Tuesday, May 29, 2012

SALA YA TASBIH

Asalaam-Aleiykum Ameagiza Bwana Mtume s.a.w tuipate sala hii ya tasbih ikiwa tutaweza basi tuisali kwa siku mara moja, Au kama hatuwezi basi iwe kila ijumaa na kama haiwezekani basi hata kwa mwezi mara moja, na kama hivo pia ni ugumu basi tufanye mwaka mara moja, na kama hatuwezi kabisa basi angalau katika umri wako uipate mara moja. Imekua Sala hii akiipata muumin basi husamehewa Dhanbi zake zote, kwanini ikawa hivo, kwa sababu hiyo ni sala pekee inoweza angalau kwa mara moja ukapata bahati ya kuipata hicho kitu kinachoitwa sala, kwa sababu ya shuruti za idadi ya hizo tasbih za dhikr zilizomo humo, hupati nafasi ya kufikiri Bank, au kuwaza nyimbo za tarab, au kukumbuka mambo yako ya mipira,Jaribu uipate utaona ladha ya sala hii. Vipi inasaliwa? Utasali Rakaa nne,na kila kwenye Rakaa Utasoma Suratil fatiha(Alhamdu)na sura nyengine yoyote ile uitakayo,utakapomaliza kusoma hali yakua bado umesimama utasema maneno haya(Subbhana-Allah-,Walhammdulillah-wallah-illah-illah-Allah-wallahu-Akbar)mara kumi na tano(15), Ikisha utarukuu utasema mara (10)halafu ukinyanyua kichwa kutoka kwenye rukuu utasoma mara (10),Ikisha utakwenda katika sijda utasoma mara (10)ikisha ukinyanyua kichwa kutoka katika sijda utasoma mara (10)Ikisha utasujudu tena utasoma mara (10)na ukinyanyua kichwa kutoka katika sijda utasoma mara(10)na hivo utakua umepata mara (75)katika kila rakaa na humo ndani yake utakua umepata (Tasbih)(Tahmid)(Takbir)wa (Tahlil)na jumla yake utakuwa umepata hizo dhikr 300 kwa kila neno moja katika hayo manne utapata idadi mara 75.Amekua mwenye kufaulu mwenye kuipata sala hii kwa wingi kama alivosema Mollah wako katika sura ya (Nasr)فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُ‌ۚ إِنَّهُ ۥ ڪَانَ تَوَّابَۢا "Msabih Mollah wako mlezi,na umuombe msamaha,hakika yeye ndiye anaepokea toba" Alipokutana Bwana Mtume s.a.w na Sayyidna Ibrahim Khalil a.s katika mbingu ya saba Nabii Ibrahiim a.s alimwambia Bwana Mtume s.a.w "Nitolee salamu kwa umma wako wape habari waambie peponi kuna udongo mzuri, na maji yake masafi na matuta ya kupanda na mbegu zake ni (Subhanna-Allah)Wal-hamdulillah(Wallaillah-illah-Allah)Wallahu-Akbar. Mwenye-enzi-Mungu atujaalie tupate fadhila zake katika Ibada hii.

30 comments:

  1. Iyo sala mbona hujatoa ushahidi wa aya wa hadith ya mtume? Usiwadanganye wenzako.

    ReplyDelete
    Replies

    1. Rasulullah ﷺ is narrated to have said to his uncle Hazrat ‘Abbas (R.A):

      O Abbas! O my uncle! Shall I not give you a gift? Shall I not show you something by means of which Allah will forgive your sins, the first and the last of them, the past and recent, the unintentional and the intentional, the small and huge, the secret and open? The Holy Prophet ﷺ then taught him the Salah al-Tasbih. Furthermore he advised him that it be offered daily, if possible. If not, then every Friday or once a month or once a year or at least once in one’s life time. (Abu Dawood

      Delete
    2. Kwani ni Aya ipi iliosema "na tumieni simu"

      Delete
    3. Subhanallah Allah akusameh

      Delete
    4. kuna mijitu ujue kama mishenzi eti inataka ushahidi wa hii sala nawengine wanasema bidaa daah wew kama haikufai Acha kusali so lazima tunaotaka kua karibu na Allah tutasali maana ndani yake hakun maasiiiii

      Delete
  2. mbona nasikia swali hii ni bidaa na haifai kuswaliwa...?
    naomba uthibitisho wa hadithi au ayaa..?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani hio simu yako ina dalili au aya inayo kuruhiau kuitumia?

      Delete
  3. mbona nasikia swali hii ni bidaa na haifai kuswaliwa...?
    naomba uthibitisho wa hadithi au ayaa..?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza iyo bidaa unaijua , maana kila kitu ni bidaa sasa kama unataka visivyo vya bidaa sali sala 5 za faradhi , itoshe kwako, kwani unafaham maana ya uchawa wewe , hapa duniani watu wana machawa wao , wanajipendekeza kwao , basi iwe nongwa na makosa mtu kijikurubisha kwa mola wake na kujipe dekeza kwake kwa kufa ya maammalat ya kheri

      Delete
    2. Hao wanaotuambia kila kitu ni bidaa , ila wao tu mambo yao yote wayafanyayo ni sahihi na yameshiba ushahidi wa aya za qorani tukufu na sunna za Bwana Mtume Muhammad S.A.W , ndugu zangu hapa duniani tumeletwa kufanya ibada sasa wewe umeumbwa binaadam ukapewa akili sasa kama utaona ni dhambi kuamka usiku au ukaamua hata mchana kusali sala za sunna ukamuomba Allah kwa kumtukuza na kutubia madhambi yako , basi kaa ukilala

      Delete
  4. uongo mtupu kila kitu kwa dalili tunaomba dalili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kukata maneno tu tafta elimu kwanza usifate mkumbi mbona mtume hakuwahi kutoa khutba ya ijumaa kwa kiswahilI na leo mnatoa khutba kwa kiswahili

      Delete
  5. Nimeelewa vema kabisa salam alykum

    ReplyDelete
  6. Mbona mnawakusanya waumini uwanja wa taifa kwa mashindano ya kusoma qur an, na hamna ushahidi wowote? Acheni vurugu nyie wahabi tafuteni elimu, swala hii ya tasbih imethibiti

    ReplyDelete
  7. Sawa rakaa NNE unakweda mbili unatoa salami au unakwenda zote NNE bila ya salamu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unaenda mbili unatoa salam then unaenda tena mbili

      Delete
  8. Samahani shekhe naomba kujua rakaa ya mwisho ya wasoma atahiyatu kwanza ndiyo usome hizo tasbihi au tasbihi 10 kwanza Kisha usome atahiyatu?au atahiyatu haisomwi kabisa?

    ReplyDelete
  9. Asalaam alykum Warhamatullah Wabarakaatuhu. Naomba kuuliza katika rakaa ya pili na ya nne tasbih utaileta baada ya tahiyatt au kabla

    ReplyDelete
  10. Nami kwa mara ya kwanza na soma swala hii ya swalatu'tasbii asante nitajaribu Kadri nowezavyo kuiswali swallah hii

    ReplyDelete
  11. A alekum kila Suna vizuri kuswali

    ReplyDelete
  12. Utainuiaje hii swala kila baada ya salam

    ReplyDelete
  13. Anaetaka dalili ya swala ya tasbihi atafute mtu ampe maana ya aya hizi zifuatazo, surat kahfi aya 30, 88 na 110, surat hajji aya ya 77, surat bakara aya ya 277, surat an'aam aya 150 , surat nahli aya ya 30, surat aaraf aya ya 42, surat nisai aya ya 124, surat twaha aya ya 14, surat nisai aya ya 83, lakini akatafute mtu mwenye elimu ndo amtafsirie hizo aya asende akajisomea mwenyewe hapo atajua kama si kila kitu alichokua hajafanya mtume ni haram na mwisho nampa usia kila anaona kila kitu akasema ni haram aya yake ni 116 surat nahli

    ReplyDelete
  14. Asalam alaikum shekh wangu naomba kuuliza je muda Gani mzuri wa hii swala

    ReplyDelete
  15. mda mzul ni usiku wa manane kuanzia saa 00:00

    ReplyDelete
  16. Allah akulipe mema inshallah...
    lakini natamani zaidi kujuwa, yaani ifafanuliwe inasaliwa vipi kama hata zile mfano (RABBANAA WALAKALHAMDU) vipi ziwemo au ni tasbihi tu peke yake?
    Maana apo hakujafafanuliwa ni hadithi tu iyo. 🙂

    ReplyDelete
    Replies
    1. Assalamu alaykum, mi nauliza tunasema tu hizo tasbih pekee, hatusemi zile subhana rabbiyal aala, subhana rabbiyal adhwim, rabbana lakal hamdu, nk au mote tunasema tu tsbih basi na mwisho tunamalizia tu na attahiyatu basi? Ama?

      Delete
  17. Hiv unasifa zile subhan rabil adhimu au ndo unasom izo tasibh 2

    ReplyDelete