Asalaam Aleiykum
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umewasili hutopenda nikakupa kitu kipya ili ukitumie kwenye Mwezi huu upate kuiona tafauti kwenye Funga yako, Hutaki nikupe siri ya (Mawalii) wanavoishi katika Mwezi huu, basi kama unataka Fatilia Darsa hii ili ukifunga Mwaka huu uwe umeipata (Saum)yako kwa Mtazamo Mwengine kabisa.
Kwa Kukufahamisha hayo, nia yangu ni kukutaka uitizame Ramadhani kwa mtizamo wa kila Pembe. Tunaishi zama za (Google) kila mtu anataka aitizame Ramadhani kwa upande wake, kama vile unavotizamwa mwezi wa muandamo, Na mimi ntaendelea kukuonesha pembe hizi mpaka pale utakapo ipata Ramadhani kwa ukamilifu, kwa sababu sasa hivi umegawika mapande mawili,unaweza ukaipata kwa maana, na kuna wengine wanakosa maana wanapata kwa vitendo, kwa hiyo kwenye Ramadhan lazima viwili hivi vikutane, lazima ufunge kwa Maana na vitendo, ntakuonesha vipi inafanyika.
Kufahamu kwa ufasaha wacha tuanze Darsa yetu kwa kuchemsha(Akili)sio(Bongo). Napenda kukujulisha tafauti ya Wanafunzi(Student's)na(Disciple's)Wafuasi, Wanafunzi wanaweza kuwa wengi wanakuja wanasoma wanakusanya (Information) ikisha wanakwenda zao, Wala hawakumbuki Shule(School) au Walimu wao, Kwa kuwa hawakumbuki hata akipita njiani mara chache sana kumsalimia Mwalimu. Lakini Mfuasi yeye anakua karibu na Maalim, anamshiba Sheikh wake, anakaa nae kwa karibu zaidi na mahusiano yao yanakua ya (Communion) hayakatiki ila kwa kupatikana sababu Maalum, Anapata Mfuasi huyo mafundisho, anafundishwa mambo, anazijua kanuni ndio maana neno (Discipline) limetokana na (Disciple)Nidhamu, kwa hiyo unapoitwa Mwanafunzi jijue wewe nani, na unapoitwa Mfuasi ujijue cheo chako kikoje(Tafauti yake mmoja anasomeshwa na mwengine anafundishwa). Hayo ni ya Mwanafunzi na Mfuasi, sasa nini tafauti unapoitwa Muislam na unapoitwa Muumin.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment