Asalaam Aleiykum,
Nini cha kufanya mpaka urejee katika hali ya kawaida, Unatakiwa uwe tayari na ujitaarishe kumeza kidonge ambacho ukikimeza tu, kinaanza kazi yake ya kukuponesha, na unakipata kidonge hicho kwenye Quraan sura ya Hashir aya ya 18 na 19.
يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡتَنظُرۡ نَفۡسٌ۬ مَّا قَدَّمَتۡ لِغَدٍ۬ۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ
"Enyi Mloamini Mcheni Mwenye Enzi Mungu, Na kila Mtu aangalie, (Atizame)(Be Witness)anayoyatanguliza kwa ajili ya kesho, Na Mcheni Mwenye Enzi Mungu, Hakika (Yeye)anazo habari za mnayoyatenda"
Imetajwa kumcha Mungu kwenye aya hiyo mara mbili, Mara ya kwanza ni kuzinduliwa kuwa umeze kidonge cha Ucha Mungu, halafu uwe Shahidi kwa matendo yako, moja baada ya moja, kwa ajili ya kesho(Akhera)na kesho hapa hapa duniani utizame (Chain of Reaction)ukifanya sasa hivi tizama baadae itatokea nini(Be Witness)utajua kinatokea nini, Na ukianza kutizama matendo yako kidogo kidogo Dhiki inapotea kwani hiyo Dhiki imeingia moyoni kwako baada ya kugundua upo (Empty)nafasi iwazi.
Na kutajwa mara ya pili kuwa ukianza Kumcha Mollah wako ukawa shahidi wa vitendo vyako, Dhiki inapotea kwa ajili hutendi maovu, na kila wakati unakua kwenye kuelewa Mollah wako ni mwenye kukuona na hiyo ndio (Taqwa), na hicho ndio kitu kinachopungua katika maumbile yako, na kikipungua tu, unakaribisha Dhiki ikutawale ndio maana ukaambiwa kwenye aya inayofatia.
وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ نَسُواْ ٱللَّهَ فَأَنسَٮٰهُمۡ أَنفُسَہُمۡۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡفَـٰسِقُونَ
"Wala msiwe kama wale walomsahau Mwenye Enzi Mungu, Na (Mwenye Enzi Mungu)Akawasahaulisha Nafsi zao, Hao ndio waasi wakubwa"
Kumsahau Mwenye Enzi Mungu ndio huko kukaribisha matendo ya Dhiki, Na ukimsahau Mwenye Enzi Mungu na yeye anakusahaulisha kuwa yeye yupo na dawa yako ya hiyo Dhiki ni Ucha Mungu, Nafsi inasahau kabisa ndio unaendelea kuteseka na unazama katika Bonde la maasi, usijione mbona mimi nasali na Dhiki bado ninazo,(No)Mwenye Enzi Mungu kakupa (Challenge)jitizame wewe Una Sali au unafanya mazoea(Hata kasuku akizoea Ata sali)itizame Sala yako kweli unaipeleka ipasavyo.
Basi hichi kidonge cha kwanza utakunywa kutwa Mara 5 nacho hicho cha (Taqwa), ukiitia moyoni mwako ukaitenda kwa (Ikhlasi)basi utakua ushaanza kupata ponesho la Dhiki, kwa Sababu penye Taqwa Dhiki haikai. Sasa kwanini inakaa? Sababu hitajio lako kubwa ni Taqwa, na wewe hilo umelitupa hulitaki, unalichukia au kama unafanya kwa ajili umemsikia Sheikh fulani kautaja Moto, na wewe unauogopa ndio unaanza kusali, lakini hupeleki Sala yako kwa ajili ya mapenzi ya Mollah wako, nakupa mfano huo ulotajwa utazame matendo yako hapo juu, jitizame ukitoa sadaka au kumsaidia mtu wewe unafanya kwa ajili gani, la kwanza utagundua hufanyi kwa ajili ya Mollah wako sababu kwenye moyo wako hakuna linalotokezea, la Pili utaelewa unafanya kwa ajili ya kitu fulani, na la Tatu hakuna Hisia unafanya (Empty Heart)Na ukiona hivyo elewa Dhiki imejificha kwenye moyo wako, ndio maana Bwana Mtume s.a.w akaashiria mara tatu kwenye kifua chake na kusema (Taqwa)ipo humu, Nenda Moyoni ukagundue kinatokezea nini ili upate jawabu lako.
Na ukiipata Taqwa hapo unapewa kidonge cha Pili cha siri bila mwenyewe kujua unaona Dhiki imetoweka umekua mja wa furaha, ukiona Ndege anaimba wewe unacheka na dawa yenyewe ni hii (Alam-Nashrah aya ya 5)
فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا
"Basi Hakika baada ya Dhiki Faraji"
Faraji ndio maumbile yako, usikubali kabisa kuishi kwenye Dhiki, hama utoke kwenye Dhiki uende kwenye Taqwa, ukutane na faraj, faraji ndio afya, faraj ndio mapenzi, faraj ndio (Nature) yetu, usikubali kinyume cha hayo, Na Mollah wetu atatusaidia kuipata Faraj.
No comments:
Post a Comment