, waache wao wafurahi na wewe furahi, nenda katika maisha haya ukiwa umeridhika, shukuru na wewe umepewa nafasi mpaka leo unaishi na unashuhudia maisha haya, videge vinaruka, mawingu yamependeza, mvua imenyesha, leo umekula vizuri, umeamka unaumwa kidogo yote hayo ni sehemu ya maisha, lazima uridhike na upite ukiwa (Present) Shahidi, sio upite (Automatic)ukiulizwa jana umekula nini hujui, vipi utaona Uzuri wa maisha, Shukuru umepangiwa usipate zaidi, cheka moyoni kuwa umeigundua (Qadar) ya Mwenye enzi Mungu na huna pingamizi nayo. Tizama Ulimwengu wako ulivyo, panua uangalizi wako wa Shuhuda uwe unaona mambo kwa kutumia moyo wako sio macho, na kama unatumia macho pekee ndio utaona huishi kununa, unaishi kwenye hasira, lakini ukitumia kuona kwa kupitia moyo basi wewe unakua shahidi wa kweli, ukipewa mkono na mtu unahisi mpaka umoto wake, mtu akikupa kitu ona kakupa kwa mapenzi, na wewe ukitoa kitu usisubiri shukurani ona umetoa kwa mapenzi, ukifanya hivyo kidogo kidogo utaanza kuona Uzuri wa maisha.
Endelea part 4

UZURI WA MAISHA PART 4

Asalaam Aleiykum

 وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ 
"Na Mollah wako atakupa mpaka uridhike"
Wengi katika sisi tunapewa mpaka tunaridhika, mwanzo ulikua huna familia, Mollah kakukutanisha na Mkeo mmepata kizazi, kakunyanyua maisha umepata uwezo wa kujenga, umemaliza masomo umepata kazi nzuri, una marafiki wapenzi, umezungukwa na familia, umepata cheo katika jamii na kazini, vipi leo unakataa kuridhika, vipi unaona maisha haya ya tafrani, lazima wewe ndio una matatizo lakini sio maisha abadan,kuyaona maisha haya uzuri wake kinachotakiwa Ridhika, kila jambo lako litakua zuri.
 أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمً۬ا فَـَٔاوَىٰ 
"Je hakukuta yatima akakupa makaazi"
Ili uwe shahidi ya hayo katika mpito wa maisha unakumbushwa kutokana na mwenendo wa maisha ya Binaadamu hilo linatokea kila leo, la wazee mmoja au mwengine kufariki na Mtu kulelewa na watu wengine, kwa hiyo kuoneshwa Uzuri wa maisha haya unapokuja kwenye Ulimwengu huu basi unapewa makaazi ya kuhifadhiwa, na kama walivofanyiwa wengi walopoteza wazee wao, na taratibu hii inaendelea mpaka hivi sasa.
وَوَجَدَكَ ضَآلاًّ۬ فَهَدَىٰ
"Akakukuta umepotea(Hujui cha kufanya)akakuongoza"
Sote tunafikwa na hali hii katika maisha haya, kuna baadhi wanazama kwenye uharibifu ikisha wanaletewa uongofu utokao kwake wakaja kuwa watu wema, hukuongoza Mollah wako katika kufanya mema na kuyaepuka mabaya, hukuachisha kufanya maovu ukawa ni mwenye kutenda Ibadah, na kila mmoja humteremkia uongozi huu na mtu ana khiyari yake kufata au kutokufata.
وَوَجَدَكَ عَآٮِٕلاً۬ فَأَغۡنَىٰ
"Na akakukuta maskini akakutajirisha"
hakuna anozaliwa tajiri, sote tunatokea katika hali duni, ikisha Mollah wetu anatupa kwa taratibu alotupangia mwenyewe mpaka tukaridhika, isipokua wale wanoamua kuchukuwa wenyewe kwa njia za mabavu, rushwa na mengineyo hao kawapangia malipo yake katika maisha haya.
فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ 
"Basi usimuonee yatima"
Ukaona huyu hana msaidizi wacha ni mdhulumu, au kumnyanyasa, usiharibu mwenendo huu wa maisha mazuri kwa kumfanyia yatima uzito na dhuluma, kumbuka yuko alo juu yako na yeye atakuonea kama unavoonea.
 وَأَمَّا ٱلسَّآٮِٕلَ فَلَا تَنۡہَرۡ 
"Na wala usimkaripie aombae"
Mpaka mtu akaja kwako kukuomba ujue ana shida kwa hali unayoijua, basi hata kama huna mjibu kwa unenyenyekevu, na kama unacho usizuie mpe japo kidogo, ili huzuni iondoke moyoni kuwa umemnyima, wewe utafarijika na yeye atapata faraja, na huo ndio uzuri wa maisha. 
 وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ
"Na Neema ya Mollah wako hadithia"
Sasa ushakua na fahamu, ushaishi maisha haya na umeyaona mengi katika mambo ni mazuri kuliko mabaya, umeridhika na ulichonacho, umejaaliwa kutembea hapa na pale, umefika huku na kule, umekutana na huyu na yule, umeonja hiki na kile, kuna siku umefurahi na siku umelia, kuna muda ulikua na maradhi sasa umepona, yote hayo wewe ni shahidi umeyapitia na unaendelea kuishi nayo, basi ona uzuri wa maisha Mbingu Buluu, bahari shuwari, usiku unaingia, mchana unangara, unavuta pumzi bila ya matatizo, huna tatizo lolote wewe na familia yako, unapata kula yako, pengine (Bank)pesa zimetulia, unafanya ibada kwa utulivu, watoto wanasoma hawana shida yoyote, hizo zote ni Neema za Maisha Mazuri, na inatakiwa uzihadithie kwa mdomo na vitendo ili upate kuona uzuri wa maisha. 
Mollah tujaalie kuona Uzuri wa maisha haya ili tusipate dhiki na uchovu wa kutoamini Maisha hayo yajayo ya Akhera. Amin.


Sunday, September 22, 2013

FURAHA YA MAPENZI PART 1

Asalaam Aleiykum,

Napokea wingi wa malalamiko hususan kutoka kwa ndugu zangu Wanawake, wakinieleza masikitiko yao kuhusiana na kadhia hii ya mapenzi, Wanalalamika ndani ya majumba yao penzi limehama na halipo tena, au bado limebakia upande mmoja, walalamikiwa hapo ni Wanaume, wanataka ushauri nini kifanyike ili wapate na wao mapenzi kutoka kwa Waume zao, au kuna kosa gani wanatenda ili hata imewakuta hali kama hii. Nakuomba uzame katika Darsa hii ili ukitoka upate Lulu ya Mapenzi, ujue vipi utaitumia.
Wengi katika sisi tunajua neno mapenzi, lakini hatujui nini kitendo mapenzi, na kinapokuvaa unakua katika hali gani?, kwa lugha ya uchambuzi tunapata hisia za mapenzi, wote hiyo ni haki yetu, lakini hatujui hii hali ya Mapenzi inakuaje, na wengi inawatokezea wakati wa (Teen Age) tena kwa muda mfupi, baada ya hapo unaikandamiza hali hiyo unakua si mwenye kujua tena nini Mapenzi, na ina uzuri gani kuishi ndani ya hali hiyo, kinachobakia unaishi katika hali ya ujambazi wa mapenzi na huko ndio kubakiwa na neno tupu lisilokua na maana.
Lakini vizuri sababu usilolijua halikusumbui, leo hapa nataka nikuoneshe japo kidogo kiji njia ukiweza kupita hutorudi tena nyuma utayasaka mapenzi popote yalipo, na ujue hayapo popote ila yanateremshwa kutoka kwa Mollah wako, kinachotakiwa kwako ni subira. Kabla ya kwenda huko wacha tuwafahamishe pande zote mbili kinachowasibu ili yapate kuwapungua mateso, wapate kupandisha mbegu ya (Mahaba).
Kwanza Nawafahamisha hili, (Kupitia Mapenzi, Machungu hugeuka Furaha)
NINI Mapenzi?
Mapenzi ni kitu kilichojificha ambacho hakielezeki kama vile usivoweza kuileza nini Afya, Hali hii inatokea huko Mbinguni kama ilivo haidiwa kuwa inateremshwa pamoja na Rehma. Kwa ufahamu wetu sisi Mapenzi ni Hisia(Feeling) nzuri za furaha(Blissful) zenye kukusahaulisha kama wewe upo ila penzi ndio lenye kuishi, ukiijua hali hiyo wewe ushayajua mapenzi, au ukimpata mwenye kujua akakufahamisha basi huyo atakupeleka kwenye (Level) nyengine kirahisi kabisa kama utamsikiliza.
Mapenzi haya yana ngazi 99 mie leo nazitaja 3 lazima uzipite kufikia hali hiyo ya (Blissful)Furaha, hali ambayo utakua nayo huko Peponi, lakini hapa Ulimwenguni lazima uzipite uzitumie hizo ngazi tatu kufikia huko kwenye (Totality of Love).
Kwenye Mapenzi Mfalme anageuka kuwa Mtumwa,
Unapata kuzijua ngazi hizi tatu ili Umjue nani (Gigolo) na yupi (Lover Boy) na nini (Love).
Ngazi ya mwanzo kabisa na ndio ya chini iliopo baina ya magoti na kitovu ni (Sex) kwenye ngazi hii sana utawakuta wanaishi wanaume, na ikiwa mtu atajisahau hapa hapa, anakua hana tafauti na mnyama ambaye sote tuna (Share) naye hali hii ya utamanifu, na hapo inabidi ifanyike kazi kubwa ya kumsukuma (Dume) hili kwa kufahamishwa Bwana wee kuna (Lift) hebu panda uende ngazi ya pili uka (Enjoy) Ghorofa ya Pili ambayo ni nzuri zaidi kushinda hii ya kwanza unayopoteza nguvu(Energy) zako na kuzitumia bila ya 
Hekima.
Kwanini nikasema hivyo kwa sababu ukimwachia Mtu wako katika (Energy) hii ya (Sex)ya machafuko hana matumaini ya kupasi mtihani, na hapo wengi wamefeli, hapo pana matatizo makubwa sana yanayotokea, na uharibifu mkubwa unapatikana hapo, na ndoa zote zinaanza kubomoka hapo  kwa ajili ya (Kumcheza Kipole) unatokea uharibifu ambao hauwezi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote, yanazaliwa hapo magonvi yote ya kwenye ndoa, hapo ndipo linapouwawa penzi la kwenye Nyumba, hapo ndio yana sababishwa maradhi ya mfanyaji na anayefanyiwa, ndio maana mkaambiwa ama kwenye jambo hili msikurubie kabisa nyinyi hamna nguvu ya kutoka kwenye (Magnet) hii kama inavotajwa katika sura ya Israa aya ya 32"وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓ‌ۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ فَـٰحِشَةً۬ وَسَآءَ سَبِيلاً۬ "
"Wala msikaribie Zinaa, hakika hilo ni jambo chafu na njia Mbaya"
Yenye kufungua chungu ya njia za mabaya, ukigusa una nasa, na ukinasa umekwisha, na ukisha unakua si mwenye kushugulika tena na Nyumba yako, penzi halikai tena moyoni mwako, yanabakia matamanio pekee yanokupeleka kwa yule asiye kuwa wako, na hata kama utashughulika kwa yule aliye wako, inakua kwa kitendo maalumu cha mahitajio yako, na huyo mwenzio ana hisi kuwa kwake yeye ni unata kitu kimoja wala si mwenye kushughulika na (Feeling) zake, na ukikwama katika ngazi hii vigumu kunasuka, unakua kama yule mwenye kutumia madawa ya kulevya, na hapo ndio unaanza Mushkel mkubwa, kutokana na maafa yaliyomo kwenye akili yako, mpaka uso unaondoka furaha, kwenye mawazo yako kuna kitu kimoja na wala hakiingi chengine abadan, unakua tafran, huna mapenzi mpaka kwa wanao, wala ya kitu chochote, umeambiwa hakika hilo jambo chafu na njia mbaya, maisha yanaanza kuharibika na unaselelea kwenye penzi la kitu kimoja tu nalo ni hio (Sex) Unakua huthamini utu wala huoni haya unageuka kuwa mnyama unayeishi na wanaadamu, na wala huna matumaini ya kupanda kwenda kwenye hiyo ngazi ya Pili ambayo sana wanaishi Wanawake na furaha za maisha ikiwa wanapata ukamilifu wa Mapenzi. huko ngazi ya pili kwenye haya Mapenzi kunatokea nini na kuna ladha ya aina gani kama utayapata mapenzi, na ufanye nini ili uyapate hayo mapenzi, na unajuaje kama sasa unaishi ndani ya mapenzi, kutaka kulijua hilo Endelea Part 2

FURAHA YA MAPENZI PART 2

Asalaam Aleiykum,

Tumeshaona vipi mwenye kuendekeza matamanio haya ya mapenzi ya (sex)jinsi anavoteseka na kuwatesa wenzie, hatukatai yumo kwenye njia ya mapenzi lakini ni ya muda mchache sana, na anapomaliza haja zake anajikuta tafrani, hana furaha, na ili kujizubaisha inabidi aende mawindoni tena ili kupata furaha zake za muda mfupi, na hizo ndio zinakua shughuli zake mchana kutwa, muulizeni nini kila wakati kinaingia ndani ya kichwa chake, mawazo gani yanatawala senema yake kwenye akili, atakunyima jawabu lakini muda wote ni mawazo ya mapenzi ya utamanifu.
Huyu sasa anahitaji msaada, anahitaji kuambiwa sio kila kitu kinaanzia hapo na kuishia hapo kwenye ngazi ya mwanzo ambayo ya kitovuni na kwenye magoti. Huyu anataka kufahamishwa na apewe nasaha ya kwamba acha kujidhuru, jaribu kutunza (Energy)yako, jifundishe kusubiri, toa nafasi ya kutamani, jipe siku mbili tatu nguvu zikomae, halafu afahamishwe kuna ngazi ya pili ambayo utapata furaha, ashikwe mkono kuvutwa kwenye ngazi hiyo.
Ipi Ngazi ya Pili?
Ni ngazi ilotokea kitovuni kuelekea kwenye moyo, hapo inakaa furaha na utulivu, (kule kwetu Zanzibar)kuna ngazi nje, Ngazi ndani, na Ngazi mia, naifananisha hiyo ngazi ya mwanzo ni ngazi ya nje shughuli zako zote ni kwenda nje, ukikiona kile umekitamani, cha huyu unakitaka, cha yule umempokonya fujo tupu, ukiamua kuchupa kwenda kwenye hii ngazi ya pili ambayo ni ya ndani inabidi urudi kwenye Moyo wako na kufanya utafiti mkubwa, Ndio maana ukaona (Symbol)alama ya mapenzi ni Moyo, umechorwa kwa mfano wa kopa, kwenye hiyo kopa ukiitizama ina mifano mitatu, chini bonde, juu milima, ikisha alama hizo zilizo na mizani sawa zinakutana katikati kuifanya hiyo kopa, unajua kwanini ikawa hivyo, sababu katika hayo mapenzi kuna kushuka na kupanda na pia kuna kukaa sawasawa katikati, imekua hivyo sababu nyinyi kwenye hiyo nyumba au kitanda mnaishi watu wanne, (Kumbuka wewe una sehemu mbili Ubavu wa kushoto Mama yako na Ubavu wa kulia Baba yako, na mwenzio anakuja na mfano huo huo) kwa hiyo tafauti lazima iwepo, kama bahari mara imechafuka mara imetulia na hiyo ndio alama ya kopa, alama ya Mapenzi na kuonekana kwake kwa mfano wa Moyo.
Utizame moyo daima una furaha unacheza na kupiga mpaka siku yako ya kufa, ila wewe ndio unaoupelekea matatizo, hiyo ndio ngazi ya pili(Ngazi Ndani) na hapo sana utawakuta wanaishi wanawake, Moyo ni wenye kupokea hewa, unasukuma damu, na mapenzi yakishuka huko yatokako yanaanzia hapo na kusudio la mwanzo la hayo mapenzi ni kuipenda (Roho)Mapenzi ni (Sipiritual) nataka uwe na tahadhari kubwa, isije ikawa unashushiwa  mapenzi yanakukuta unaangalia masofa,utakua mwenye kupenda (Furniture) usije ukawa unashushiwa mapenzi unaangalia mpira, mapenzi yako yote itakua mipira, na yasije kushuka mapenzi yakakukuta kwenye Taarab utaumia, utakua unakwenda bila ya kualikwa na ukiikosa harusi unakua mgonjwa, au yanakukuta (Disco) basi jijue utakua (Muflis)au umo kwenye kutizama mchezo wako senema itakua huna faida na jambo hilo, uchunge moyo wako hususan katika hili la kuteremkiwa na mapenzi, ni jambo adhimu sana.
Mwanamme penzi lake linaanzia kichwani ndio maana utaona mambo yake yote ni (Through action)kulieleza hili itabidi nikupeni kisa cha Nabii Musa a.s alipokua akikimbia kutoka kwa (Firauni)tizama jambo la mwanzo lilomtokea kwa kujawa na mapenzi na huruma kwa ajili ya watoto wa kike walokua wanataka kuwanywesha maji mifugo yao, (Through action)kaonesha mapenzi yake kwa njia ya huruma akawasaidia  kisha akenda kivulini akarudi moyoni kwake akazungumza na Mollah wake na kumwambia maneno haya, al-Qasas aya ya 24

"" فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰٓ إِلَى ٱلظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّى لِمَآ أَنزَلۡتَ إِلَىَّ مِنۡ خَيۡرٍ۬ فَقِيرٌ۬ "
Basi (Nabii Musa)akawanyweshea, ikisha akarudi kivulini, na akasema Mollah wangu bila shaka mimi ni Muhitaji wa kheri utakayoniteremshia.
Elewa hakuna kheri kubwa kama mapenzi, (Through Love you find God)(Taqwa)Kwa hiyo na wewe kaa pembeni ufikiri moyoni mwako unataka kheri gani ikuteremkie. Kabla Nabii Musa a.s hajamaliza uzuri dua yake anarejea mtoto wa kike huku akicheka cheka na kuona haya na maneno haya.

فَجَآءَتۡهُ إِحۡدَٮٰهُمَا تَمۡشِى عَلَى ٱسۡتِحۡيَآءٍ۬ قَالَتۡ إِنَّ أَبِى يَدۡعُوكَ لِيَجۡزِيَكَ أَجۡرَ مَا سَقَيۡتَ لَنَا‌ۚ"
Basi akamjia mmoja katika wale (Wanawake)wawili anakwenda na huku anaona haya, akasema Baba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea (Mifugo). Na mpaka inapomalizikia aya.
Watoto wakike mapenzi yamewashukia moyoni, mtu hawamjui lakini wamemshauri Baba yao amwambie Nabii Musa a.s achague yupi atakaye kumuoa, Na Mtume wa Mwenye Enzi Mungu akamchagua yule yule alopangiwa na kuvutika nae kwa mapenzi akawa mkewe, na wewe huyo ulonaye ndio ulopangiwa kwa hiyo kakae na wewe kipembeni ukayaombe mapenzi muda bado unao pata (Experience)usitoke mbio huko uendako kuna mateso na siko ulikopangiwa. Sasa na wewe Dua yako ikipokelewa nini kitatokea.
Endelea Part 3

FURAHA YA MAPENZI PART 3

Asalaam Aleiykum,

Tahadhari na kinachotokea hapo, usije ukaomba dua ikawa hujijui penzi likadondoka kutoka kichwani na kwenda magotini utaingia hasarani, hutopata msaada, usicheze na nguvu ya (Sex).
Ama kwa upande wa Wanawake wao moja kwa moja linaporomoka moyoni na ndio maana utaona kajaa mapenzi, mwenye huruma, rahisi kusamehe, shujaa wa kupokea mazuri na machungu, mstahamilivu na mwenye kuonesha mapenzi yake kupitia hisia (Feeling).
Anaonesha mambo yake kwa njia za hisia akitaka kujulikana kakasirika ananuna inakua hakuna (Communion)wala(Communication).
Sasa vipi Wawili nyie mfanye mpate furaha ya mapenzi. La kwanza kabisa kufanyika inabidi umpe mkono mwenzio ili apande kwenye ngazi ya pili iliyopo moyoni, Na akifika muombe hebu tujaribu japo miezi mitatu kuwa tutafanya mambo yetu pamoja, Pia umfahamishe tafauti ya (Likes) na (Love)Mapenzi maana yake ni (Sharing)ndio ukaambiwa wapende maskini, wapende mayatima, na pia ukamuona mama anavo (Share)mapenzi yake kwa watoto wake wote, Kwa hiyo na wewe (Share) Na Mumeo au Mkeo, na mapenzi yanataka mbolea, na mbolea yenyewe ni hiyo (Action) ndio nikasema fanyeni mambo yenu pamoja, tokeni pamoja, nendeni kutembea pamoja, shirikianeni katika kila jambo linalohusu wawili nyinyi,Nendeni Baharini mkakoge pamoja, shikaneni mikono sasa mnaona haya za nini wakati nyinyi ni mke na mume, ukiona wenzio wanamtizama alo wako jitupe begani, unaogopa nini na wewe umevaa (Niqab)fanya uhakika kila uendapo awe pembezoni mwako, Wakiristo wao wanavaa pete, wewe mvae mumeo au mkeo, usisubiri ukiweza mfate mpaka kazini, sio kama mnavofanya hivi sasa utawakuta mtu na mkewe wanafatana mmoja yuko mbele mmoja yuko nyuma utadhani mke wa mkulima, mbona mnakimbiana kuna nini, ikisha mnauliza mbona hakuna mapenzi.
Mkirudi nyumbani kazi zenu ziwe za ushirika, ukimuona mwenzio anavua soksi kimbilia upate kuzivua wewe,Mfungue vifungo vya shati au zipu, Mbebeleze japo hajalia, Somaneni tabia kama anatabia inakukera(Mfano)anavuta sigara toka ukamnunulie kinyonyo, akisema hee mbona kinyonyo mwambie Sheikh Baja kasema (Kinakuachisha kuvuta sigara baada ya wiki tatu tu). Zitizameni kauli zenu,isiwe ukisema kitu hichi changu hichi chako, lazima mtumie kauli ya chetu, jueni kwamba ulimi kama mshale neno likisha kutoka halirudi nyuma, pia tambueni (Kwamba Ulimi umeumbwa na Mate kuteleza kazi yake)asiseme mtu kitu ndio ikawa sababu ya (Talaka), Fanyianeni (Surprise)Mnongoneze kwenye simu leo utakuta kitu kizuri, akija mpe ndizi mbivu alaa anataka nini tena, Fukiza nyumba yako, unajua maana ya kufukiza, ni kuondosha Tafrani na kuituliza akili, kufukiza ni dawa ya Akili, sio harufu nzuri pekee bali ni dawa ambayo kama utakua na desturi ya kufikiza kila siku utaona nyumba yako inavopata utulivu wa upendo. Ukimaliza toka wende ukanunue maua, unaijua siri ya Maua, Nini maua? Maua ni chembe ya mpenzi, ndio maana unaona Wapenzi wanapeana maua, Maua yana uwezo wa kutibu moyo ulojeruhiwa(Si unajua Nyuki anafonza Maua kutengeneza Asali) na unaelewa Asali ni Dawa, Na mimi nakwambia ipo dawa nyengine maua inayotoa nayo (Through Communion) Yamwage Maua ima chumbani au Ukumbini umualike mgeni mapenzi ili upate mafanikio yake.  Mwenzio kakaa kwenye sofa usende kukaa sofa la pili kaa nae, umemkuta mwenzio anapika kivamie kitunguu ukikate wewe, ukimkuta anakogesha watoto, basi wewe nenda kapige deki, unaona haya nini wakati Nabii Musa a.s kateka maji. Kwenye (Love)Mapenzi Akili (Mind)inatoweka na ikisha kutoweka hujali tena kama unaibiwa, au unajenga Ghorofa, wewe mfalme au unacheo cha Ubalozi, au umevaa Majuba ya Sheikh, hiyo ndio hali inayokukuta ukiteremkiwa na mapenzi. Ama yule alokua hana mapenzi yeye kutwa anapanga akuuibie vipi, atakudanganya namna gani, ukijiona umo katika hali hiyo jijue huna mapenzi ila wewe ni (Cheater)unamdanganya mwenzio na kujidanganya mwenyewe, na hakuna maradhi makubwa kama kujidanganya mwenyewe.Ikiwa kweli hamu yako na nia yako ni mapenzi na unayata kwa dhati,
Ukionekana msimamo wako huo Basi Mwenye enzi Mungu atakuteremshia hicho kiitwacho mapenzi, na yakisha kushuka hayo mapenzi ndio unapata hiyo (Eternal Happiness)Furaha ya mapenzi na ukiyapata hayo, wewe unayayuka kabisa (In love you Disappear only Beloved remain) unakua hupo kabisa, anobakia ni mpenzi, unafanya kila kitu kwa ajili yake, inakua raha moyoni mwako ukimuona mpenzi wako kafurahi, na hata huko kuona kunaondoka yeye anageuka kuwa wewe, na kama yeye pia anarejesha hayo mapenzi kama unavohisi wewe, hapo nyote wawili mnakua wabarikiwa nyote mnayayuka(Disappeared)na (Only love Remain)hapo yoyote atokuja nyumbani kwenu, atakae kuwa karibu na nyinyi anapata (viberation)ya mapenzi yenu, na hapo inapatikana salama mpaka ya vizazi vyenu kutokana na mapenzi mnayopendana na daima mnakua furahani, na penzi likishamiri mpaka siku zinapotea, hamuulizi hata wakati, (No time no limit)na mnapata ufunguzi wa muono wa mambo kwa njia nyengine kabisa, sasa mnajua kuwa kila kitu katika Ulimwengu huu ni mapenzi, tafauti yenu na wasopendana ni ile wao wanajua kupenda chakula, kupenda mtu, kupenda maji, nk, lakini nyinyi mnakua mnajua kwamba vitu vyote hivyo vinaishi ndani ya mapenzi kama mlivo nyinyi, na chengine kabisa mnachogundua kuwa mnayo (Raw Material)yaani hiyo (Sex Energy) Sasa mnafahamu kuwa tukipumzika tukapeana nafasi basi inakua siku tunayokutana ni kama siku ya sikukuu, na katika kipindi hichi cha mapumziko mapenzi yetu yanazidi sana, Sasa kuna siri gani ya mahusiano haya ya (Raw Material) na mapenzi? Endelea Part 4

FURAHA YA MAPENZI PART 4

Asalaam Aleiykum,

Siri iliyopo hapo nikuwa Ukipenda wewe una (Disappear)Mkipendana nyote mna(Disappear) penzi pekee ndio linabakia, na (When love Disappear)Penzi likiondoka halendi kokote ila linarudi kwa mwenyewe alolileta, na likirudi hapo ndio sasa linabadilika na kuwa (Taqwa)." وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةً۬ مِّنِّى "
"Nimekutilia mapenzi yanayotokana kwangu" (Maneno hayo anaambiwa Nabii Musa a.s)(Taha 39 mpaka mwisho wa aya) Na wewe utayapata kama utajitupa kikweli kwa Mollah wako, hiyo ndio ngazi ya tatu ngazi ya Taqwa, ukifika  katika Taqwa mapenzi yako yanabadilika kuwa (Blissful) kuwa (Joy plus Celebration) hapo tena siwezi kuhadithia nini kinatokea, hadith hazina maana tena, kumbukumbu hazitakiwi hapo, huwezi kutoa hadidu rejea, hapo unatokea mripuko wa mapenzi, mfano wa FashFash au (Fire Work)hapo inabidi ufike mwenyewe, na pahala hapo ndio  watu wanatumia kila mbinu na maarifa kupafikia na pametajwa baadhi ya mbinu wanazotumia Makasisi au Mapadri walotajwa katika sura ya (Hadid aya ya 27)

ثُمَّ قَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِم بِرُسُلِنَا وَقَفَّيۡنَا بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ وَءَاتَيۡنَـٰهُ ٱلۡإِنجِيلَ وَجَعَلۡنَا فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ رَأۡفَةً۬ وَرَحۡمَةً۬ وَرَهۡبَانِيَّةً ٱبۡتَدَعُوهَا مَا كَتَبۡنَـٰهَا عَلَيۡهِمۡ إِلَّا ٱبۡتِغَآءَ رِضۡوَٲنِ ٱللَّهِ فَمَا رَعَوۡهَا حَقَّ رِعَايَتِهَا‌ۖ فَـَٔاتَيۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۡہُمۡ أَجۡرَهُمۡ‌ۖ وَكَثِيرٌ۬ مِّنۡہُمۡ فَـٰسِقُونَ
Ikisha tukawafatishia nyuma yao Mitume wetu, Na tukamfuatishia Isa bin Maryam, na tukampa Injili, Na tukaweka upole na Rehma katika nyoyo za wale waliomfata, na Uruhubani (Wakutooa au Kuolewa)wameubuni(wenyewe)Sisi hatukuwaandikia hayo,(Waliyafanya haya wenyewe)ili kutaka Radhi(Mapenzi) ya Mwenye enzi Mungu, lakini hawakuufata(Huo Utawa)kama inavotakiwa kuufata, basi tukawapa wale waloamini miongoni mwao ujira wao, na wengi wao ni (W)maasi.
Hiyo ndio (Power of Sex) ukijidai kuizuia itakuadhiri na ukiichezea sana itakukashifu(Hapo havuki mtu) ila mtu afate muongozo wa Mollah wetu kuitumia (Energy) hii kwa uangalifu baina ya (Mume na Mke)tena kwa Mapenzi, hakuna njia nyengine ila utaingia hasarani.
Wako waloweza kuufata huo (Utawa) kikamilifu ndio wakaambiwa watalipwa kutokana na jitihada yao hiyo, Lakini Mwenye enzi Mungu hakututakia mazito anajua tunapata taabu, ndio akatuletea njia zake za mapenzi tuishi kwa Raha na furaha, Maisha yanatakiwa baina ya (Positive na Negative) Baina ya (Mke na Mume) ndipo yanapopatikana Mapenzi Kamili.
Mwisho sina Budi kunukuu maneno ya (Rumi)
God has placed a ladder before our feet, we must climb it, step by step.

Sunday, September 15, 2013

REHMA NA MATIBABU YA QURAAN PART 1

Asalaam Aleiykum,

Imeteremka Quraan na mambo makubwa manne ambayo yametajwa katika sura ya Yunus aya ya 57, lakini huwezi kuyapata mambo hayo au kuyajua kwa ufasaha mpaka upite katika Sura ya Aaraf aya ya 204 inayosema.
"وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ"
"Inaposomwa Quraan isikilizeni, Ikisha tulieni ili mpate kurehemewa"
Jambo la kwanza linalotakiwa kutoka kwako Usikilize, Na kusikiliza kwenyewe sio unasikia kila kitu, huyu kazungumza, mawazo haya na yale, hujamaliza kufunga hesabu, fulani kasema nini, hivo utakua sio kusikiliza bali inakua kusikia, Na kusikia kutwa nzima unasikia kila kitu, Gari imepita unasikia, Ndege wanaimba unasikia, watu wanazungumza unasikia, lakini kusikia huko hakuna faida yoyote inayopatikana, Na hata kukumbuka kutwa umesikia nini hutambui sababu hakuna maana kusikia huku.
Lakini katika kusikiliza unaingia katika shughuli ilokamilika na kupatikana (Totality) yako kwa ukamilifu au kwa lugha nyengine (Attention).Katika kusikiliza Quraan kuna kitu kinatokea na leo tunataka kukizungumza hicho ambacho kitakua madhumuni ya Darsa yetu pamoja na hayo mambo manne, Ili tupate kujua nini kinatokezea?, kwanini kinatoke, Na inakuwaje mpaka kikatokea, na inapatikana nini katika matokeo hayo.
Umo katika kupata Maalumati haya yazingatie kwa makini sana na uwe mtulivu ili upate kupata mafanikio na faida hii ya Quraan, Aya tulioitaja hapo juu mbali ya kusema Sikiliza pia imesisitiza kutulia, basi ikiwa umepata kuyaona maji mtungini au kisimani yalivotulia na hivo ndio unatakiwa na wewe utulie inaposomwa Quraan, Utulize Akili yako(Usiutingishe mtungi)utulie Mwili wako(Usikisumbue kisima)iwe hakuna (Movement)yoyote, shuwari kabisa, pasiwepo kishawishi chochote, anasoma uzuri,katia shada, mbona hakuvuta pale, au nikimaliza hapa nataka niwahi dukani, au mara umemsalimia huyu na mara useme na yule, hapo utakua ushatingisha mtungi na hupati faida yoyote na unakosa kikubwa zaidi nako ni huko Kurehemewa.
Nini Kurehemewa?
Kurehemewa kuko kwa aina nyingi sana, kuvuta pumzi kurehemewa, kusamehewa pia Rehma, kusikia nayo ni Rehma, kuona Rehma, mpaka kunyanyua kwako mguu na hiyo pia Rehma, Na mpaka haya ninayosema mimi na kuyaandika pia hii ni Rehma, wewe unayesoma pia umepata Rehma, hiyo ni kuonesha Rehma ziko nyingi na wanazipata viumbe vyote, lakini hili la Quraan kulipata lazima utimize shuruti yake nayo hiyo,(Usikilize na uwe Umetulia)huna mawazo yoyote kichwani, huna tafsiri yoyote, na hapo ndio utaweza kuipata hiyo Rehma.
Haiwezekani kuipata Rehma kwa njia tuifanyavo hivi sasa, kama vile imegeuzwa kitabu cha kufanyia mashindano, (najua mashabiki watakuja na nguvu za hoja chungu nzima)kutetea wanavo fanya lakini siwezi kukaa kimya, lazima niseme sio kusudio lake, haikuletwa Quraan hii ili mtu apate kupata zawadi, imeletwa ili mtu apate Rehma, Kimegeuzwa kitabu hichi ndio njia ya (Past Time)nikiendesha gari ntaisikiliza, na wako watu hawasikilizi mpaka asome Sheikh Fulani, ndio anamkosha mpaka anapata usingizi, wengine wanasema siwezi kupika mpaka nitie Quraan, huku nasikiliza na huku napika, vipi unadhani Rehma itapatikana, ikisha unasema haikai hata aya moja siwezi kuhifadhi, vipi utajua maana yake na wewe huna utulivu, vipi utaipata nuru wakati hutaki kutoka kizani, sasa ukivipata viwili hivyo nini kinatokezea? Endelea part 2

REHMA NA MATIBABU YA QURAAN PART 2

Asalaam Aleiykum,

Umeshatulia kwa makini kusubiri nini kinatokezea, tukio gani la maajabu linakukuta mpaka ukaridhika na kusema ama kweli haya mambo sio bure, hivi ndivo inavokua, hivi ndivo inavotibu, namna kama hii ndio unapata Mawaidha, na kwa sababu hii ndio ina niongoza, na sasa nimeshagundua Rehma yenyewe basi kuanzia sasa sitoihama tena Quraan. "Yunus 57"

"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٌ۬ مِّن رَّبِّڪُمۡ وَشِفَآءٌ۬ لِّمَا فِى ٱلصُّدُورِ وَهُدً۬ى وَرَحۡمَةٌ۬ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

"Enyi Wanaadamu yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mollah wenu, Na dawa katika yale yaliyomo kwenye vifua vyenu, Na muongozo na Rehma kwa walioamini"
Umepatikana uzuri wa kuonesha mpangilio wa ufanyaji wa kazi yake hii Quraan katika hiyo aya ya 57 ya Sura ya Yunus, Na kama tulivoona mwanzo imeanza na Wanaadamu wote na mwisho ikachagua (Select) kwa walio Amin pekee. Sasa mambo gani yalotajwa hapo ambayo leo yatupasa tuyaangalie kwa undani ili tupate maana halisi ya maneno haya tuweze kuyafanyia kazi.
Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mollah wenu, Nini Mawaidha? Mawaidha ni Nasaha, kujulishwa kwamba katika Ulimwengu huu unatakiwa ufanye jinsi kadhaa wa kadhaa ili upate kuishi kwa salama, Usiibe ujue ukiiba na wewe utaibiwa na kama hujaibiwa basi jua utateseka kwa njia nyengine kama sheria za mwizi zinavoamrisha, Na kukatwa mkono kuna dhahir na siri, unaweza usikatike mkono lakini ukakatiwa biashara, sasa kama mkono ulikua ukinyooka sasa haunyooki tena, Usidhulumu utadhulumiwa na kama hujadhulumiwa aloleta Nasaha hizi ataingilia kati kwa namna anoijua yeye ili na wewe Udhulumike hapa Ulimwenguni na huko Akhera uendako. Lazima Amri  ya Hukumu ipite midamu keshaleta Nasaha na nyinyi hamkuzifata, Na ukipinga Sheria za Mollah wako na ukayadharau Mawaidha yake, ukapinga Nasaha zake, kama unavofanya kila siku, yanapita huku yakitokea kule hata sikio halishituki, imekua Quraan haifanyi chochote juu yako ndio akasema Mollah wako na kukupigia mfano huu wa aya ya ( 21) sura ya ( Al-Hashr)
"لَوۡ أَنزَلۡنَا هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ عَلَىٰ جَبَلٍ۬ لَّرَأَيۡتَهُ ۥ خَـٰشِعً۬ا مُّتَصَدِّعً۬ا مِّنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِ‌ۚ وَتِلۡكَ ٱلۡأَمۡثَـٰلُ نَضۡرِبُہَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ "
"Lau kama tungeiteremsha hii Quraan juu ya Mlima, Ungaliuona ukinyenyekea na kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenye enzi Mungu, Na hii ni mifano tunawapigia wanaadamu ili (wapate)kufikiri"
Wapi leo hutaki hata kufikiri,inasomwa Quraan msahafu mzima ikimalizika unapiga makofi na hata (Mashaallah)inakushinda unasema (well done).
Sasa Vipi Inatibu?
Hilo ni ponyo(Dawa) kwa yalio vifuani mwenu, Matibabu yapo ya aina mbili yaani (Physical and Mind) na wataalamu wanatwambia 90% ya maradhi yetu yanatokana na Akili(Mind) na 10% ilobaki ndio hiyo (Physical) Quraan inatibu  hayo yote mawili, vipi inatibu au huko kuponesha, itabidi urudi nyuma mwanzoni kabisa kwenye maudhui hii ili upate kujikumbusha pale ilipotajwa  (kusikiliza na kutulia) Kusikiliza kunatokana na Sauti (Sound) kabla ya kuendelea nataka ujijue wewe mwenye umeumbwa kwa udongo utoao sauti (Al-Hijr 26)"وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن صَلۡصَـٰلٍ۬ مِّنۡ حَمَإٍ۬ مَّسۡنُونٍ۬"
Na tulimuumba mwanaadamu kwa udongo mkavu unaotoa sauti, unatokana na matope meusi yalovunda.
Na hiyo sauti ndio mnatumia kufanya (Communication) na mambo mengine kama itavo onekana sehemu ya tatu.
Endelea Part 3

REHMA NA MATIBABU YA QURAAN PART 3

Asalaam Aleiykum,

Hii Quraan Inatumia Sauti(Sound)na ukimya wa Sauti(Soundless)kufanya utibabu wake, Na hiyo Sauti nyenzo yake kubwa za kutendea kazi yake ni (Air)upepo na (Water) maji, kumbuka wewe mwenyewe 85% ya (Body)mwili wako umetawaliwa na maji, na upepo unahitajika(Oxygen) kwa (Supply)ya vilivyomo kwenye kifua chako.
Quraan inatibu kwa kutumia (Secret coded massage) zilizomo kwenye sura au aya kukutibu wewe maradhi mbali mbali ima iwe kwa kusomewa au kwa kuandikwa, yote hayo yanatoa huduma zake kwa yule mwenye kufanyiwa, Na kwanini isiwe hivyo, kwanini unabisha, wakati unafahamu kuwa sauti hiyo hiyo ukiambiwa mtu wako wa karibu amefariki(unatoka na machozi) na ukiiambiwa amepona maradhi(Unafurahi), nini kinatokea hapo, wewe uko mbali hujawa shahidi wa hayo yote mawili lakini sauti inakubadilisha, sasa ikiweza kufanya kazi hiyo kwanini isiweze kufanya kazi ya kukupa ponyo kwa yaliyomo kwenye kifua chako.
Kumbuka aloleta Mti shamba ukutibu ndio yule yule aloleta hii Quraan na Muujiza wake wa hayo Mambo 4 niliyoyataja, na ukichunguza utagundua hayo na utakutana na mshangao mkubwa nikikwambia kuna sura zikisomwa kwa sauti maalum kama mgonjwa taabani basi inafanyika safari yako ya (Umauti)kuwa nyepesi na ya haraka, elimu hiyo inaitwa (Burdai)na mpaka leo wako wachache walo nayo huko Zanzibar.
Hivyo ndio yanavopatikana masomo haya ya Quraan kwa yule mwenye kujua asome kitu gani kukutibu kitu hayo maradhi, na inayopatikana hapo ni hiyo (Combination of sound)na matamko ya aya yaliyomo kwenye hiyo aya, na pia inategemea mjuzi wa elimu hii na ufahamu wake wa kutumia elimu hii ya Kitabu hichi.Usije ukaondoka hapa na kutaka kusoma kimafamba, ndio yatakukuta ya yule alotaka pesa na kusoma (Surat-masad-Lahab).
Na huo Muongozo ambalo ni jambo la tatu ni ndio huo wa kukutoa kwenye giza na kukupeleka kwenye nuru, kukufahamisha mabaya ukayaepuka na mazuri ukayafata, kutujulisha kwamba kuna moto na pepo vinatusubiri, vipi tumuabudu Mollah na kuwatendea wema, wazee na watoto, maskini na mayatima, wajane na waloharibikiwa katika maisha nk, Muongozo wenyewe ni hii dira ya Uislam ambayo tunaifata, na kama utaifata ipasavyo hutoweza kupotea.
Na Rehma hii ya Quraan imetengewa (Special)kwa waloamini, Rehma ziko nyingi na viumbe wote ni wenye kuzipata, lakini hii ya Quraan inatokea kwa Muumin pekee, hii ni hususia kwa kuwa kuna kitu kinatokea, unapatikana mripuko fulani ndani ya nafsi yako na huo haupati kila mtu, na chunguza pale inaposomwa Quraan umekaa wewe na Muislam mwenzako lakini yeye ana Iman hafifu na dini yake, si mwenye kuitaka Quraan, wala hashughuliki nayo, inaposomwa wewe kinaingia kitu fulani moyoni, hiyo ndio Rehma, hicho kinacho kuingia inaweza kua ponyo(Dawa)au muongozo au Nasaha, na hiyo ndio (Rahman Rahiim) inaweza kuwa chochote, wewe sikiliza tulia wacha yende ndani ikapasue, haikuumizi ila ni Rehma tu, na yule mwenzio aliyekuwepo hapo hapati chochote anaona kitabu kama vilivyo vitabu vyengine.
Nakuomba uelewe kama wewe Muumin uzidishe juhudi sasa ushiajua siri yake hii Quraan, usikubali tena ikasomwa au kuisoma mwenyewe ukawa una mawazo mengine, tulia usikilize ili uzipate hizo Rehma, na kidogo kidogo ukifatilia utakuja kuyaamini maneno yangu, nazungumza katika uzoefu sio katika ukanda wa kusikia. Tulia usikize uyapate mambo hayo 4 pamoja utakua mwenye kufanikiwa, utakua umehifadhi kitu kikubwa ndani ya Moyo wako, Na daima utatembea na Rehma hizo za Quraan. Mollah atujaalie kusoma na kufahamu, atukirimu kusikiliza na kutulia ili tupate Rehma zake. Amin.

Sunday, September 8, 2013

HEKIMA YA UZEE PART 1

Asalaam Aleiykum,

Hudhuria aya ya 269 ya sura ya Al-Baqara ukutane na maelezo ya Quraan yenye kuhusiana na mafunzo ya Hekima na ukumbusho wake, "

"يُؤۡتِى ٱلۡحِڪۡمَةَ مَن يَشَآءُ‌ۚ وَمَن يُؤۡتَ ٱلۡحِڪۡمَةَ فَقَدۡ أُوتِىَ خَيۡرً۬ا ڪَثِيرً۬ا‌ۗ وَمَا يَذَّڪَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَـٰبِ
"(Mwenye enzi Mungu)"Humpa Hikima amtakaye, Na aliyepewa Hekima bila ya Shaka amepewa kheri nyingi(Kitu cha thamani)Na hawakumbuki ila wenye Akili.
Yametajwa maneno haya  mawili ili kuonesha nini hikima na ipi Akili, na imepatikana tafsiri ya wazi pale iliposemwa hawakumbuki isipokua wenye Akili.
Nini Hekima? Najua hutoshangaa nikikwambia Uzee ni kifo (A very slow death)Kifo hichi kimeambatana na Uhai, kila siku Unakufa na kila siku unaishi, na ndani ya huo Uhai ndimo inaishi hiyo Hekima, na katika hicho Kifo kinabakia hiyo Akili, Na Akili ina kazi mbili ima  kukumbuka ya Zamani (Death) au Kukumbuka mepya(Life)yenye kuishi wakati huu tulonao.
Leo hii imeniwajibikia juu yangu kukusaidia ili ukumbuke na upate kuzingatia japo kwa uchache hicho kifo cha Akili na kuzaliwa kwa Hekima ambayo inakusaidia kuona vipi unapita katika Mauti haya ya Aina Mbili. Watu wengi wameghafilika na kitendo hichi cha Umauti ambao uko wazi na sote ni wenye kushuhudia, lakini labda tumejitoa fahamu au kwa ukweli kabisa tumelala usingizi mzito na kutofahamu nini kinaendelea. Ama kifo cha Mwanzo chenye kutokea ni (Physical Death) Na hili limetajwa katika sura ya Yaasin 68 "وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَڪِّسۡهُ فِى ٱلۡخَلۡقِ‌ۖ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ"
"Na tunayempa umri(Akawa mtu mzima)tunamrejesha nyuma katika Umbo(Uzee)Basi hawayatii Akilini(Kuyafikiri)"
Huko kurejeshwa nyuma ni kupita katika (Process)ya Kifo, kifo chenyewe kwanza ilikua (Foward) sasa imekua (Reverse) na vyote hivyo vinapita katika jambo hili moja la kudumu, jambo la milele nalo hilo (Life) au Maisha, na katika hayo maisha ndipo inatokea hiyo (Hikima) ambayo inashuhudia vifo vyote viwili cha mwanzo (Physical) na cha Pili (Mind), Kijue kifo cha mwanzo kinatokea vipi?
Kina mambo haya yafatayo:Ambayo yanakutokea unayajua, unayaona lakini bila  kutumia (Hekima)
(1)Kupungua kwa pumzi/kuchoka, (2)Kupungua kwa Nguvu(3)Kupungua kwa Usingizi(4)Masikio kutokusikia Uzuri(5)Macho kupungua Nuru yake(6)Kupunguza Kuongea(7)Kuwasili kwa Maradhi(8)Kukunjika kwa Ngozi(9)Mifupa kuwa Dhaifu(10)Kungoka na Meno(11)Na Kupotea kwa Sex(Matamanio)
Kinakutafuna kifo hichi mpaka ufikie Umri wa Miaka (7x6=42)au Umri wa Miaka 40 na 42 ndio unafikia hichi cha pili ambacho unashuhudia (Death of Mind)Kifo cha Akili, ambacho mambo yake ni haya:(1)Kuanza kuona Mabadiliko(2)Kupungua kwa (Social activity)(3)Marafiki wanatoweka(4)Ukenda Disco au Taarab unakua wewe wa mwanzo kuonekana(5)Vivazi vyako vinakua tafauti(6)Fikra zako zinakua za Woga(7)Akili yako inakua haina uwezo tena kuhimili mafunzo mepya(8)Kwa kuwa ushafikia kikomo unabaki kungangania Historia(9)Unakua Mkaidi(10)Hufurahi na chochote na hata kama kufurahi ni kujionesha tu(11)Hupendezewi na kufurahi na wenzio(12)Umechoshwa na maisha(13)Unatamani Maisha ya Vijana(14)Unafilisika Kifikra(Maarifa) Sasa kutaka kumjua Mwenye hekima ni kumgundua yule alopata ku(Jump) au (Chance) ya kuipata hiyo Hikima na yeye akaichukua na kuitumia ipasavyo, na kila mmoja anapewa nafasi hii, wako wanopewa mapema ambao ni wachache sana, na hupewa baina ya miaka 28 na 35, na ukipata Fadhila hii unakua umepewa Fadhila kubwa kabisa na Mollah wako, unageuka kuwa mtu mwengine kabisa, kwa sababu Hekima (Wisdom)sio (Knowledge),Elimu wanafundisha watu kama wewe, zimejaa kwenye vitabu, ni kama (copy). Lakini Hekima (Wisdom)Inatokea kwa Mollah wako, ni kitu ambacho (Beyond Education)Kwenye (Wisdom)kuna kitu kimetokezea na wewe kwa furaha una (Share) na wenzio.Sasa kutaka kuijua hiyo Hekima endelea Part 2

HEKIMA YA UZEE PART 2

Asalaam Aleiykum,

Na Mwenye kupata hiyo hekima ndio anakua na uwezo wa kuvishuhudia kwa Ukamilifu vifo hivi viwili vinavyotokezea cha mwili na cha Akili, Mwenye Hekima anacheka, mwenye Hekima ana furaha, anaridhia kwa kujua kuna kitu chenye Thamani kushinda viwili hivi.
Sasa Unakuwaje ukiipata hiyo Hekima(Wisdom)?
Kitu cha kwanza kabisa unakua mwenye Furaha sababu hekima na (Happiness)vinaenda sambamba, sababu hata dhiki ikiwepo wewe unaiona kwa upeo mwengine, Na kubwa katika hilo unakua unaishi katika (Level)nyengine ya (Consciousness) sio ya (Mind) tena.
Kwa ajili ya kuishi kwako kwenye (Consciousness)unakua una uwezo wa kushiriki(Level)zote za jamii, ukiwa kwenye kundi la watoto wanakuona mwenziwao, ukiwa na vijana wala hawababaiki wanajua unawafahamu nyendo zao,Ukiwa na Wazee wanakuhisi wewe Mmoja katika wao, Kila anaye kuona anataka ushauri kutoka kwako kwa sababu wanavutika na Hekima zako, Kila anaekuheshimu na wewe unamuheshimu, Kila ukionekana upo kwenye furaha, Na hiyo ndio alama kubwa ya Hikima(Wisdom) ambayo inatokea inapotokea Afya,Furaha,Msiba na Kadhalika.
Mwenye Hekima Hawi Muongozaji bali anakua Muelekezaji,Mwenye Hekima anakua mwepesi kukiri kosa lake, hawi mshindani,wala si mwenye kutafuta ushindi, ila yeye anakua Mja wa subira.
Mwenye Hekima Maradhi na msiba vikija anaviangalia sababu kashatambua hivo vitu viko vinakuja wala hana uwezo wa kuvizuia, Maradhi yakifika haya muhuzunishi, Kifo kikikaribia anaelewa sasa wakati ushafika wa kuondoka kikamilifu kwenye huu Mwili(Body).
Marafiki wakipungua anajua sasa ni wakati wa kumtafuta yule Rafiki yake Mkubwa aliye hai Milele wala simwenye kumkimbia, na huyo ni Mollah wake Muumba.
Mwenye Hekima daima anakua na Fikra mpya, na wala haogopi mambo mepya, anakua sio mkaidi wa kupinga kila jambo, anafurahi akiona wenzie wanafurahi, Mwisho kabisa mwenye Hekima anao ujuzi wa kujua kwamba matamanio ya (Sex)yakitoweka basi (Energy)hiyo sasa inakua (Transformed to Love)inageuka mapenzi, anakua Mtu huyo mapenzi matupu, sasa hana Dhara kwa yoyote yule, akishauriwa mambo ya hatari anasema laa msifanye, pakitaka kutokea dhara anakua wa mwanzo kuiepusha.
Sasa soma Part 3 Umuhudhurie yule asokua na Hekima anakua hali gani?

HEKIMA YA UZEE PART 3

Asalaam Aleiykum,

Mtizame yule ambaye anaishi kwa  kutumia Akili, Vitizame visa vyake, kitu cha kwanza (Sex)Matamanio yakimalizika, sasa wewe ushachoka, wacha hizo nguvu zilobaki kidogo tuzigeuze kuelekea kwenye mapenzi, laa bali utamkuta anahangaika kwenye maduka ya madawa kutafuta dawa za kumtia nguvu za matamanio, anagombana na (Nature)makadirio ya Mollah wake, kwa sababu kanasa kwenye akili anakumbuka zamani kwa hiyo ana nasa kutamani (ndogo ndogo)ukimuona mtu kama huyo elewa hekima haijawasili hapo au kuzaliwa kwenye kichwa hicho.
Asiyekua na Hekima utamuona anapinga kila mabadiliko, mchunguze kiongozi wako utagundua hayo, popote pale ikiwa msikitini au kwengineko utaona wimbi hili la Akili linavopoteza watu, Utawaona wamebaki kwenye Historia na mambo ya zamani, siwenye kutaka maendeleo wa mabadiliko yoyote yatokee, wanangangania madaraka lazima waongozee sababu hekima hakuna, Na wanahofu kama hawaongozi watafanya nini, na hofu yote hiyo wanaona (Sex)inapotea (Wisdom)wakati wake ushapita, marafiki wanatoweka hawapo tena, maisha ya upweke yanatisha mtu peke yako, wana hofu watafanya nini na ukweli ushawadia, ndio maana wanakua ni wenye kupinga kila jambo, wagumu kukubali chochote kile, Na (Sex)ikipotea watageuka kuanza kulimbikiza mali, na akitokea kijana ana mawazo mepya atapingwa na kuzuliwa kila aina ya Fitna, na sababu kubwa hawana hekima, hawana mawazo, wamefilisika na wamefikia kikomo cha fikra, na sasa wameshindwa kuchupia  Meli ya Hekima, utaona mazungumzo yote zamani tuliamua hivi,historia ilisema hivi, zama zilopita tulipanga hivi, hawataki kabisa kusikia, wenye hekima wanasemaje, sasa tufanye vipi, na siku zijazo tufanyeje.
Watizame waso hekima walivotawaliwa na hasira, chuki, mashaka ya maisha, na mwisho kabisa uchu wa nguvu za kutawala chochote kile iwe paka au mwanaadamu, sasa ikiwa unataka kujijua labda hekima imekuingia au kukushukia au imo mbioni kuchipua au unataka nikusukume kwenye bonde la hekima itabidi ujifanyie mtihani wa Hekima wewe mwenyewe, ili upate kujijua kama unayo mbegu ya hekima na uzidishe subira basi muombe mtu akuulize swali (Random),liwe la Dini au Siasa au la Kisomi, halafu tizama vipi utalijibu, ukitaka kutafuta (Refrence)au Hadidu Rejea basi jijue wewe bado, wewe ni (Copy)bado ni (Chori chori)lazima uibe pahala, hotuba lazima uandikiwe, basi jua bado Hekima haijafika, huna kitu, sio (Original)hakuna kitu kinachotokea katika (Being)yako, Lakini Mwenye Hekima(Wisdom) anajibu (Direct)hataki (Copy) hendi kwenye (History)hatumii Akili ila anatumia (Consciousness)yake. Na hiyo ndio Hekima, na huo ndio Uzee wenye manufaa,Na ukimuona mtu kama huyo mfanye Rafiki yako na wewe ufaidike kwa sababu ana kitu si kutoka kwenye Ulimwengu huu. Namuomba Mollah atujaalie Hekima itokanayo kwake. Amin.

Sunday, September 1, 2013

KWANZA KA HAJJ MOYONI IKISHA UKAHIJJ MAKKA PART 1

Asalaam Aleiykum,

Anayekusudia kwenda Mji Mtakatifu wa Mecca anakua na dhamiri ya kutenda Ibada ili kutimiza nguzo ya Kiislam ya kuitikia wito wa Mollah wake, Unapotaja nguzo umeshatia maana ya kua umeijenga kwa imara na kuweza kuhimili vishindo vyote, Ima viwe vya Kimbunga, au Mtetemeko wa Ardhi, au mvua na mafuriko, ikiwa kimoja katika hivyo chaweza kuiangusha nguzo yako basi elewa nguzo hiyo sio imara, Na wala usipate taabu kuijenga kwa nyumba ya Hajj itakua umeingia hasarani.
Sasa vipi Utajua kama nguzo yako Imara au imejengwa kwa matope matupu, Na hivyo vitu nilivovitaja hapo juu vya (Mafuriko na Mitetemeko ya Ardhi) ni hayo mambo yanayokutoa kwenye Ibadah au Ucha Mungu, na kuijua kama nguzo yako ni Imara inakubidi ufanye Hijja hiyo ya Moyoni, uende ukamuulize (Civil Engineer) jee Nguzo yako inaweza kuhimili Zege la Ibada, Na hutopata Muhandisi aliyebobea katika jambo hili la Ibadah kama ulivo Moyo wako, umefikiwa mpaka kutajwa na Mollah wako, Vipi?
"إِلَّا مَنۡ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلۡبٍ۬ سَلِيمٍ۬"
Isipokua atakae kuja kwa Mwenye enzi Mungu na Moyo safi.
Moyo ulosalimika  Amekwisha (Surrender) kawa na Alama nyeupe, nini nyeupe? Ukiichunguza Rangi nyeupe utakuta ni mkusanyiko wa Rangi zote ndio unaoifanya Rangi kuwa Nyeupe, Nyeupe ndio hiyo (Light) Nyeupe ndio hiyo (Nuru)Nyeupe ni hiyo (Peace)katika moyo wako, umeshafanya mambo yote sasa unasema mimi basi,  mimi najisafisha na taka zote za moyo, na hakuna kujisafisha kuliko na ukamilifu kama huku kwenda Hajj, Lakini haupatikani ukamilifu huo mpaka kwanza uka Hajj kwenye Moyo wako.
Haipatikani Hijja kama Moyo utakua bado una machafu, hatukatai utakwenda Mecca lakini sio Makka, Utakwenda (Holiday)lakini sio (Holyday)lazima uzitafute tafauti zake uzijue, na tafauti yake ni kubwa sana baina ya maneno hayo na matendo yake, nini Tafauti yake? Unakwenda Makka, Maharusi yamekujaa moyoni lazima nikirudi nirushe Roho, unakwenda Makka ukirudi lazima Ujenge nyumba ya tatu, Unakwenda Makka lazima ukirudi ushinde Udiwani, Unakwenda Makka ukirudi watakutambua lazima uwapandishe Mahakamani, Unakwenda Makka unasema fulani lazima umpate, Unakwenda Makka unatoa Ahadi nikrudi nitakusaidieni lakini mniwekee zawadi yangu, unakwenda Makka ukirudi unahudhuria Sherehe za Taarab, Unakwenda Makka fulani hujamsamehe na wewe hujasamehewa, Unakwenda Makka huzungumzi na Fulani, Unakwenda Makka Familia yako inateseka na Njaa, Unakwenda Makka umechukua Mkopo, Unakwenda Makka umefurika Mali za wizi, vipi wewe unakwenda Makka, Sasa huko Makka Uende vipi? Endelea Part 2

KWANZA KA HAJJ MOYONI IKISHA UKAHIJJ MAKKA PART 2

Asalaam Aleiykum,

Kwanza nenda kafanye Hijja kwenye Moyo wako, hilo ni jambo la mwanzo linalotakiwa, sio kuonesha watu na wewe umekwenda Makka, hudhuria kwenye Moyo uondoshe Chuki, uondoshe Tamaa, Ondosha fitna moyoni, Sahau majeraha yalokupata, Rudisha mali uliyodhulumu, Wasemehe waliokukosea na pia omba usamehewe, Nenda (Deep) kwenye kisima cha Moyo wako anza kupenda walokaribu yako, watakie mema, waonee huruma, anza kujipenda mwenyewe kuwa umefanyiwa ukarim wakuweza hata kufikiria kwenda kuhudhuria nyumba ya Mwenye enzi Mungu, Wapende Maskini, Upende Ulimwengu na vilivyomo ikisha fungua Moyo ushukuru ya kwamba uko hai na unajitaarisha kwa safari hii Tukufu ya kwenda kwenye nyumba ya Mwenye enzi Mungu, Omba mapenzi ya Ucha Mungu yakushukie, fanya hima kwa kipindi hicho cha kusubiri uone nini kinatokea katika Moyo wako, jitizame mwenyewe kwa siri jee nabadilika, niko tayari mimi sasa kwenda Hajj, na kama muangalifu utayashuhudia mabadiliko yanatokea taratibu na utauona moyo wako unasafika, hamaki zinapungua, unakua mwenye huruma, husda inakatika, unaona mambo kwa mtizamo mwengine kabisa, unakua mpole, Imani na ukimya unakutawala, unapenda kusaidia wenzio, ukiona dalili hizo zimekushukia sasa wewe tayari ushakamilisha Hijja ya Moyoni na wakati wowote sasa moyo unaweza kushukiwa Miujiza kutoka Mbinguni, sababu umeshakua msafi, na sasa uko tayari kwenda kwenye hiyo Hijja ya nje, Hijja ya Kuhudhuria Nyumba ya Mollah wako Duniani, Pahali walipoishi viumbe watukufu katika (Historia) ya Ulimwengu huu, wakaacha mifano na (Special-Energy)zao mpaka leo zina (Viberate) Sasa funga Safari ya kwenda kwenye Mji huo, huku unamuendea Mollah wako na Moyo ulosalimika.
Endelea Part 3

KWANZA KA HAJJ MOYONI IKISHA UKAHIJJ MAKKA PART 3

Asalaam Aleiykum,

Sasa Nenda Makka uko huru wewe msafi, ondoa shaka ingia kwenye mji huu ukiwa na Imani utapokewa kwa mapenzi na Mollah wako, huku machozi yakikumiminika.
Al-Imran 96-97,
"إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٍ۬ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِى بِبَكَّةَ مُبَارَكً۬ا وَهُدً۬ى لِّلۡعَـٰلَمِينَ"
Kwa hakika Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili watu(kufanya Ibadah)ni ile iliyoko Makka, yenye Baraka na Uongozi kwa ajili ya Walimwengu wote.
Sasa ushabadilika na umekua msafi nenda kwenye nyumba hii ya Ibadah, Ikiwa umeweza kuhijj kwenye Moyo wako ukagundua mambo yanotokea kwenye nafsi yako, basi sasa itakua rahisi pia kuyaona na kuhisi Baraka za mji huu wa Makka zinavoshuka, Na Baraka zipo za aina nyingi, Machozi yakikumiminika elewa hizo ni Baraka, Kuona siri za mji huo hiyo ni Baraka, kukubaliwa Ibadah zako hiyo ni Baraka, na huo Uongozi ni kuhudhuria kwako sehemu hiyo na kupata jina maalum la kukumbusha kuwa wewe ulokwenda ni kiongozi wa mfano kwa wenzio wote walokua bado hawajenda kwenye mji huu Mtukufu wa Makka, kwa hiyo ongoza kwa Mfano, sio ukirudi tu unakua kama walokua hawajenda, unakua kiongozi wa Rusha Roho, kiongozi wa mapambano ya siasa, mkuu wa upokeaji Rushwa,Mdhalilishaji wa viumbe wenzio, utakua huna Hijja na ni muflis kabisa.
"فِيهِ ءَايَـٰتُۢ بَيِّنَـٰتٌ۬ مَّقَامُ إِبۡرَٲهِيمَ‌ۖ وَمَن دَخَلَهُ ۥ كَانَ ءَامِنً۬ا‌ۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلاً۬‌ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ عَنِ ٱلۡعَـٰلَمِينَ"
Humo mna ishara zilizo wazi, mahali alipokua akisimama Nabii Ibrahim (a.s) Na anayeingia (Mji Huo)anakua katika Salama, Na Mwenye enzi Mungu amewajibishia(Wajib) watu wafanye Hijja katika Nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko,  Na atakae kanusha(Kupuuza), Basi Mwenye enzi Mungu si Muhitaji wa Walimwengu.
Katika mji huu kuna Ishara zilizo wazi lakini mtu anakwenda mpaka anarudi hazioni wala kuzihisi mpaka anarudi, vipi leo atagundua zilizofichika, na yoyote yule anayeingia  mji huu keshaipata Salama kutokana na hiyo(Special Energy) ya mji huu, vipi unaipata salama hiyo?.
"Anahadithia Jabiri r.a" "Kwamba Bwana Mtume s.a.w "Kasema hakika hii nyumba ni (Alama)nguzo katika nguzo ya Uislam" Mwenye kuhijj au kufanya Umra anaipata Dhamana kutoka kwa Mollah wake, Atakapokufa anaingia peponi,(Ndio maana nikakwambia kwanza Kahijj moyoni)usije ukenda na kesi za kudhulumu na mauaji ukategemea utachukuliwa Dhamana, Na akirejea kwa watu wake anakua mwenye ujira kwa Mwenye enzi Mungu, na Baraka (Zinamiminika)". Jua wewe unarejea na Baraka maalumu umepata Special (Energy) basi fanya ubaki nayo kwa kuwa Mcha Mungu. Na akaendelea kusema Bwana Mtume s.a.w "Anaekufa njiani ikiwa anakwenda au anarudi akawa (hajachafua hijja yake kwa jambo ovu au kuondoa heshima yake)Basi Humsamehe Mollah wake" Na kwanini usisamehewe na wewe ushajisafisha kabla ya kwenda na ukiwa unarudi. Na hiyo ndio Hijja unayotakiwa uitekeleze kuitikia wito wa Mollah wako useme:
Laabaiyka Allahumma Laabaiyka Laa Sharika Laka Labaiyka.
Mollah awakubalie wote wenye nia ya kwenda kufanya Hajj na warejee kwa salama wawe wenye mafanikio na kuishi na hizo Baraka.Amin