Asalaam Aleiykum,
Jaribu kujikumbusha mfano huu wa kugundua au kupata(Uamsho)unapokua mzima wa afya hushughuliki na mguu wala mkono, hupati tabu ya kukumbuka meno wala masikio lakini wacha kimoja katika viungo hivo vipate maradhi utaona hapo (Attention)yote Akili yote inahamia hapo, deko lote linakuwepo hapo kwenye huo mguu, umeshapata kujiuliza kwanini? tega jicho uzuri tupo katika kuuchambua Moyo tupate siri zake ili tujue vipi tuna(Falling in love)vipi tunapata hisia, inakuaje mahusiano haya na hii jinsi yangu mimi mwanaadamu, nini habari ya kipande hichi changu cha nyama kilichopo kwenye kifua changu.
Mcha Mungu kagundua Moyo ni chombo cha mawasiliano ya njia ya (Communion)inapata mawasiliano yake (Direct)au(Pure)mawasiliano haya iwe yanatokea huko kusikojulikana au hapa Ulimwenguni, yawe ya siri au dhahiri chombo hichi kina uweza wa kuya hifadhi iwe kwa kuona au kusikia.Ndio utaona Bwana Mtume s.a.w akaambiwa katika sura ya (Najm)"مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ""Moyo haukusema uongo (Kwa)uliyoyaona".
Kwani na wewe kuna mengi unayaona huwezi kuyakataa, hebu tizama Mfano huu wa mtoto mdogo, Analia, Anacheka ana hamaki na Akili yake bado haijakua, vitu hivyo vimetokea wapi, hakuna pengine isipokua Moyoni, hapo ndipo panapo kaa mapenzi, hisia, chuki, hamaki,furaha na imani na chochote kile kilicho husiana na hiyo (Communion)ndio maana utaona mfano huu kama una mgonjwa una uguza umekaa naye siku zote anapo kufa wewe wa karibu huzuni zako haziwi sawa na yule aliye mbali, kwa aliye mbali akiwasili anakua na huzuni kubwa sababu ya hiyo (Communion)ndio maana walimwengu wakasema unacho kitia moyoni taabu kukitoa, ndio Mcha Mungu akasema "nilipogundua katika huu Moyo wangu kumbe anaweza kukaa asiye kuwa wewe" mkapewa mfano katika Quraan vipi kitu kinaweza kuingia kikenda kukaa moyoni ili iwe alama kwenu.Quraan Aaraf-204,
" وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ"
"Na Ikisomwa Quraan isikilizeni, Nyamazeni ili mpate kurehemewa". hapo yametajwa mambo mawili la kwanza kusikiliza na la pili kunyamaza,Isikilizeni ili ipate kuingia kwenye moyo, usizungumze kwani ukizungumza haitokaa moyoni ipe nafasi itulie, ulipoambiwa nyamaza sio kwenye Akili unaendelea kuzungumza utakosa faida ya huko Kurehemewa, na kusudio la kurehemewa hapo ni hilo la (Uamsho), hivo wewe hujawahi kutengeneza kitu, au unafanya mtihani, au umeulizwa swali hujui jawabu lake umekaa una fikiri halafu ghafla linakujia jawabu, limetokea wapi, "Nilipojua katika huu Moyo wangu anaweza kukaa asiye kuwa wewe"hiyo ndio maana ya sikizeni na nyamazeni kimya yakiingia maneno ya Quraan katika nyoyo zenu yaka kaa basi tena hugeuka Imani na huko ndiko kurehemewa kuna patikana kwa njia ya sauti.
Endelea-part-4
No comments:
Post a Comment