Tuesday, May 29, 2012
SALA YA TASBIH
Asalaam-Aleiykum
Ameagiza Bwana Mtume s.a.w tuipate sala hii ya tasbih ikiwa tutaweza basi tuisali kwa siku mara moja, Au kama hatuwezi basi iwe kila ijumaa na kama haiwezekani basi hata kwa mwezi mara moja, na kama hivo pia ni ugumu basi tufanye mwaka mara moja, na kama hatuwezi kabisa basi angalau katika umri wako uipate mara moja. Imekua Sala hii akiipata muumin basi husamehewa Dhanbi zake zote, kwanini ikawa hivo, kwa sababu hiyo ni sala pekee inoweza angalau kwa mara moja ukapata bahati ya kuipata hicho kitu kinachoitwa sala, kwa sababu ya shuruti za idadi ya hizo tasbih za dhikr zilizomo humo, hupati nafasi ya kufikiri Bank, au kuwaza nyimbo za tarab, au kukumbuka mambo yako ya mipira,Jaribu uipate utaona ladha ya sala hii.
Vipi inasaliwa?
Utasali Rakaa nne,na kila kwenye Rakaa Utasoma Suratil fatiha(Alhamdu)na sura nyengine yoyote ile uitakayo,utakapomaliza kusoma hali yakua bado umesimama utasema maneno haya(Subbhana-Allah-,Walhammdulillah-wallah-illah-illah-Allah-wallahu-Akbar)mara kumi na tano(15), Ikisha utarukuu utasema mara (10)halafu ukinyanyua kichwa kutoka kwenye rukuu utasoma mara (10),Ikisha utakwenda katika sijda utasoma mara (10)ikisha ukinyanyua kichwa kutoka katika sijda utasoma mara (10)Ikisha utasujudu tena utasoma mara (10)na ukinyanyua kichwa kutoka katika sijda utasoma mara(10)na hivo utakua umepata mara (75)katika kila rakaa na humo ndani yake utakua umepata (Tasbih)(Tahmid)(Takbir)wa (Tahlil)na jumla yake utakuwa umepata hizo dhikr 300 kwa kila neno moja katika hayo manne utapata idadi mara 75.Amekua mwenye kufaulu mwenye kuipata sala hii kwa wingi kama alivosema Mollah wako katika sura ya (Nasr)فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُۚ إِنَّهُ ۥ ڪَانَ تَوَّابَۢا
"Msabih Mollah wako mlezi,na umuombe msamaha,hakika yeye ndiye anaepokea toba"
Alipokutana Bwana Mtume s.a.w na Sayyidna Ibrahim Khalil a.s katika mbingu ya saba Nabii Ibrahiim a.s alimwambia Bwana Mtume s.a.w "Nitolee salamu kwa umma wako wape habari waambie peponi kuna udongo mzuri, na maji yake masafi na matuta ya kupanda na mbegu zake ni (Subhanna-Allah)Wal-hamdulillah(Wallaillah-illah-Allah)Wallahu-Akbar.
Mwenye-enzi-Mungu atujaalie tupate fadhila zake katika Ibada hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Iyo sala mbona hujatoa ushahidi wa aya wa hadith ya mtume? Usiwadanganye wenzako.
ReplyDelete
DeleteRasulullah ﷺ is narrated to have said to his uncle Hazrat ‘Abbas (R.A):
O Abbas! O my uncle! Shall I not give you a gift? Shall I not show you something by means of which Allah will forgive your sins, the first and the last of them, the past and recent, the unintentional and the intentional, the small and huge, the secret and open? The Holy Prophet ﷺ then taught him the Salah al-Tasbih. Furthermore he advised him that it be offered daily, if possible. If not, then every Friday or once a month or once a year or at least once in one’s life time. (Abu Dawood
Kwani ni Aya ipi iliosema "na tumieni simu"
DeleteSubhanallah Allah akusameh
Deletekuna mijitu ujue kama mishenzi eti inataka ushahidi wa hii sala nawengine wanasema bidaa daah wew kama haikufai Acha kusali so lazima tunaotaka kua karibu na Allah tutasali maana ndani yake hakun maasiiiii
Deletembona nasikia swali hii ni bidaa na haifai kuswaliwa...?
ReplyDeletenaomba uthibitisho wa hadithi au ayaa..?
Kwani hio simu yako ina dalili au aya inayo kuruhiau kuitumia?
Deletembona nasikia swali hii ni bidaa na haifai kuswaliwa...?
ReplyDeletenaomba uthibitisho wa hadithi au ayaa..?
Kwanza iyo bidaa unaijua , maana kila kitu ni bidaa sasa kama unataka visivyo vya bidaa sali sala 5 za faradhi , itoshe kwako, kwani unafaham maana ya uchawa wewe , hapa duniani watu wana machawa wao , wanajipendekeza kwao , basi iwe nongwa na makosa mtu kijikurubisha kwa mola wake na kujipe dekeza kwake kwa kufa ya maammalat ya kheri
DeleteHao wanaotuambia kila kitu ni bidaa , ila wao tu mambo yao yote wayafanyayo ni sahihi na yameshiba ushahidi wa aya za qorani tukufu na sunna za Bwana Mtume Muhammad S.A.W , ndugu zangu hapa duniani tumeletwa kufanya ibada sasa wewe umeumbwa binaadam ukapewa akili sasa kama utaona ni dhambi kuamka usiku au ukaamua hata mchana kusali sala za sunna ukamuomba Allah kwa kumtukuza na kutubia madhambi yako , basi kaa ukilala
Deleteuongo mtupu kila kitu kwa dalili tunaomba dalili
ReplyDeleteAcha kukata maneno tu tafta elimu kwanza usifate mkumbi mbona mtume hakuwahi kutoa khutba ya ijumaa kwa kiswahilI na leo mnatoa khutba kwa kiswahili
DeleteNimeelewa vema kabisa salam alykum
ReplyDeleteMbona mnawakusanya waumini uwanja wa taifa kwa mashindano ya kusoma qur an, na hamna ushahidi wowote? Acheni vurugu nyie wahabi tafuteni elimu, swala hii ya tasbih imethibiti
ReplyDelete👍jibu mujarrab
DeleteSawa rakaa NNE unakweda mbili unatoa salami au unakwenda zote NNE bila ya salamu
ReplyDeleteUnaenda mbili unatoa salam then unaenda tena mbili
DeleteSamahani shekhe naomba kujua rakaa ya mwisho ya wasoma atahiyatu kwanza ndiyo usome hizo tasbihi au tasbihi 10 kwanza Kisha usome atahiyatu?au atahiyatu haisomwi kabisa?
ReplyDeleteUnasoma tahyatu tu
DeleteJazākAllāh
ReplyDeleteAsalaam alykum Warhamatullah Wabarakaatuhu. Naomba kuuliza katika rakaa ya pili na ya nne tasbih utaileta baada ya tahiyatt au kabla
ReplyDeleteNami kwa mara ya kwanza na soma swala hii ya swalatu'tasbii asante nitajaribu Kadri nowezavyo kuiswali swallah hii
ReplyDeleteA alekum kila Suna vizuri kuswali
ReplyDeleteUtainuiaje hii swala kila baada ya salam
ReplyDeleteAnaetaka dalili ya swala ya tasbihi atafute mtu ampe maana ya aya hizi zifuatazo, surat kahfi aya 30, 88 na 110, surat hajji aya ya 77, surat bakara aya ya 277, surat an'aam aya 150 , surat nahli aya ya 30, surat aaraf aya ya 42, surat nisai aya ya 124, surat twaha aya ya 14, surat nisai aya ya 83, lakini akatafute mtu mwenye elimu ndo amtafsirie hizo aya asende akajisomea mwenyewe hapo atajua kama si kila kitu alichokua hajafanya mtume ni haram na mwisho nampa usia kila anaona kila kitu akasema ni haram aya yake ni 116 surat nahli
ReplyDeleteAsalam alaikum shekh wangu naomba kuuliza je muda Gani mzuri wa hii swala
ReplyDeletemda mzul ni usiku wa manane kuanzia saa 00:00
ReplyDeleteAllah akulipe mema inshallah...
ReplyDeletelakini natamani zaidi kujuwa, yaani ifafanuliwe inasaliwa vipi kama hata zile mfano (RABBANAA WALAKALHAMDU) vipi ziwemo au ni tasbihi tu peke yake?
Maana apo hakujafafanuliwa ni hadithi tu iyo. 🙂
Assalamu alaykum, mi nauliza tunasema tu hizo tasbih pekee, hatusemi zile subhana rabbiyal aala, subhana rabbiyal adhwim, rabbana lakal hamdu, nk au mote tunasema tu tsbih basi na mwisho tunamalizia tu na attahiyatu basi? Ama?
DeleteHiv unasifa zile subhan rabil adhimu au ndo unasom izo tasibh 2
ReplyDelete