Asalaam Aleiykum,
Unaijua tafauti baina ya Furaha na Raha, vishawahi kukuta viwili hivi kwa wakati mmoja? Na kama huijui basi zinduka usingizini uelewe kuwa viwili hivi umbali wake kama Shamba na mjini, upeo wake mkubwa na inatakiwa kazi (Ya Ndovu na Mwanae)kuvikutanisha viwili hivi, Ikiwa Mja mwenye kutaka kufahamu na kutaka kujua ili unufaike kwa kuvipata vitu hivi viwili kwa wakati mmoja basi tuliza fahamu yako ili unufaike na darsa hii ya kukujulisha tafauti baina ya Raha na Furaha.
Kwanza kabisa napenda kukujulisha kwa hali ulokua nayo sasa hivi ni vigumu kabisa kutafautisha nini Raha na nini Furaha, kwa hali ulonayo, inapokaa Raha furaha haionekani, vigumu Furaha kukufikia, na Inapokuwepo Furaha unakuwa ushaisahau Raha ndio maana Furaha ikimalizika unateseka sababu ni vigumu kwako kurejea katika hali ya Raha. Ukitaka kuyaelewa kwa uzuri mambo haya kwanza wacha nikuchukue katika Mji wa Furaha nikuoneshe mambo yake halafu nikupeleke kwenye mji wa Raha pia Ukashuhudie kukoje, halafu utaamua mwenyewe unataka kuishi katika Mji gani.
Hivi karibuni katika ziara zangu za nyumbani katika mji wa Mrima vijana waliniuliza swali niwape tafauti ya Raha na Furaha, Nikaanza kuwajibu kwamba Furaha ni kitu cha (Temproray)chenye kupita au kina kuja mara moja na kutoweka, hakidumu, na wewe ukichunguza utayagundua hayo, Furaha ni yenye kukaa kwenye Akili kwa muda, kwani si ushawahi kufanya harusi na ukiamka furaha zimekwisha, ukinunua kitu ukawa nacho muda mdogo tu furaha imekwisha, ukimuona rafiki yako wa siku nyingi unafurahi baada ya muda furaha imekwisha, iko mifano mingi furaha inavopita katika akili zetu kwa muda mchache, na zikitoweka furaha hizo tunakuwa wateja wakuzitafuta tena na tena mpaka
tunasahau kuwa sisi tuna kitu muhimu tunacho ishi nacho nayo ni hiyo Raha ambayo mtu anatakiwa kwenda (Beyond)ili kuigundua tena hiyo Raha.
Kutaka kwenda kuigundua hiyo Raha itakubidi uteremke Bondeni, utoke juu Akilini uteremke taratibu moyoni kwenye raha za kudumu.
Endelea part 2 ujue nini Raha
No comments:
Post a Comment