Asalaam Aleiykum,
Uhusiano wako na mama yako mpaka leo unabaki miujiza ambayo hatuwezi kutambua undani wake, kwanza kabisa huyu Mama akizaliwa tu anakuja na mayai yake kamili ndani ya tumbo lake, na katika mayai hayo moja wapo ndio hilo lilo kuzaa wewe, jee mapito yako kwa mama huyu ni bahati au kitu kilichopangwa?Kaa ufikiri kadhia hii halafu ujue kwanini ikatokea hivyo, mtizame Mama yako kwa jicho la huruma ujue kutokana na kudra ya Mwenye-enzi-Mungu yeye karidhia sababu ya uhai wako ianzie kwenye kiwili wili chake, yuko tayari achukue machungu yote na taabu zote ili na wewe upate ladha hii ya maisha ya kidunia.
Na muujiza mwengine ambao unadumu mpaka ya wawili nyie kuondoka katika Ulimwengu huu ni ule unao anzia tumboni katika kiunganishi chako wewe na Mama yako yaani kwenye (kitovu)Hapo katika miezi yote tisa yakuumbwa kwako ndio unapata huduma ya uhai wako, zinapita hapo (Electric-Transfer)baina yako na mama yako, ikawa aanchokila na wewe unapata faida zake, akihema kwa kupokea nguvu za uhai na wewe unapata kuishi(Umo tumboni umelala masaa ishirini na nne)kila kitu unafanyiwa, nje kukitokea msuko suko na wewe unashtuka mule ndani, kila kitu kimeambatana na Mama yako huku wewe umetulia unaendelea kuumbwa, na kila hatua ya kuumbwa kwako basi matatizo,magonjwa na shida zote zinamfika Mzazi wako huku yeye anastahamili na kumuomba Mwenye-enzi-Mungu "Ewe Mollah wangu nijaalie nikitoe kiumbe hichi kwa salama, hayo ndio maombezi ya Mama kwa mwanae ambae hata hajamuona au hamjui atakua kiumbe wa aina gani?.
Mapenzi ya Mama yanaanzia ungali tumboni, na inapotimia miezi tisa unazaliwa na kitu cha mwanzo kinofanyika unapewa uhuru wako ili uweze kuishi mwenyewe unakatwa ile(Life-support)Kitovu ,ile kamba ya uhai ikisha katwa baina yako na Mama yako sio mwisho wa wewe kumuhitaji Mzazi wako, ila baada ya muda mfupi tu una muhitaji huyu Mama aendelee kukupa huduma hii ya Uhai ili upate kuishi, hapo tena mahusiano ya tumboni yamekatika yanaanza ya kwenye (Kifua)kunyonyeshwa.Unaendelea kuwa muhitaji, unaendelea kumtegemea Mama takriban kwa miaka miwili au karibu na hapo, Na kama Mama atakua katili au hana huruma au ujana unamtesa akakudhulumu kukunyonyesha katika kipindi hichi basi maisha yako yote yatakua na matatizo ya hapa na pale kuhusiana na mapenzi au mahusiano yako na watu wengine.
Lakini Mama mwema ni yule apendaye kumnyonyesha mwanae na huku akimuombea Taufik kwa Mollah wake,Mjaalie mwanangu akue bila ya matatizo mpe afya njema na lau kama Mama huyu ataulizwa ghafla baina yako na mwanao nani unataka afe mwanzo, basi bila ya kusita au kujishauri atasema bora afe yeye ili huyu mtoto abaki.
Nani kama Mama? Huyu ndie leo wewe mtoto eti unaomba atakufa lini, mbona anateseka na anakutesa na wewe.Huyu ndie Mama mwenye kupokea machungu yote unayomletea au yanayokupata, huyu ndie mama mwenye kukupa mapenzi bila ya masharti yoyote.Huyu ndie Mama mwenye kusamehe kabla hata hujaomba hiyo samahani, Wallahi hakuna shaka ya mapenzi yako isipokua mfano wa miujiza,Hata watu wote wakikuchukia yeye anabakia kukupenda,yuko radhi akae na njaa ili upate kula wewe,yuko tayari akae macho ili wewe upate kulala,"wewe Mama mimi nikiumwa wewe unahangaika usiku kucha huku watu wote wamelala", uko radhi uteseke ili mimi nifurahi, wewe ndie unaenijua naumwa nini wakati hata siwezi kujieleza,Na sifa yako nyengine halipungui penzi lako hata tukiwa kumi unatupenda sote katika hali ilo sawa.
Nani kama Mama?endelea part-3
No comments:
Post a Comment