Asalaam Aleiykum,
Baada ya kusoma sifa za Majina ya Mwenye Enzi Mungu nimeona kuna haja ya kurejea katika Darsa zetu za kawaida ili tuendelee kupata faida za kawaida za matunda ya dini yetu, leo hii tunaitizama Ihsan na fadhila kubwa tuloipata katika dini ya Kiislam kutoka kwa Mtume s.a.w pale alipo wacha kumchagua kiongozi wa kuindeleza Dini hii, alijua hii Dini ya Haki na italindwa na Mwenyewe alomtuma kuufikisha ujumbe huu, isionekane kwamba hakufanya uteuzi laa, alifanya uteuzi lakini ulikua wa Kisiasa kwani yeye alikua ni Mjumbe wa Mwenye Enzi Mungu na pia Mkuu wa Dola ya Kiislam, kama Mkuu wa Dola na kiongozi wa Waumini aliteua Magavana(Governor), lakini kwa upande mwengine kama Mjumbe wa Mwenye Enzi Mungu alikaa kimya na hivyo ndio walivofanya Wajumbe wote kabla yake.
Hakuchagua Khalifa au huyu awe Sheikh wenu, Hakuchagua Mchungaji wala kuwepo na Muangalizi, ila yeye alipewa na kufahamishwa maneno na Mwenye Enzi Mungu kuwajulisha Umma wake yakwamba Dini ni (Indivisual)mtu pekee, huna haja ya kushikiwa dini yako, na kama utayafahamu maneno hayo (In-deep understanding)basi kuanzia leo hutotaka mtu yoyote awe Sheikh wako au kuwa Imam wako, yatosha wewe Mwenyewe kuifanya kazi hiyo, na wala usitafute mtu wakukusomea dua na hivi na vile.
Utayafanya Maombi hayo kwa uchache au kwa wingi bila ya kutegemea yoyote, lakini cha msingi mpaka haya maneno yapasue akili yako huku ukiambiwa(Babu jinga inama ufikiri dini yako unashikiwa), kabla ya kuyagusa maneno hayo(Adhimu)Naomba nikumbushe kitu kuhusiana na Mtume s.a.w alivokua anapenda Usawa, Haki, na Uongofu, ndio mpaka leo ukaona wale alokua nao pamoja wakati ule hawakuitwa wanafunzi wake, au wafuasi wake bali walikuwa wakiitwa (Masahaba zake)Marafiki zake.
Nani Rafiki?
Rafiki ni mtu ambaye yuko karibu na akishirikiana na wewe katika mahusiano ya kiroho, Ikiwemo furaha na Misiba, kwenye shida na Raha zote, Rafiki ni Mwenye kukushauri katika mambo yote ya wema, na hana shaka wala wasiwasi juu yako kwenye jambo lolote la Ukweli, Kinyume na hayo anza kutilia wasiwasi Urafiki wenu.
Sasa twende tukahudhurie hayo maneno aloteremshiwa Bwana Mtume s.a.w ili tupate kujua vipi na wewe utakua Sheikh, wacha leo tuondoshe Viburi vya wale wanodhani Dini ni Mali yao, wacha tuwafichue wale wanotumia migongo ya wenzao kuwapanda na kuwadanganya na kuwadharau wenzao, kuendelea kuwabagua na kuwatenga, kuzidi kuwalaza ili wapate kuonekana wao ndio wenye kujua na wanayo mamlaka kamili ya uwezo wa kumpeleka mtu peponi, na maandalizi yote wanayo wao, napenda uelewe katika Uislam hakuna kitu kama hicho,na ukimgundua mtu ana nyendo kama hizo basi mkimbie haraka sana.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment