Asalaam Aleiykum
Hakika mbora wenu Mbele ya Mwenye Enzi Mungu ni yule Mwenye vitendo vya Mapenzi juu ya Mollah wake, ni yule mwenye Mapenzi na Mollah wake(Taqwa)Na Ukimpenda Mollah wako unakua si mwenye kumsahau hata dakika moja, na hiyo ndio alama kubwa ya mapenzi ya Mwenye Enzi Mungu, na ikiwa kweli umefika katika daraja ya Mcha Mungu basi kwenye masaa 24 isikupite hata dakika kumsahau Mollah wake, na ukishindwa kufanya hivyo basi wewe umo tu kwenye kundi la wale wenye kujitahidi.
Utakapofikia Daraja hiyo basi jua hakuna Sheikh kama wewe, hakuna Imam kama wewe, lakini ikiwa kinyume na hayo jijue wewe bado na wacha kuwapumbaza wenzako, wacha kuwapa (Boarding Pass)za pepo ya uongo wenzio, unafanya jambo la hatari litakuangamiza, Kwani aliye kipenzi cha Mwenye Enzi Mungu ni yule Amchaye, na Mcha Mungu wa kweli ndio huyo mwenye kuishi na huo ukweli, ambaye keshakutana na mambo ya Mwenye enzi Mungu, kashaoneshwa Taa ya Mollah wake ambayo inamuongoza akiwa sokoni yeye yupo na Mollah wake, akiwa darasani yuo na Mollah wake, akiwa na family yupo na Mollah wake, akiwa kwenye halaiki za siasa yupo na Mollah wake, kila aendapo yeye ni mwenye Kumkumbuka Mollah wake, huku anakua kavaa taji la sifa ya upole na ukarimu, si mwenye kumbagua yoyote, unapomkuta Wallahi utaona Nuru ya Rahiim inammurika, huyo ndio anofaa kuwa Mwalimu wenu, huyo ndio anofaa kuwa Sheikh wenu, kuwa Imam wenu, kuwa kiongozi wenu, kinyume na hivyo itakua nyote mnapotea.
Hakika Mwenye enzi Mungu ni mjuzi(Wa hayo yote)na ni mwenye habari zote, anakujueni mnavopanga mipango yote ya njama za kujiona nyinyi bora, anafahamu mbinu zenu za kutaka kuwashikia wenzenu dini yao, eti dua lazima uombe wewe ndio iwe kubuli, hakuna kabisa kitu kama hicho katika Uislam.hakuna mwenye kuijua siri hiyo katika dini ndio katika aya ya (11 ya sura hiyo hiyo ya Hujurat)Inasema,
يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَسۡخَرۡ قَوۡمٌ۬ مِّن قَوۡمٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُونُواْ خَيۡرً۬ا مِّنۡہُمۡ وَلَا نِسَآءٌ۬ مِّن نِّسَآءٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُنَّ خَيۡرً۬ا مِّنۡہُنَّۖ وَلَا تَلۡمِزُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَلَا تَنَابَزُواْ بِٱلۡأَلۡقَـٰبِۖ بِئۡسَ ٱلِٱسۡمُ ٱلۡفُسُوقُ بَعۡدَ ٱلۡإِيمَـٰنِۚ وَمَن لَّمۡ يَتُبۡ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Enyi Mloamini Wanaume wasiwadharau Wanaume wenzao,Huwenda wakawa bora kuliko wao, Wala Wanawake wasiwadharau Wanawake wenzao, Huwenda wakawa bora kuliko wao,(Na)Wala msitukanane kwa Kabila, wala msiitane kwa majina mabaya,(Na)Jina Baya kabisa kuambiwa Mtu ni asi baada ya kuwa ni Muislam,(Na kufanya hivyo ni Dhanmbi)Na wasotubu basi hao ndio Madhalim,(Wamedhulumu nafsi zao kwa kuipinga amri ya Mollah wao).
Kama mna Imani ya kweli, basi sikieni maneno ya Mollah wenu, na kama husikilizi kaa peke yako ujiulize wewe uko kundi gani?Basi ikiwa unaendelea kumsikiliza Binaadamu mwenzako hilo ni shauri lako, Na huenda hao mnaowadharau mkawaona sio Masheikh wakawa bora kuliko nyinyi, Na wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao huwenda wakawa bora kuliko wao, wala msitukanane kwa kabila, au kikundi fulani wakajiona sisi bora kuliko wale, yote hayo ni maneno msihadaike na maneno hakuna anojua yupi bora, hakuna anoshushiwa (Wahyi)akaambiwa nyinyi ndio mnokwenda Peponi yote hayo ni maneno, usikubali kuyumbishwa na maneno mazuri, kumbuka nyuma ya maneno mazuri kuna ubaya ulojificha, fanya uchunguzi utalijua hilo.
Na hakuna jina baya kama ukipita ukamtangazia mwenzio yule asi, yule si Sheikh, yule kafiri, yule jinsi kadhaa wa kadhaa, ikiwa unayatenda hayo basi jijue wewe mwenyewe ndio asi mkubwa na unataka dawa ili upone, na wala usifikiri huo ni Ucha Mungu, huko ni kuingia hasarani, na unatakiwa utoke kwenye kundi hilo na utubu kwa dhanmbi zako hizo, Rejea kwa Mollah wako Uwe Mcha Mungu upate daraja ya watu wema, Uwe katika watendao mazuri, upate cheo cha hakuna Sheikh kama wewe, hakuna Imam kama wewe, na hicho ndio cheo kikubwa kukipata hapa Ulimwenguni, Na hicho ndio cheo cha Ucha Mungu ambacho sote tunatakiwa tupigane kukipata, na ukisha kukipata wewe utakua umeipata Nuru ya Mwenye enzi Mungu, lakini hivi sas kwa wakati huu bado umo kwenye kuiona Taa, ondoka katika taa ukaione Nur -ala-Nur, Na hayo ndio mafanikio makubwa ambayo sote tunayataraji kuyapata.
Tunamuomba Mollah wetu atuwezeshe kuipata Nur yake.
No comments:
Post a Comment