Asalaam Aleiykum.
furaha ilioje ukipata nafasi ya kuyasikia maneno ya Mcha Mungu hasa wakati kama huu umemaliza siku za furaha za Eid-Adh haa, Anasema nini Mcha Mungu.
"Nilipojua kwamba katika Moyo wangu kuna uwezekano wa kukaa asiye kuwa wewe Mollah wangu, Basi nilifanya mimi jitihada na mashindano makubwa ili kuhakikisha kuwa haingii akakaa mwengine yoyote asiye kuwa wewe Mollah wangu, niliendelea mimi kuujaza Moyo wangu uongofu wa kila jambo utokao kwako hata ikawa haikubakia nafasi yoyote ya kukaa asiye kuwa wewe Mollah wangu".
Anasema Mcha Mungu nilipojua au nilipogundua au uliponijia mimi (Uamsho) katika moyo wangu kwamba kuna uwezekano wa kukaa asiye kuwa wewe, hapo nilianza kufanya jitihada kubwa nilishindana sana kwa ajili yako Mollah wangu ili asije kuingia yoyote yule Moyoni mwangu, Katika maneno haya kuna siri kubwa Mcha Mungu anataka kutupa na sisi faida ili tupate huo (Uamsho)litutoke lepe lepe la usingizi ili tusikubali tena kumpisha kila ajae kukaa katika Mioyo yetu.
Nini maana ya neno Uamsho?
Katika matumizi ya lugha ya Wacha Mungu neno hili kama mengine yote yana maana mbili, Maana ya kwanza ni ile inotumika katika sauti za kila leo kama vile ukiambiwa Uamsho, wewe utafasiri kwa maana nyingi tu unavopenda, labda umelala umekuja kuamshwa, Pengine unaamshwa ukale daku mwezi wa Ramadhan, au tafsiri nyengine kuwa kuna watu washaamka na sasa wanakuamsha na wewe pengine unadhulumiwa au unatawaliwa na shetani wanakuzindua, sasa basi tena kutawaliwa simama udai haki yako, wote huo unaweza kuita Uamsho, hiyo ni maana ya nje ya Uamsho. Ama katika maana ya ndani ya Uamsho inakua kama alivoitaja Mcha Mungu nilipojua (Awaken) vipi inakua muamko huu? Mfano utaupata katika usingizi wako wa kawaida, hebu jichunguze vipi inakua pale mwanzo ukiamka asubuhi, jitahidi usifungue macho utaona kitu cha mwanzo kinacho kujia ni (Awareness)kujijua mie nishaamka hapo hujijui mie fulani babaake fulani au mie fulani mke wa fulani, habari hizo hufatia baadae.
Kitu cha mwanzo kukushukia ni elimu ya kujijua mie ni macho na hapo Mcha Mungu husema (Alhamdullillah)ukitulia katika hali hiyo ndio utagundua kumbe kuamka ni (Process)kama vile inavoingia Alfajiri au Magharib, ndio Mcha Mungu akasema "(Nilipogundua kumbe katika moyo wangu anaweza kukaa asiye kuwa wewe)"na ukitaka kujua vipi anakaa asiye kuwa wewe basi ukiliacha lile sharti la usifungue macho, ukaja ukayafungua hapo utaanza kuona mtiririko wa asiye kuwa yeye unavo miminika, zinaanza kuingia (Information)zote unasahau hata kama ulikua umelala, unaanza kukumbuka viporo vyote ulobakisha jana, basi kabla hujaamia katika hizo kumbukumbu kitu cha mwanzo kinacho kujia ni hiyo elimu ya kujua, na huo ndio Uamsho, ambao watu wengine wanautilia mkazo tu ili usije ukalala tena au ukaja kulazwa, sasa ufanye nini endelea part 2 ujue taaluma hii ya uamsho inaishia wapi.
No comments:
Post a Comment